Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 11.7
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.Luc 22.39-22.45 Luc 9.18 Psaumes 10.17 Jude 1.20 Luc 6.12
2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.]Ecclésiaste 5.2 Matthieu 6.6-6.15 Psaumes 11.4 2 Chroniques 20.6 2 Thessaloniciens 1.1-1.2
3 Utupe siku kwa siku riziki yetu.Matthieu 6.34 Proverbes 30.8 Matthieu 6.11 Esaïe 33.16 Jean 6.27-6.33
4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni [lakini tuokoe na yule mwovu].Matthieu 26.41 Matthieu 6.12-6.15 Luc 22.46 Matthieu 18.35 1 Corinthiens 10.13
5 Akawaambia, Ni nani kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafiki yangu, nikopeshe mikate mitatu,Luc 18.1-18.8
6 kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; 7 na yule wa ndani amjibu akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa, nasi tumelala kitandani mimi na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe?Luc 13.25 Galates 6.17 Luc 7.6 Matthieu 25.10
8 Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.Luc 18.1-18.8 Matthieu 15.22-15.28 Colossiens 4.12 Romains 15.30 Genèse 32.26
9 Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.Marc 11.24 Jean 16.23-16.24 Matthieu 21.22 Jean 15.16 Jean 15.7
10 Kwa kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.Jacques 5.11 Psaumes 31.22 Jacques 4.3 Lamentations 3.18 Lamentations 3.54-3.58
11 Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe au samaki, badala ya samaki atampa nyoka?Matthieu 7.9 Esaïe 49.15
12 Au akimwomba yai, atampa nge?Ezéchiel 2.6 Luc 10.19 Apocalypse 9.10
13 Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?Matthieu 7.11 Jean 4.10 Romains 8.32 Ezéchiel 36.27 Romains 7.18
14 Naye alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu.Matthieu 9.32-9.34 Marc 7.32-7.37 Matthieu 12.22-12.24
15 Wengine wao wakasema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo.Matthieu 9.34 Matthieu 10.25 Jean 10.20 Jean 8.52 Jean 8.48
16 Wengine walimjaribu, wakimtaka ishara itokayo mbinguni.1 Corinthiens 1.22 Marc 8.11-8.12 Jean 6.30 Matthieu 16.1-16.4 Matthieu 12.38-12.39
17 Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka.Matthieu 9.4 2 Chroniques 10.16-10.19 Matthieu 12.25-12.29 2 Chroniques 13.16-13.17 Esaïe 9.20-9.21
18 Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli.Matthieu 12.26 Luc 11.15 Matthieu 12.31-12.34 Jacques 3.5-3.8 Matthieu 4.10
19 Basi, kama mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu.Luc 9.49 Matthieu 12.27-12.28 Luc 11.31-11.32 Matthieu 12.41-12.42 Romains 3.19
20 Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia.Exode 8.19 Luc 10.9 Luc 10.11 Matthieu 3.2 Actes 28.23-28.28
21 Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama;Marc 3.27 Matthieu 12.29
22 lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.Esaïe 49.24-49.25 Esaïe 53.12 1 Jean 3.8 Apocalypse 20.1-20.3 Colossiens 2.15
23 Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutawanya.Matthieu 12.30 Luc 9.50 Marc 9.40 Apocalypse 3.15-3.16
24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema,Psaumes 63.1 Matthieu 12.43-12.45 Job 1.7 Job 2.2 1 Pierre 5.8
25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka.Matthieu 12.44-12.45 2 Pierre 2.10-2.19 Psaumes 81.11-81.12 2 Thessaloniciens 2.9-2.12 Jude 1.8-1.13
26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.Jean 5.14 2 Pierre 2.20-2.22 Hébreux 6.4-6.8 Jude 1.12-1.13 1 Jean 5.16
27 Ikawa alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya.Luc 1.42 Luc 23.29 Luc 1.48 Luc 1.28
28 Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.Luc 8.21 Luc 6.47-6.48 Jacques 1.21-1.25 Esaïe 48.17-48.18 Matthieu 7.21-7.25
29 Na makutano walipokuwa wakimkusanyikia, alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona.Luc 11.16 Marc 8.11-8.12 Luc 12.1 Matthieu 12.38-12.42 Marc 8.38
30 Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki.Jonas 1.17 Jonas 2.10 Jonas 3.2-3.10 Matthieu 12.40-12.42 Luc 24.46-24.47
31 Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani.2 Chroniques 9.1 1 Rois 10.1-10.13 Hébreux 11.7 Romains 2.27 Matthieu 12.42
32 Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.Hébreux 7.26 Jonas 1.2-1.3 Jonas 3.5-4.4 Luc 11.31 Jonas 4.9
33 Hakuna mtu awashaye taa na kuiweka mahali palipositirika, au chini ya pishi; bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuuona mwanga.Marc 4.21-4.22 Matthieu 5.15-5.16 Luc 8.16-8.17 Jean 12.46 Philippiens 2.15-2.16
34 Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote unao mwanga; lakini likiwa bovu, mwili wako nao una giza.Matthieu 6.22-6.23 2 Corinthiens 11.3 Psaumes 81.12 Actes 26.18 Actes 13.11
35 Angalia basi, mwanga ulio ndani yako usije ukawa giza.Proverbes 16.25 2 Pierre 1.9 Jean 7.48-7.49 Jean 9.39-9.41 Apocalypse 3.17
36 Basi kama mwanga umeenea katika mwili wako wote, wala hauna sehemu iliyo na giza, mwili wako wote utakuwa na mwanga mtupu; kama vile taa ikumulikiapo kwa mwanga wake.Proverbes 6.23 Hébreux 5.14 Proverbes 4.18-4.19 Esaïe 42.16 Matthieu 13.52
37 Alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani.Luc 7.36 Luc 14.1 1 Corinthiens 9.19-9.23
38 Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula.Marc 7.2-7.5 Jean 3.25 Matthieu 15.2-15.3
39 Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovu.Tite 1.15 Genèse 6.5 Jacques 4.8 Actes 5.3 Jean 12.6
40 Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia?Luc 12.20 1 Corinthiens 15.36 Psaumes 94.8-94.9 Proverbes 8.5 Jérémie 5.21
41 Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.Luc 12.33 Tite 1.15 Luc 16.9 Actes 10.15 Proverbes 14.31
42 Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.Luc 18.12 Matthieu 23.23 Michée 6.8 1 Samuel 15.22 Malachie 3.8
43 Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni.Luc 20.46 Marc 12.38-12.39 Proverbes 16.18 3 Jean 1.9 Matthieu 23.6-23.7
44 Ole wenu, kwa kuwa mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu wapitao juu yake hawana habari nayo.Actes 23.3 Osée 9.8 Matthieu 23.27-23.28 Nombres 19.16 Psaumes 5.9
45 Mtu mmoja katika wana-sheria akajibu, akamwambia, Mwalimu, kwa kusema hayo umetushutumu sisi nasi.Jérémie 6.10 Jérémie 20.8 Jean 7.7 1 Rois 22.8 Jean 9.40
46 Akasema, Nanyi wana-sheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.Luc 11.45 Luc 11.52 Esaïe 10.1 Esaïe 58.6 Galates 6.13
47 Ole wenu, kwa kuwa mwajenga maziara ya manabii, na baba zenu ndio waliowaua.Matthieu 23.29-23.33 1 Thessaloniciens 2.15 Actes 7.51
48 Basi, mwashuhudia na kuziridhia kazi za baba zenu; kwa kuwa wao waliwaua nanyi mwawajengea maziara.Job 15.6 Ezéchiel 18.19 2 Chroniques 36.16 Matthieu 21.35-21.38 Jacques 5.10
49 Na kwa sababu hiyo hekima ya Mungu ilisema, Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na kuwafukuza,Colossiens 2.3 1 Corinthiens 1.30 Proverbes 1.2-1.6 1 Corinthiens 1.24 Actes 26.10-26.11
50 ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kupigwa msingi wa ulimwengu;Jérémie 7.29 Psaumes 9.12 Jérémie 51.56 Esaïe 26.21 Exode 20.5
51 tangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu. Naam, nawaambieni ya kwamba itatakwa kwa kizazi hiki.Matthieu 23.35 1 Jean 3.12 Hébreux 11.4 Genèse 4.8-4.11 2 Chroniques 24.20-24.22
52 Ole wenu, enyi wana-sheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.Matthieu 23.13 Malachie 2.7 Jean 7.47-7.52 Actes 4.17-4.18 Luc 11.45-11.46
53 Alipotoka humo, waandishi na Mafarisayo walianza kumsonga vibaya, na kumchokoza kwa maswali mengi,1 Corinthiens 13.5 Jérémie 20.10 Esaïe 9.12 Jérémie 18.18 Psaumes 22.12-22.13
54 wakimvizia, ili wapate neno litokalo kinywani mwake.Marc 12.13 Matthieu 22.15 Marc 3.2 Psaumes 37.32-37.33 Psaumes 56.5-56.6

Cette Bible est dans le domaine public.