Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 21.13
Bible en Swahili de l’est


Naissance d’Isaac et départ d’Ismaël

1 Bwana akamjia Sara kama alivyonena, na Bwana akamfanyia kama alivyosema.
Genèse 18.10 Genèse 18.14 Galates 4.23 1 Samuel 2.21 Genèse 17.19
2 Sara akapata mimba akamzalia Ibrahimu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.
Hébreux 11.11 Galates 4.22 Genèse 17.21 Genèse 18.10 Genèse 18.14
3 Ibrahimu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
Genèse 17.19 Genèse 21.6 Matthieu 1.2 Romains 9.7 Josué 24.3
4 Ibrahimu akamtahiri Isaka mwanawe, alipokuwa mwenye siku nane, kama Mungu alivyomwamuru.
Actes 7.8 Genèse 17.10-17.12 Lévitique 12.3 Deutéronome 12.32 Exode 12.48
5 Naye Ibrahimu alikuwa mtu wa miaka mia, alipozaliwa mwana wake Isaka.
Genèse 17.17 Genèse 17.1 Romains 4.19
6 Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.
Esaïe 54.1 Genèse 17.17 Genèse 18.12-18.15 Psaumes 126.2 Luc 1.14
7 Akasema, N’nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.
Genèse 18.11-18.12 Nombres 23.23 Ephésiens 3.10 Psaumes 86.10 Psaumes 86.8
8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
Genèse 26.30 Genèse 29.22 Genèse 40.20 1 Rois 3.15 1 Samuel 1.22
9 Sara akamwona yule mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka.
Genèse 16.15 Galates 4.29 Genèse 16.1 Psaumes 44.13-44.14 Psaumes 22.6
10 Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.
Jean 8.35 1 Jean 2.19 Genèse 25.6 Genèse 36.6-36.7 Genèse 17.21
11 Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya mwanawe.
Genèse 17.18 Hébreux 12.11 2 Samuel 18.33 Genèse 22.1-22.2 Matthieu 10.37
12 Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.
Hébreux 11.18 Genèse 17.19 Esaïe 46.10 1 Samuel 8.7 Genèse 17.21
13 Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.
Genèse 21.18 Genèse 16.10 Genèse 17.20 Genèse 25.12-25.18
14 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Genèse 16.7 Genèse 22.3 Genèse 26.33 Ecclésiaste 9.10 Esaïe 16.8
15 Yale maji yakaisha katika kiriba, akamlaza kijana chini ya kijiti kimoja.
2 Rois 3.9 Psaumes 63.1 Exode 15.22-15.25 Genèse 21.14 Jérémie 14.3
16 Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia.
Genèse 44.34 1 Samuel 30.4 Genèse 27.38 Zacharie 12.10 1 Rois 3.26
17 Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko.
Genèse 16.11 Exode 3.7 Matthieu 15.32 Exode 22.27 Genèse 16.9
18 Ondoka, ukamwinue kijana, ukamshike mkononi mwako, kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.
Genèse 21.13 Genèse 16.10 Genèse 17.20 Genèse 25.12-25.18 1 Chroniques 1.29-1.31
19 Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
Nombres 22.31 Luc 24.16-24.31 Esaïe 35.5-35.6 2 Rois 6.17-6.20
20 Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
Genèse 39.21 Genèse 28.15 Genèse 39.2-39.3 Genèse 16.12 Genèse 25.27
21 Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Nombres 10.12 1 Samuel 25.1 Nombres 13.26 Nombres 13.3 Genèse 26.34-26.35

Abraham à Beer-Shéba

22 Ikawa wakati ule Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakamwambia Ibrahimu, wakinena, Mungu yu pamoja nawe katika yote unayotenda.
Genèse 26.28 Genèse 26.26 Genèse 20.2 Esaïe 8.10 Genèse 39.2-39.3
23 Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
Josué 2.12 Genèse 20.14 1 Samuel 20.42 1 Samuel 20.13 Deutéronome 6.13
24 Ibrahimu akasema, Nitaapa.
Hébreux 6.16 Romains 12.18 Genèse 14.13
25 Kisha Ibrahimu akamlaumu Abimeleki kwa sababu ya kisima cha maji ambacho watumwa wa Abimeleki wamekinyang’anya.
Genèse 26.15-26.22 Proverbes 17.10 Genèse 29.8 Genèse 13.7 Juges 1.15
26 Abimeleki akasema, Mimi sijui ni nani aliyetenda neno hili, wala hukuniambia, wala sikusikia habari hii ila leo tu.
2 Rois 5.20-5.24 Genèse 13.7
27 Ibrahimu akatwaa kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.
Genèse 31.44 Proverbes 21.14 Proverbes 18.24 Genèse 26.28-26.31 1 Samuel 18.3
28 Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao.
29 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?
Exode 12.26 1 Samuel 15.14 Genèse 33.8
30 Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
Genèse 31.52 Josué 22.27-22.28 Genèse 31.44-31.48 Josué 24.27
31 Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili.
Genèse 26.33 Genèse 21.14 2 Samuel 17.11 Juges 20.1 Genèse 26.23
32 Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.
Genèse 26.8 Exode 13.17 Juges 13.1 Genèse 14.13 Genèse 26.14
33 Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la Bwana Mungu wa milele.
Psaumes 90.2 Esaïe 40.28 Genèse 4.26 Genèse 12.8 Deutéronome 33.27
34 Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.
Genèse 20.1 Hébreux 11.13 Psaumes 39.12 1 Chroniques 29.15 Hébreux 11.9

Cette Bible est dans le domaine public.