1  Basi ikiwako faraja yo yote katika Kristo, yakiwako matulizo yo yote ya mapenzi, ukiwako ushirika wo wote wa Roho, ikiwako huruma yo yote na rehema, 
Colossiens 3.12  1 Jean 4.12  2 Corinthiens 13.14  1 Corinthiens 12.13  Psaumes 133.1  
 2  ijalizeni furaha yangu, ili mwe na nia moja, wenye mapenzi mamoja, wenye roho moja, mkinia mamoja. 
Romains 12.16  1 Corinthiens 1.10  1 Pierre 3.8-3.9  2 Corinthiens 13.11  Jean 3.29  
 3  Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. 
Romains 12.10  Ephésiens 4.2  Ephésiens 5.21  Galates 5.26  1 Pierre 5.5  
 4  Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. 
1 Corinthiens 10.24  Romains 15.1  Jacques 2.8  Romains 12.15  Matthieu 18.6  
 5  Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; 
Matthieu 11.29  1 Jean 2.6  1 Pierre 2.21  1 Pierre 4.1  1 Corinthiens 10.33-11.1  
 6  ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; 
Hébreux 1.3  Jean 5.18  Apocalypse 21.6  2 Corinthiens 4.4  Hébreux 13.8  
 7  bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; 
2 Corinthiens 8.9  Matthieu 20.28  Jean 1.14  Galates 4.4  Romains 8.3  
 8  tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba. 
Hébreux 12.2  Jean 10.18  Matthieu 26.39  Romains 5.19  2 Corinthiens 8.9  
 9  Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; 
Matthieu 28.18  Hébreux 2.9  1 Pierre 3.22  Hébreux 1.4  Esaïe 52.13  
 10  ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; 
Esaïe 45.23-45.25  Matthieu 28.18  Hébreux 1.6  Apocalypse 5.13-5.14  Jean 5.28-5.29  
 11  na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba. 
Jean 13.13  Romains 14.9  1 Jean 4.15  Psaumes 110.1  1 Corinthiens 12.3  
 12  Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. 
2 Pierre 1.5-1.10  1 Corinthiens 15.58  Luc 13.23-13.24  Philippiens 3.13-3.14  Hébreux 4.11  
 13  Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema. 
Hébreux 13.21  2 Corinthiens 3.5  2 Timothée 1.9  Jean 3.27  Jacques 1.16-1.18  
 14  Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, 
1 Pierre 4.9  1 Corinthiens 10.10  Philippiens 2.3  Proverbes 13.10  Jacques 1.20  
 15  mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, 
Matthieu 5.14-5.16  Matthieu 5.45  1 Pierre 2.12  1 Corinthiens 1.8  Tite 2.10  
 16  mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure. 
Galates 2.2  2 Corinthiens 1.14  Psaumes 71.17  1 Thessaloniciens 2.19  1 Jean 1.1  
 17  Naam, hata nikimiminwa juu ya dhabihu na ibada ya imani yenu, nafurahi; tena nafurahi pamoja nanyi nyote. 
2 Timothée 4.6  2 Corinthiens 12.15  Romains 15.16  Colossiens 1.24  Philippiens 1.20  
 18  Nanyi vivyo hivyo furahini, tena furahini pamoja nami. 
Jacques 1.2-1.4  Philippiens 4.4  Philippiens 3.1  Ephésiens 3.13  
Missions de Timothée et d’Épaphrodite
 19  Walakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 
1 Thessaloniciens 3.2  Philippiens 1.1  1 Corinthiens 4.17  Matthieu 12.21  Romains 15.12  
 20  Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 
Philippiens 2.2  1 Corinthiens 16.10  Colossiens 4.11  Psaumes 55.13  2 Timothée 1.5  
 21  Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 
1 Corinthiens 10.24  1 Corinthiens 13.5  2 Timothée 3.2  Philippiens 2.4  2 Corinthiens 1.5  
 22  Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake. 
1 Corinthiens 4.17  1 Timothée 1.2  2 Timothée 1.2  2 Corinthiens 2.9  Philippiens 2.20  
 23  Basi, natumaini kumtuma huyo mara, hapo nitakapojua yatakayonipata. 
1 Samuel 22.3  Philippiens 2.19  
 24  Nami naamini katika Bwana ya kuwa nitakuja na mimi mwenyewe hivi karibu. 
Philémon 1.22  2 Jean 1.12  Romains 15.28-15.29  Philippiens 2.19  3 Jean 1.14  
 25  Lakini naliona imenilazimu kumtuma kwenu Epafrodito, ndugu yangu, mtenda kazi pamoja nami, askari pamoja nami; tena ni mtume wenu na mhudumu wa mahitaji yangu. 
Philippiens 4.18  Philémon 1.1-1.2  Philippiens 4.3  Philémon 1.24  2 Timothée 2.3-2.4  
 26  Kwa kuwa alikuwa na shauku kwenu ninyi nyote, akahuzunika sana, kwa sababu mlisikia ya kwamba alikuwa hawezi. 
Romains 12.15  Philippiens 1.8  2 Corinthiens 9.14  Esaïe 61.3  Job 9.27  
 27  Kwa maana alikuwa hawezi kweli kweli, karibu na kufa; lakini Mungu alimhurumia; wala si yeye peke yake, ila na mimi pia; nisiwe na huzuni juu ya huzuni. 
Philippiens 2.30  Esaïe 38.17  Jérémie 10.24  1 Corinthiens 10.13  Habakuk 3.2  
 28  Kwa hiyo nimefanya bidii nyingi zaidi kumtuma, ili mtakapomwona tena mpate kufurahi, nami nipunguziwe huzuni yangu. 
Genèse 46.29-46.30  2 Timothée 1.4  1 Jean 1.3-1.4  Actes 20.38  Genèse 45.27-45.28  
 29  Mpokeeni, basi, katika Bwana, kwa furaha yote, mkawahesabu watu kama huyu kuwa watu wa kuheshimiwa. 
1 Corinthiens 16.18  Romains 16.2  1 Timothée 5.17  1 Thessaloniciens 5.12  Luc 9.5  
 30  Maana kwa ajili ya kazi ya Kristo alikaribia kufa akaponza roho yake; ili kusudi ayatimize yaliyopungua katika huduma yenu kwangu. 
1 Corinthiens 16.17  Philippiens 4.10  Actes 20.24  Philippiens 2.27  Apocalypse 12.11