Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Luc 10.3
Bible en Swahili de l’est


1 Basi, baada ya hayo Bwana aliweka na wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe.Luc 9.52 Marc 6.7-6.13 Matthieu 10.1-10.4 Luc 9.1-9.2 Luc 1.76
2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.Matthieu 9.36-9.38 1 Timothée 4.10 1 Corinthiens 3.6-3.9 1 Timothée 4.15-4.16 2 Thessaloniciens 3.1
3 Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu.Matthieu 10.16 Ezéchiel 2.3-2.6 Actes 20.29 Jean 15.20 Actes 9.16
4 Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani.2 Rois 4.29 Luc 22.35 Luc 9.3-9.6 Genèse 24.56 Luc 9.59-9.60
5 Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu;1 Samuel 25.6 Ephésiens 2.17 Actes 10.36 Esaïe 57.19 2 Corinthiens 5.18-5.20
6 na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu.2 Corinthiens 2.15-2.16 Psaumes 35.13 2 Thessaloniciens 3.16 Jacques 3.18 1 Pierre 1.14
7 Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii.Luc 9.4 1 Timothée 5.13 Galates 6.6 Philippiens 4.17-4.18 Matthieu 10.10-10.11
8 Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;1 Corinthiens 10.27 Luc 9.48 Jean 13.20 Matthieu 10.40 Luc 10.10
9 waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.Matthieu 3.2 Actes 28.7-28.10 Luc 10.11 Daniel 2.44 Luc 17.20-17.21
10 Na mji wo wote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo, nanyi mkipita katika njia zake semeni,Luc 9.5 Actes 18.6 Matthieu 10.14 Actes 13.51
11 Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia.Luc 10.9 Romains 10.21 Matthieu 10.14 Marc 6.11 Actes 13.51
12 Nawaambia ya kwamba siku ile itakuwa rahisi zaidi Sodoma kuistahimili adhabu yake kuliko mji huo.Matthieu 10.15 Matthieu 11.24 Ezéchiel 16.48-16.50 Marc 6.11 Lamentations 4.6
13 Ole wako Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu.Esaïe 23.1-23.18 Ezéchiel 26.1-28.26 Romains 11.8-11.11 Joël 3.4-3.8 Job 42.6
14 Lakini, siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko ninyi.Luc 12.47-12.48 Romains 2.1 Jean 15.22-15.25 Amos 3.2 Jean 3.19
15 Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.Matthieu 4.13 Esaïe 14.13-14.15 Matthieu 10.28 2 Pierre 2.4 Matthieu 11.23
16 Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.Matthieu 10.40 1 Thessaloniciens 4.8 Jean 13.20 Jean 12.48 Marc 9.37
17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.Marc 16.17 Luc 9.1 Luc 10.1 Romains 16.20 Luc 10.9
18 Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme.Esaïe 14.12 Apocalypse 9.1 Apocalypse 20.2 Jean 12.31 Apocalypse 12.7-12.9
19 Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.Marc 16.18 Psaumes 91.13 Actes 28.5 Romains 16.20 Luc 21.17-21.18
20 Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.Exode 32.32 Hébreux 12.23 Daniel 12.1 Philippiens 4.3 Apocalypse 3.5
21 Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza.2 Corinthiens 4.3 1 Corinthiens 2.6-2.8 Ephésiens 1.11 Matthieu 13.11-13.16 Esaïe 66.1
22 Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia.Jean 1.18 Jean 6.44-6.46 Jean 10.15 Matthieu 28.18 Matthieu 11.27
23 Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi.Matthieu 13.16-13.17
24 Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.Hébreux 11.13 1 Pierre 1.10-1.12 Jean 8.56 Hébreux 11.39
25 Na tazama, mwana-sheria mmoja alisimama amjaribu; akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?Luc 18.18 Matthieu 22.34-22.39 Luc 7.30 Matthieu 19.16-19.19 Actes 16.30-16.31
26 Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje?Esaïe 8.20 Romains 10.5 Romains 3.19 Galates 3.21-3.22 Romains 4.14-4.16
27 Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako.Matthieu 22.37-22.40 Marc 12.30-12.31 Deutéronome 6.5 Deutéronome 30.6 Romains 13.9
28 Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.Lévitique 18.5 Ezéchiel 20.11 Matthieu 19.17 Néhémie 9.29 Galates 3.12
29 Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani?Luc 16.15 Romains 4.2 Matthieu 5.43-5.44 Jacques 2.24 Lévitique 19.34
30 Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa.Luc 18.31 Luc 19.28 Ezéchiel 30.24 Jérémie 51.52 Lamentations 2.12
31 Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.Malachie 1.10 Proverbes 24.11-24.12 Psaumes 142.4 Jérémie 5.31 Osée 6.9
32 Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapita kando.Psaumes 109.25 Proverbes 27.10 Actes 18.17 2 Timothée 3.2
33 Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na alipomwona alimhurumia,Proverbes 27.10 Matthieu 10.5 Exode 2.6 1 Rois 8.50 Jérémie 39.16-39.18
34 akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.Luc 2.7 1 Thessaloniciens 5.15 Esaïe 1.5-1.6 Proverbes 24.17-24.18 Genèse 42.27
35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na cho chote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.Proverbes 19.17 Matthieu 20.2 Romains 16.23 Luc 14.13
36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?Matthieu 17.25 Matthieu 21.28-21.31 Luc 7.42 Matthieu 22.42
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.1 Jean 3.16-3.18 Michée 6.8 Luc 6.32-6.36 Matthieu 23.23 Jean 13.15-13.17
38 Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake.Jean 12.1-12.3 Luc 8.2-8.3 Actes 16.15 Jean 11.19-11.20 Jean 11.1-11.5
39 Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake.Luc 8.35 Actes 22.3 Jean 12.3 Proverbes 8.34 Deutéronome 33.3
40 Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie.Jean 6.27 Luc 12.29 Matthieu 14.15 Jonas 4.1-4.4 Luc 9.55
41 Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi;Philippiens 4.6 Matthieu 6.25-6.34 Marc 4.19 1 Corinthiens 7.32-7.35 Luc 8.14
42 lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.Psaumes 27.4 Jean 10.27-10.28 Jean 5.24 Psaumes 16.5-16.6 Luc 18.22

Cette Bible est dans le domaine public.