Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 69.13
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Mungu, uniokoe, Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.Psaumes 69.14-69.15 Psaumes 42.7 Psaumes 45.1 Esaïe 43.2 Psaumes 18.4
2 Ninazama katika matope mengi, Pasipowezekana kusimama. Nimefika penye maji ya vilindi, Mkondo wa maji unanigharikisha.Psaumes 40.2 Psaumes 32.6 Psaumes 88.6-88.7 Genèse 7.17-7.23 Jérémie 38.6
3 Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofu Kwa kumngoja Mungu wangu.Psaumes 119.82 Psaumes 6.6 Esaïe 38.14 Psaumes 119.123 Deutéronome 28.32
4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nalilipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.Psaumes 35.19 Jean 15.25 Psaumes 40.12 Esaïe 53.4-53.7 1 Pierre 3.18
5 Ee Mungu, unajua upumbavu wangu, Wala hukufichwa dhambi yangu.Psaumes 19.12 Jérémie 16.17 Psaumes 17.3 Psaumes 38.5 Psaumes 44.20-44.21
6 Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.2 Samuel 23.3 Psaumes 72.18 Psaumes 7.7 Psaumes 25.3 Actes 13.23
7 Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu, Fedheha imenifunika uso wangu.Jérémie 15.15 Psaumes 44.22 Esaïe 50.6 Jean 15.21-15.24 Matthieu 26.67-26.68
8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, Na msikwao kwa wana wa mama yangu.Psaumes 31.11 Psaumes 38.11 Jean 1.11 1 Samuel 17.28 Matthieu 10.35-10.36
9 Maana wivu wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.Romains 15.3 Psaumes 119.139 Jean 2.14-2.17 Psaumes 89.50-89.51 Marc 11.15-11.17
10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga, Ikawa laumu juu yangu.Psaumes 35.13 Psaumes 109.24-109.25 Luc 7.33-7.34 Psaumes 102.8-102.9
11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu, Nikawa mithali kwao.Jérémie 24.9 1 Rois 9.7 Job 17.6 Joël 1.13 Deutéronome 28.37
12 Waketio langoni hunisema, Na nyimbo za walevi hunidhihaki.Job 30.8-30.9 Matthieu 27.20 Actes 4.26-4.27 Genèse 19.1 Matthieu 27.12-27.13
13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.Esaïe 49.8 2 Corinthiens 6.2 Romains 15.8-15.9 Luc 22.44 1 Samuel 25.8
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe nao wanaonichukia, Na katika vilindi vya maji.Psaumes 144.7 Psaumes 69.1-69.2 Psaumes 109.21 Psaumes 42.7 Luc 19.14
15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.Psaumes 88.4-88.6 Jonas 2.2-2.7 Nombres 16.33-16.34 Esaïe 43.1-43.2 Apocalypse 12.15-12.16
16 Ee Bwana, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.Psaumes 63.3 Psaumes 109.21 Psaumes 25.16 Psaumes 51.1 Esaïe 63.7
17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.Psaumes 27.9 Psaumes 102.2 Psaumes 44.24 Psaumes 40.13 Job 7.21
18 Uikaribie nafsi yangu, uikomboe, Kwa sababu ya adui zangu unifidie.Jérémie 14.8 Psaumes 31.5 Psaumes 22.19 Josué 7.9 Psaumes 10.1
19 Wewe umejua kulaumiwa kwangu, Na kuaibika na kufedheheka kwangu, Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote.Hébreux 12.2 Psaumes 2.2-2.4 Jean 8.49 Psaumes 69.7-69.9 Psaumes 22.6-22.7
20 Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.Job 16.2 Esaïe 63.5 Psaumes 142.4 Marc 14.50 Psaumes 42.10
21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.Marc 15.23 Matthieu 27.34 Luc 23.36 Matthieu 27.48 Marc 15.36
22 Meza yao mbele yao na iwe mtego; Naam, wakiwa salama na iwe tanzi.Romains 11.8-11.10 Malachie 2.2 Proverbes 1.32 Esaïe 8.14-8.15 1 Pierre 2.8
23 Macho yao yatiwe giza wasione, Na viuno vyao uvitetemeshe daima.Daniel 5.6 Jérémie 30.6 Romains 11.10 Esaïe 6.9-6.10 Romains 11.25
24 Uimwage ghadhabu yako juu yao, Na ukali wa hasira yako uwapate.Psaumes 79.6 Osée 5.10 1 Thessaloniciens 2.15-2.16 Deutéronome 31.17 Esaïe 13.8
25 Matuo yao na yawe ukiwa, Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.Matthieu 23.38 Actes 1.20 Esaïe 6.11 Matthieu 24.1-24.2 1 Rois 9.8
26 Maana wanamwudhi mtu uliyempiga Wewe, Wanasimulia maumivu ya hao uliowatia jeraha.Esaïe 53.4 Zacharie 1.15 Esaïe 53.10 2 Chroniques 28.9 Zacharie 13.7
27 Uwaongezee uovu juu ya uovu, Wala wasiingie katika haki yako.Esaïe 26.10 Néhémie 4.5 Romains 1.28 2 Timothée 4.14 Esaïe 5.6
28 Na wafutwe katika chuo cha uhai, Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.Luc 10.20 Philippiens 4.3 Ezéchiel 13.9 Apocalypse 3.5 Hébreux 12.23
29 Nami niliye maskini na mtu wa huzuni, Mungu, wokovu wako utaniinua.Psaumes 89.26-89.27 Psaumes 40.17 Matthieu 8.20 Psaumes 22.27-22.31 Ephésiens 1.21-1.22
30 Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo, Nami nitamtukuza kwa shukrani.Psaumes 28.7 Psaumes 34.3 Psaumes 118.21 Psaumes 40.1-40.3 Psaumes 118.28-118.29
31 Nayo yatampendeza Bwana kuliko ng’ombe, Au ndama mwenye pembe na kwato.Psaumes 50.13-50.14 Hébreux 13.15 Psaumes 50.23 1 Pierre 2.5 Osée 14.2
32 Walioonewa watakapoona watafurahi; Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.Psaumes 22.26 Psaumes 34.2 Psaumes 25.9 Esaïe 55.6-55.7 Jean 20.20
33 Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake.Psaumes 68.6 Psaumes 102.20 Ephésiens 3.1 Luc 4.18 Apocalypse 2.10
34 Mbingu na nchi zimsifu, Bahari na vyote viendavyo ndani yake.Psaumes 96.11 Esaïe 49.13 Esaïe 55.12 Psaumes 150.6 Psaumes 98.7-98.8
35 Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.Psaumes 51.18 Esaïe 44.26 Esaïe 46.13 Apocalypse 14.1 Psaumes 147.12-147.13
36 Wazao wa watumishi wake watairithi, Nao walipendao jina lake watakaa humo.Psaumes 102.28 Psaumes 37.29 Romains 8.28 Psaumes 91.14 Jean 14.23

Cette Bible est dans le domaine public.