Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 68.1
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika, Nao wamchukiao huukimbia uso wake.Esaïe 33.3 Nombres 10.35 Psaumes 89.10 Exode 20.5 Ezéchiel 5.2
2 Kama moshi upeperushwavyo, Ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto, Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.Psaumes 37.20 Michée 1.4 Osée 13.3 Psaumes 97.5 Esaïe 9.18
3 Bali wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha.Psaumes 64.10 Apocalypse 18.20 1 Thessaloniciens 5.16 Psaumes 43.4 Deutéronome 12.12
4 Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Mtengenezeeni njia ya barabara, Apitaye majangwani kama mpanda farasi; Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.Exode 6.3 Deutéronome 33.26 Psaumes 18.10 Psaumes 66.4 Psaumes 68.33
5 Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu.Psaumes 10.14 Deutéronome 10.18 Jérémie 49.11 Esaïe 1.23 2 Chroniques 6.2
6 Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.Psaumes 107.10 Psaumes 113.9 Psaumes 107.34 Psaumes 146.7 Psaumes 107.14
7 Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako, Ulipopita nyikani,Exode 13.21 Juges 5.4 Juges 4.14 Habakuk 3.12-3.13 Michée 2.13
8 Nchi ilitetemeka Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu; Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.Exode 19.18 Juges 5.4-5.5 Exode 19.16 Psaumes 77.18 Deutéronome 5.23-5.25
9 Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.Ezéchiel 34.26 Psaumes 78.24-78.27 Deutéronome 11.10-11.12 Psaumes 65.9-65.13 Deutéronome 11.14
10 Kabila yako ilifanya kao lake huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa.Psaumes 74.19 Psaumes 78.20 Psaumes 74.1-74.2 Nombres 16.3 Job 5.10-5.11
11 Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;Exode 15.20 Psaumes 68.25 Exode 14.15 Exode 17.9-17.16 Ephésiens 4.11
12 Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia; Na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara.Josué 10.16 Juges 5.19 1 Samuel 30.24 Josué 12.7-12.24 Josué 10.42
13 Kwa nini kulala mazizini arukapo hua, Mbawa zake ziking’aa kama fedha Na manyoya yake kama dhahabu?Genèse 49.14 Ephésiens 2.1-2.3 Psaumes 105.37 Tite 3.3 Ezéchiel 16.6-16.14
14 Mwenyezi Mungu alipotawanya wafalme huko, Kulinyesha theluji katika Salmoni.Esaïe 1.18 Psaumes 51.7 Josué 12.1-12.24 Nombres 21.3 Josué 10.10-10.43
15 Ni mlima wa Mungu mlima Bashani, Ni mlima mrefu mlima Bashani.Psaumes 2.6 Deutéronome 3.10 Psaumes 87.1-87.2 Psaumes 78.68-78.69 Esaïe 2.2-2.3
16 Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu Mlima alioutamani Mungu akae juu yake? Naam, Bwana atakaa juu yake milele.Deutéronome 12.5 Psaumes 132.13-132.14 Hébreux 12.22-12.23 Apocalypse 21.2-21.3 Psaumes 87.1-87.2
17 Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu.Daniel 7.10 Deutéronome 33.2 2 Rois 6.16-6.17 Habakuk 3.8 Exode 3.5
18 Wewe umepaa juu, umeteka mateka, Umepewa vipawa katikati ya wanadamu; Naam, hata na wakaidi, Bwana Mungu akae nao.Juges 5.12 Psaumes 78.60 Psaumes 47.5 Jean 14.23 Psaumes 24.3
19 Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu.Esaïe 46.4 Ephésiens 1.3 Psaumes 55.22 Psaumes 103.1-103.22 Psaumes 32.7
20 Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.Deutéronome 32.39 Apocalypse 1.18 Apocalypse 20.1 Jean 5.23 1 Samuel 2.6
21 Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa.Habakuk 3.13 Psaumes 110.6 Psaumes 7.12 Luc 13.5 Ezéchiel 18.27-18.30
22 Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari;Nombres 21.33 Osée 1.10-1.11 Jérémie 23.5-23.8 Amos 9.2-9.3 Exode 14.22
23 Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.1 Rois 21.19 Psaumes 58.10 1 Rois 22.38 2 Rois 9.33-9.37 Esaïe 63.1-63.6
24 Ee Mungu, wameiona miendo yako; Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifuPsaumes 24.7-24.10 Psaumes 47.5-47.7 1 Chroniques 13.8 Psaumes 63.2 1 Chroniques 15.16-15.24
25 Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda, Kati ya wanawali wapiga matari.Juges 11.34 Exode 15.20 1 Chroniques 13.8 Apocalypse 15.2-15.3 Jérémie 31.13
26 Mhimidini Mungu katika mikutano, Bwana katika makusanyiko ya Israeli.Esaïe 48.1 Deutéronome 33.28 Psaumes 26.12 Psaumes 111.1 Proverbes 5.16
27 Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao; Wakuu wa Yuda, kundi lao; Wakuu wa Zabuloni; Wakuu wa Naftali.1 Samuel 9.21 Juges 21.6-21.25 Psaumes 60.7 1 Chroniques 15.3 Esaïe 11.13
28 Ee Mungu, uziamuru nguvu zako; Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.Psaumes 42.8 Psaumes 44.4 Ephésiens 3.17-3.20 2 Corinthiens 12.9-12.10 Esaïe 40.31
29 Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu Wafalme watakuletea hedaya.1 Rois 10.10 Psaumes 76.11 Néhémie 2.8 Esdras 7.13-7.28 Psaumes 72.10-72.11
30 Mkemee mnyama wa manyasini; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita.Esaïe 37.1-37.38 Psaumes 18.44 Psaumes 89.10 Romains 7.22 Esaïe 34.7
31 Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.Esaïe 45.14 Sophonie 3.10 Psaumes 44.20 Esaïe 60.6-60.7 Esaïe 19.18-19.25
32 Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu, Msifuni Bwana kwa nyimbo.Deutéronome 32.43 Psaumes 67.2-67.5 Psaumes 117.1-117.2 Apocalypse 15.4 Psaumes 102.22
33 Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele; Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.Psaumes 18.10 Psaumes 104.3 1 Rois 8.27 Psaumes 68.4 Apocalypse 11.12
34 Mhesabieni Mungu nguvu; Enzi yake i juu ya Israeli; Na nguvu zake zi mawinguni.Psaumes 150.1 2 Pierre 1.17 Deutéronome 33.26 Apocalypse 19.6 Psaumes 29.1-29.2
35 Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu.Psaumes 29.11 Psaumes 65.5 Psaumes 66.5 Exode 15.1 Psaumes 72.18-72.19

Cette Bible est dans le domaine public.