Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Jean 5.3
Bible en Swahili de l’est


Oppositions à Jésus

Guérison à la piscine de Béthesda

1 Baada ya hayo palikuwa na sikukuu ya Wayahudi; naye Yesu akakwea kwenda Yerusalemu.
Lévitique 23.2-23.4 Exode 23.14-23.17 Exode 34.23 Deutéronome 16.16 Jean 2.13
2 Na huko Yerusalemu penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiebrania Bethzatha, nayo ina matao matano.
Néhémie 3.1 Néhémie 12.39 Néhémie 3.32 Actes 21.40 Jean 19.17
3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, nao waliopooza, [wakingoja maji yachemke.
Matthieu 15.30 Marc 3.1-3.4 Romains 8.25 Lamentations 3.26 Jacques 5.7
4 Kwa maana kuna wakati ambapo malaika hushuka, akaingia katika ile birika, akayatibua maji. Basi yeye aliyeingia wa kwanza baada ya maji kutibuliwa, akapona ugonjwa wote uliokuwa umempata.]
5 Na hapa palikuwa na mtu, ambaye amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.
Marc 9.21 Luc 13.16 Luc 8.43 Jean 9.21 Jean 5.14
6 Yesu alipomwona huyu amelala, naye akijua ya kuwa amekuwa hali hiyo siku nyingi, alimwambia, Wataka kuwa mzima?
Hébreux 4.15 Hébreux 4.13 Esaïe 65.1 Jean 21.17 Jérémie 13.27
7 Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, mimi sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; ila wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.
Psaumes 142.4 Deutéronome 32.36 1 Corinthiens 9.24 Psaumes 72.12 2 Corinthiens 1.8-1.10
8 Yesu akamwambia, Simama, jitwike godoro lako, uende.
Luc 5.24 Matthieu 9.6 Marc 2.11 Actes 9.34
9 Mara yule mtu akawa mzima, akajitwika godoro lake, akaenda. Nayo ilikuwa ni sabato siku hiyo.
Jean 9.14 Marc 3.2-3.4 Matthieu 12.10-12.13 Jean 7.23 Jean 5.14
10 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwambia yule aliyeponywa, Leo ni sabato, wala si halali kwako kujitwika godoro.
Jérémie 17.21 Luc 6.2 Luc 13.14 Néhémie 13.15-13.21 Jean 9.16
11 Akawajibu, Yeye aliyenifanya kuwa mzima ndiye aliyeniambia, Jitwike godoro lako, uende.
Jean 9.16 Marc 2.9-2.11
12 Basi wakamwuliza, Yule aliyekuambia, Jitwike, uende, ni nani?
1 Samuel 14.38 Romains 10.2 Juges 6.29 Matthieu 21.23
13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakumjua ni nani; maana Yesu alikuwa amejitenga, kwa sababu palikuwa na watu wengi mahali pale.
Luc 24.31 Jean 8.59 Luc 4.30 Jean 14.9
14 Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi.
Jean 8.11 Lévitique 26.23-26.24 1 Pierre 4.3 Apocalypse 2.21-2.23 Psaumes 118.18
15 Yule mtu akaenda zake, akawapasha habari Wayahudi ya kwamba ni Yesu aliyemfanya kuwa mzima.
Jean 5.12 Jean 9.30 Marc 1.45 Jean 1.19 Jean 9.34
16 Kwa sababu hiyo Wayahudi wakamwudhi Yesu, kwa kuwa alitenda hayo siku ya sabato.
Actes 9.4-9.5 Jean 15.20 Jean 5.13 Luc 6.11 Jean 7.19-7.20
17 Akawajibu, Baba yangu anatenda kazi hata sasa, nami ninatenda kazi.
Jean 14.10 Jean 9.4 1 Corinthiens 12.6 Actes 14.17 Hébreux 1.3
18 Basi kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na hayo alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu. Basi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambia,
Jean 10.33 Jean 8.58 Jean 10.30 Jean 19.7 Jean 5.23
19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Jean 8.28 Jean 12.49 Jean 14.10 Jean 5.28-5.30 Romains 8.11
20 Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, naye humwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; hata na kazi kubwa zaidi kuliko hizo atamwonyesha, ili ninyi mpate kustaajabu.
Jean 3.35 Matthieu 3.17 Jean 17.26 2 Pierre 1.17 Jean 14.12
21 Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao.
Jean 11.25 Romains 8.11 Jean 11.43-11.44 Luc 8.54-8.55 Deutéronome 32.39
22 Tena Baba hamhukumu mtu ye yote, bali amempa Mwana hukumu yote;
Actes 17.31 Jean 5.27 Actes 10.42 Jean 9.39 Matthieu 28.18
23 ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.
1 Jean 2.23 Luc 10.16 Jean 15.23-15.24 1 Corinthiens 6.19 2 Thessaloniciens 2.16-2.17
24 Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yuna uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Jean 3.18 Jean 3.36 1 Jean 5.11-5.13 1 Jean 3.14 Jean 20.31
25 Amin, amin, nawaambia, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hai.
Jean 4.23 Ephésiens 2.5 Luc 15.24 Apocalypse 3.1 Jean 5.28
26 Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake.
Jean 1.4 Jérémie 10.10 1 Timothée 1.17 Exode 3.14 Jean 17.2-17.3
27 Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu.
Jean 5.22 Actes 17.31 Actes 10.42 Psaumes 110.1-110.2 1 Corinthiens 15.25
28 Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.
Apocalypse 20.12 1 Thessaloniciens 4.14-4.17 Jean 4.21 Osée 13.14 Esaïe 26.19
29 Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Romains 2.6-2.10 Daniel 12.2-12.3 Actes 24.15 Hébreux 13.16 Matthieu 25.31-25.46
30 Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
Jean 6.38 Jean 4.34 Jean 5.19 Matthieu 26.39 Jean 8.28
31 Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
Jean 8.13-8.14 Jean 8.54 Proverbes 27.2 Apocalypse 3.14
32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.
Jean 8.17-8.18 Jean 12.28-12.30 Jean 12.50 1 Jean 5.6-5.9 Jean 1.33
33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
Jean 1.29-1.34 Jean 3.26-3.36 Jean 1.15-1.27 Jean 1.6-1.8
34 Lakini mimi siupokei ushuhuda kwa wanadamu; walakini ninasema haya ili ninyi mpate kuokoka.
Jean 20.31 Luc 19.41-19.42 1 Jean 5.9 Romains 10.1 Romains 12.21
35 Yeye alikuwa taa iwakayo na kung’aa, nanyi mlipenda kuishangilia nuru yake kwa muda.
2 Pierre 1.19 Matthieu 21.26 Matthieu 11.11 Luc 1.15-1.17 Ezéchiel 33.31
36 Lakini ushuhuda nilio nao mimi ni mkubwa kuliko ule wa Yohana; kwa kuwa zile kazi alizonipa Baba ili nizimalize, kazi hizo zenyewe ninazozitenda, zanishuhudia ya kwamba Baba amenituma.
Jean 10.25 Jean 15.24 1 Jean 5.9 Matthieu 11.4 Jean 3.2
37 Naye Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.
Jean 8.18 Jean 1.18 Matthieu 3.17 Jean 14.9 Deutéronome 4.12
38 Wala neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hammwamini yule aliyetumwa na yeye.
1 Jean 2.14 Deutéronome 6.6-6.9 Jean 8.37 Jacques 1.21-1.22 Psaumes 119.11
39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia.
Luc 24.27 2 Pierre 1.19-1.21 Esaïe 34.16 1 Pierre 1.10-1.11 2 Timothée 3.14-3.17
40 Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima.
Jean 3.19 Jean 6.37 Matthieu 23.37 Esaïe 50.2 Jean 6.27
41 Mimi siupokei utukufu kwa wanadamu.
1 Thessaloniciens 2.6 Jean 7.18 Jean 5.34 Jean 5.44 Jean 8.50
42 Walakini nimewajua ninyi ya kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu.
1 Jean 3.17 Jean 2.25 Jean 8.42 1 Jean 4.20 Jean 15.23-15.24
43 Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, wala ninyi hamnipokei; mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea huyo.
Jean 10.25 Jean 17.4-17.6 Matthieu 24.5 Jean 8.28-8.29 Jean 6.38
44 Mwawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
Romains 2.29 1 Pierre 1.7 Jean 12.43 Romains 8.7-8.8 2 Chroniques 6.8
45 Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
Romains 3.19-3.20 Jean 9.28-9.29 Romains 2.17-2.29 Romains 2.12 Jean 8.9
46 Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu.
Deutéronome 18.15 Deutéronome 18.18-18.19 Actes 26.22 Jean 1.45 Luc 24.27
47 Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?
Luc 16.31 Luc 16.29

Cette Bible est dans le domaine public.