1  Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake. 
Nombres 10.35  Esaïe 33.3  Psaumes 89.10  Exode 20.5  Psaumes 44.26  
 2  Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu. 
Psaumes 37.20  Michée 1.4  Osée 13.3  Psaumes 97.5  Esaïe 9.18  
 3  Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha. 
Psaumes 64.10  Psaumes 21.1  Psaumes 32.11-33.1  Psaumes 98.8-98.9  Apocalypse 18.20  
 4  Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake. 
Deutéronome 33.26  Psaumes 18.10  Exode 6.3  Psaumes 68.33  Psaumes 66.4  
 5  Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. 
Psaumes 10.14  Deutéronome 10.18  Jérémie 49.11  Luc 18.2-18.7  Jérémie 5.28  
 6  Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu. 
Psaumes 107.10  Psaumes 113.9  Psaumes 107.34  Psaumes 107.14  Psaumes 146.7  
 7  Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako, Ulipopita nyikani, 
Exode 13.21  Juges 4.14  Juges 5.4  Deutéronome 4.34  Psaumes 114.1-114.8  
 8  Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli. 
Exode 19.18  Exode 19.16  Juges 5.4-5.5  Deutéronome 5.23-5.25  Psaumes 77.18  
 9  Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu. 
Psaumes 78.24-78.27  Ezéchiel 34.26  Deutéronome 11.14  Psaumes 77.16-77.17  Deutéronome 11.10-11.12  
 10  Kabila yako ilifanya kao lake huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa. 
Psaumes 74.19  Deutéronome 26.5  Deutéronome 26.9-26.10  Psaumes 65.9  1 Pierre 5.3  
 11  Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa; 
Exode 15.20  Psaumes 68.25  Exode 14.15  Exode 17.9-17.16  1 Samuel 18.6  
 12  Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia; Na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara. 
Josué 10.16  Juges 5.19  1 Samuel 30.24  Josué 12.7-12.24  Apocalypse 6.15  
 13  Kwa nini kulala mazizini arukapo hua, Mbawa zake ziking’aa kama fedha Na manyoya yake kama dhahabu? 
Genèse 49.14  Psaumes 149.4  1 Corinthiens 6.9-6.11  Luc 15.22  Psaumes 81.6  
 14  Mwenyezi Mungu alipotawanya wafalme huko, Kulinyesha theluji katika Salmoni. 
Esaïe 1.18  Psaumes 51.7  Nombres 21.21-21.35  Juges 2.7  Juges 9.48  
 15  Ni mlima wa Mungu mlima Bashani, Ni mlima mrefu mlima Bashani. 
Psaumes 78.68-78.69  Esaïe 2.2-2.3  Michée 7.14  Psaumes 2.6  Deutéronome 3.10  
 16  Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu Mlima alioutamani Mungu akae juu yake? Naam, Bwana atakaa juu yake milele. 
Deutéronome 12.5  Psaumes 132.13-132.14  Hébreux 12.22-12.23  1 Rois 9.3  Psaumes 114.4  
 17  Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu. 
Daniel 7.10  Deutéronome 33.2  Apocalypse 9.16  Ezéchiel 1.15-1.28  Matthieu 26.53  
 18  Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana Mungu akae nao. 
Juges 5.12  Psaumes 47.5  Psaumes 78.60  Actes 1.2-1.9  Apocalypse 21.3  
 19  Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. 
Esaïe 46.4  Ephésiens 1.3  Psaumes 139.17  Psaumes 72.17-72.19  Psaumes 55.22  
 20  Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. 
Deutéronome 32.39  Apocalypse 20.1  Apocalypse 1.18  Jean 5.21  Jean 11.25-11.26  
 21  Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa. 
Habakuk 3.13  Luc 13.5  Ezéchiel 18.27-18.30  Psaumes 110.6  Psaumes 7.12  
 22  Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; 
Nombres 21.33  Esaïe 49.22  Esaïe 11.11-11.16  Osée 1.10-1.11  Jérémie 23.5-23.8  
 23  Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake. 
Psaumes 58.10  1 Rois 21.19  1 Rois 22.38  Esaïe 63.1-63.6  Apocalypse 19.17-19.21  
 24  Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu 
Psaumes 63.2  1 Chroniques 15.16-15.24  2 Samuel 6.12-6.17  Psaumes 24.7-24.10  Psaumes 47.5-47.7  
 25  Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari. 
Juges 11.34  Exode 15.20  1 Chroniques 13.8  Jérémie 31.4  Psaumes 150.3-150.5  
 26  Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli. 
Esaïe 48.1  Deutéronome 33.28  Psaumes 26.12  Psaumes 107.32  1 Chroniques 16.7-16.36  
 27  Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali. 
1 Samuel 9.21  1 Chroniques 27.12  Ezéchiel 37.19-37.27  Juges 20.35  Juges 21.6-21.25  
 28  Ee Mungu, uziamuru nguvu zako; Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu. 
Psaumes 42.8  Psaumes 44.4  Jean 5.8-5.9  Psaumes 71.3  2 Thessaloniciens 1.11  
 29  Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu Wafalme watakuletea hedaya. 
1 Rois 10.10  Psaumes 76.11  2 Chroniques 32.23  2 Chroniques 6.8-6.9  Psaumes 45.12  
 30  Mkemee mnyama wa manyasini; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita. 
2 Chroniques 20.1-20.37  2 Samuel 8.1-8.18  2 Chroniques 14.1-14.15  Job 40.21  Psaumes 22.12-22.13  
 31  Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara. 
Esaïe 45.14  Sophonie 3.10  Psaumes 44.20  Actes 8.27-8.40  Psaumes 143.6  
 32  Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo. 
Psaumes 102.22  Psaumes 100.1  Romains 15.10-15.11  Deutéronome 32.43  Psaumes 67.2-67.5  
 33  Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele; Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu. 
Psaumes 18.10  Psaumes 104.3  Psaumes 29.3-29.9  Jean 12.28-12.29  Psaumes 77.17-77.18  
 34  Mhesabieni Mungu nguvu; Enzi yake i juu ya Israeli; Na nguvu zake zi mawinguni. 
Psaumes 29.1-29.2  1 Chroniques 16.28-16.29  Psaumes 96.6-96.8  Psaumes 150.1  2 Pierre 1.17  
 35  Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu. 
Psaumes 29.11  Psaumes 65.5  Psaumes 66.5  Esaïe 45.21  Psaumes 66.20