Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 24.65
Bible en Swahili de l’est


Mariage d’Isaac et Rebecca

1 Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na Bwana alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote.
Genèse 13.2 Genèse 25.20 Genèse 21.5 Genèse 18.11 Galates 3.9
2 Ibrahimu akamwambia mtumishi wake, mzee wa nyumba yake, aliyetawala vitu vyake vyote, Tafadhali uutie mkono wako chini ya paja langu,
Genèse 47.29 Genèse 39.4-39.6 Genèse 15.2 Genèse 24.9-24.10 1 Chroniques 29.24
3 nami nitakuapisha kwa Bwana, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;
Genèse 26.34-26.35 Genèse 28.8 Deutéronome 10.20 2 Rois 19.15 1 Samuel 20.17
4 bali enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke.
Genèse 28.2 Genèse 12.7 Genèse 22.20-22.23 Genèse 11.25-12.1
5 Yule mtumishi akamwambia, Labda yule mwanamke hatakubali kufuatana nami mpaka nchi hii, je! Nimrudishe mwanao mpaka nchi ulikotoka?
Jérémie 4.2 Genèse 24.58 Exode 20.7 Proverbes 13.16 Exode 9.2
6 Ibrahimu akamwambia, Ujihadhari, usimrudishe mwanangu huko.
Hébreux 10.39 2 Pierre 2.20-2.22 Hébreux 11.9 Hébreux 11.13-11.16 Galates 5.1
7 Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, na kusema nami katika nchi niliyozaliwa, aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii; yeye atampeleka malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke tokea huko;
Genèse 13.15 Psaumes 34.7 Hébreux 1.14 Exode 33.2 Exode 32.13
8 na yule mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi, utafunguliwa kiapo changu hiki; lakini usimrudishe mwanangu huko.
Josué 2.17-2.20 Nombres 30.5 Nombres 30.8 Genèse 24.4-24.6 Jean 8.32
9 Yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la Ibrahimu bwana wake, akamwapia katika neno hilo.
Genèse 24.2
10 Kisha huyo mtumishi akatwaa ngamia kumi katika ngamia za bwana wake akaenda zake, maana mali zote za bwana wake zilikuwa mkononi mwake, akaondoka, akaja mpaka Mesopotamia, mpaka mji wa Nahori.
Genèse 11.31 Deutéronome 23.4 Genèse 29.4-29.5 Genèse 39.4-39.6 1 Chroniques 19.6
11 Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji wakati wa jioni, wakati ambapo wanawake wanakwenda kuteka maji.
1 Samuel 9.11 Jean 4.7 Exode 2.16 Genèse 24.13-24.20 Proverbes 12.10
12 Naye akasema, Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, nakuomba mambo yangu uyajalie yawe heri leo, ukamfadhili bwana wangu Ibrahimu.
Genèse 24.27 Genèse 26.24 Exode 3.15 Exode 3.6 Genèse 24.48
13 Tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji, na binti za watu wa mjini wanatoka kuteka maji,
Genèse 24.43 Jean 4.7 1 Samuel 9.11 Proverbes 3.6 Genèse 29.9-29.10
14 basi na iwe hivi; yule msichana nitakayemwambia, Tua mtungi wako, nakuomba, ninywe; naye akasema, Unywe, nami nitawanywesha na ngamia zako pia; basi huyu na awe ndiye uliyemchagulia mtumishi wako Isaka; na kwa hayo nitajua ya kuwa umemfadhili bwana wangu.
Juges 6.37 Juges 6.17 Genèse 15.8 2 Samuel 20.9 1 Samuel 10.2-10.10
15 Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake.
Genèse 11.29 Genèse 22.20-22.23 Genèse 11.27 Genèse 24.24 Genèse 24.45
16 Naye yule msichana alikuwa mzuri sana uso wake, bikira, wala mwanamume hajamjua bado; akashuka kisimani, akajaza mtungi wake, akapanda.
Genèse 26.7 Genèse 39.6 Genèse 4.1 Cantique 5.2 Nombres 31.17-31.18
17 Ndipo yule mtumishi akapiga mbio kwenda kumlaki, akasema, Tafadhali unipe maji kidogo katika mtungi wako ninywe.
Jean 4.7 Esaïe 21.14 1 Rois 17.10 Esaïe 41.17-41.18 Jean 4.9
18 Naye akasema, Unywe, bwana wangu, akafanya haraka, akatua mtungi wake mkononi mwake, akamnywesha.
1 Pierre 3.8 Proverbes 31.26 Genèse 24.14 1 Pierre 4.8-4.9
19 Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa.
Genèse 24.14 Genèse 24.45-24.46 1 Pierre 4.9
20 Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote.
21 Basi yule mtu akamkazia macho, akanyamaza, ili ajue kwamba Bwana ameifanikisha safari yake ama sivyo.
Genèse 24.12 Genèse 24.56 Psaumes 34.1-34.6 Psaumes 107.43 Psaumes 107.15
22 Ikawa, ngamia walipokwisha kunywa, yule mtu akatwaa pete ya dhahabu, uzani wake ulikuwa nusu shekeli, na vikuku viwili kwa mikono yake, uzani wake ulikuwa shekeli kumi za dhahabu,
Exode 32.2-32.3 Esaïe 3.19-3.23 Ezéchiel 16.11-16.12 Genèse 23.15-23.16 Jérémie 2.32
23 akasema, U binti wa nani wewe? Tafadhali uniambie. Je! Iko nafasi katika nyumba ya baba yako tupate mahali pa kukaa kwa muda?
24 Akasema, Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, aliyemzalia Nahori.
Genèse 24.15 Genèse 22.23 Genèse 11.29 Genèse 22.20
25 Tena akamwambia, Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha, na mahali pa kukaa wageni.
1 Pierre 4.9 Genèse 18.4-18.8 Esaïe 32.8 Juges 19.19-19.21
26 Yule mtu akainama akamsujudu Bwana.
Exode 4.31 Genèse 24.52 Genèse 24.48 Philippiens 2.10 1 Chroniques 29.20
27 Akasema, Na atukuzwe Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ambaye hakuacha rehema zake na kweli yake kwa bwana wangu. Bwana akaniongoza mimi nami njiani hata nyumba ya nduguze bwana wangu.
Genèse 24.48 Psaumes 98.3 Genèse 32.10 Genèse 24.12 Ruth 4.14
28 Basi yule msichana akapiga mbio, akawaambia watu wa nyumba ya mama yake mambo hayo.
Genèse 24.55 Genèse 24.48 Genèse 24.67 Genèse 31.33
29 Na Rebeka alikuwa na kaka, jina lake Labani. Labani akatoka mbio kumwendea yule mtu kisimani.
Genèse 29.5 Genèse 29.13 Genèse 24.60 Genèse 24.55
30 Ikawa, alipoiona ile pete, na vikuku mikononi mwa nduguye, akasikia maneno ya Rebeka nduguye, akisema, Hivyo ndivyo alivyoniambia mtu huyo, basi akamjia mtu yule, na tazama, amesimama karibu na ngamia kisimani.
31 Akasema, Karibu, wewe uliyebarikiwa na Bwana, mbona unasimama nje? Kwa maana nimeiweka nyumba tayari, na nafasi kwa ngamia.
Genèse 26.29 Ruth 3.10 Psaumes 115.15 Juges 17.2 Proverbes 18.16
32 Na mtu yule akaingia katika nyumba, akawafungua ngamia; naye akatoa majani na malisho kwa ngamia, na maji ya kuoshea miguu yake, na miguu ya watu waliokuwa pamoja naye.
Juges 19.21 Genèse 43.24 Genèse 18.4 Jean 13.4-13.14 Luc 7.44
33 Akaandaliwa chakula, lakini akasema, Sili mpaka niseme kwanza maneno yangu. Akamwambia, Haya, sema.
Proverbes 22.29 Jean 4.14 Psaumes 132.3-132.5 1 Timothée 6.2 Ecclésiaste 9.10
34 Akasema, Mimi ni mtumwa wa Ibrahimu,
35 na Bwana amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng’ombe, na fedha, na dhahabu, na watumwa, na wajakazi, na ngamia, na punda.
Genèse 13.2 Genèse 24.1 Job 42.10-42.12 Proverbes 22.4 Genèse 12.2
36 Naye Sara, mkewe bwana wangu, akamzalia bwana wangu mwana wa kiume, katika uzee wake; naye amempa yote aliyo nayo.
Genèse 25.5 Genèse 21.10 Genèse 21.1-21.7 Genèse 17.15-17.19 Genèse 18.10-18.14
37 Kisha bwana wangu akaniapisha akisema, Usimtwalie mwanangu mke wa binti za Wakanaani, ambao nakaa katika nchi yao.
Genèse 24.2-24.9 Esdras 9.1-9.3 Genèse 6.2 Genèse 27.46
38 Ila uende mpaka nyumbani kwa babangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu mke.
Genèse 24.4 Genèse 31.19 Genèse 12.1
39 Nikamwambia bwana wangu, Labda huyo mwanamke hatafuatana nami.
Genèse 24.5
40 Akaniambia, Bwana, ambaye naenenda machoni pake, atapeleka malaika wake pamoja nawe, atafanikisha njia yako; nawe umtwalie mwanangu mke katika jamaa zangu, na wa nyumba ya babangu.
Genèse 17.1 Genèse 24.7 Genèse 5.24 Genèse 5.22 Psaumes 16.8
41 Ndipo utafunguliwa kiapo changu hapo utakapowafikilia jamaa zangu; nao wasipokupa msichana huyo, utafunguliwa kiapo changu.
Genèse 24.8 Deutéronome 29.12
42 Nami nikaja leo kisimani, nikasema, Ee Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, ukinifanikishia sasa njia yangu niendayo mimi,
Néhémie 1.11 Genèse 24.12-24.14 Actes 10.22 Psaumes 90.17 Actes 10.7-10.8
43 tazama! Nimesimama karibu na kisima cha maji; basi na iwe hivi, msichana ajaye kuteka maji, nikamwambia, Nipe, nakuomba, maji kidogo katika mtungi wako ninywe,
Genèse 24.13-24.14
44 naye akaniambia, Unywe wewe, na ngamia zako pia nitawatekea, huyo na awe ndiye mke Bwana aliyemwekea mwana wa bwana wangu.
Genèse 24.14 Proverbes 19.14 Genèse 2.22 1 Timothée 2.10 Esaïe 32.8
45 Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama! Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe.
Actes 12.12-12.17 Actes 4.24-4.33 Néhémie 2.4 1 Samuel 1.13-1.15 Esaïe 65.24
46 Akafanya haraka akatua mtungi wake chini, akanena, Unywe, na ngamia zako nitawanywesha pia; basi nikanywa, akawanywesha na ngamia nao.
Genèse 24.18-24.19
47 Kisha nikamwuliza nikasema, U binti wa nani wewe? Naye akasema, Mimi ni binti Bethueli, mwana wa Nahori, Milka aliyemzalia. Nami nikamtia hazama puani mwake na vikuku mikononi mwake.
Genèse 24.22-24.24 Psaumes 45.9 Genèse 24.53 Ezéchiel 16.10-16.13 Ephésiens 5.26-5.27
48 Nikainama, nikamsujudia Bwana, nikamtukuza Bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, aliyeniongoza njiani, nimtwalie mwana wa bwana wangu binti wa ndugu yake.
Genèse 24.26-24.27 Genèse 24.52 Esaïe 48.17 Psaumes 32.8 Psaumes 48.14
49 Basi, kama mnataka kumfanyia rehema na kweli bwana wangu, niambieni kama sivyo, niambieni; ili nigeuke upande wa kuume au wa kushoto.
Genèse 47.29 Josué 2.14 Nombres 20.17 Deutéronome 2.27 Genèse 32.10
50 Ndipo Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa Bwana, wala sisi hatuwezi kukuambia neno jema wala baya.
Genèse 31.24 Psaumes 118.23 Genèse 31.29 2 Samuel 13.22 Marc 12.11
51 Tazama, huyo Rebeka yuko mbele yako, umchukue, ukaende zako awe mke wa mwana wa bwana wako, kama alivyosema Bwana.
Genèse 24.15 Genèse 20.15 2 Samuel 16.10
52 Ikawa mtumishi wa Ibrahimu aliposikia maneno yao, akainama hata nchi mbele za Bwana.
Genèse 24.48 Genèse 24.26 2 Chroniques 20.18 Psaumes 95.6 Psaumes 116.1-116.2
53 Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.
Exode 3.22 Exode 12.35 Exode 11.2 Deutéronome 33.13-33.16 Cantique 4.13
54 Wakala wakanywa, yeye na watu waliokuwa pamoja naye, nao wakakaa usiku. Wakaondoka asubuhi, naye akasema, Nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu.
Genèse 24.59 Genèse 24.56 2 Samuel 18.19 Genèse 28.5-28.6 2 Samuel 18.27-18.28
55 Ndugu yake na mama yake wakasema, Msichana na akae kwetu kama siku kumi, zisipungue, baadaye aende.
Juges 14.8 Lévitique 25.29 Genèse 4.3
56 Naye akawaambia, Msinikawilishe, mradi Bwana amefanikisha njia yangu; nipeni ruhusa niende kwa bwana wangu.
Proverbes 25.25 Esaïe 48.15 Genèse 45.9-45.13 Josué 1.8
57 Wakasema, Na tumwite huyo msichana, tumwulize mwenyewe.
58 Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda.
Luc 1.38 Psaumes 45.10-45.11
59 Ndipo wakampeleka Rebeka ndugu yao, na yaya wake, na mtumishi wa Ibrahimu, na watu wake.
Genèse 35.8 Genèse 24.53 Nombres 11.12 1 Thessaloniciens 2.5 Genèse 24.60
60 Wakambarikia Rebeka, wakamwambia, Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.
Genèse 22.17 Genèse 17.16 Genèse 48.15-48.16 Genèse 28.3 Genèse 1.28
61 Rebeka akaondoka na vijakazi wake, nao wakapanda juu ya ngamia, wakamfuata yule mtu. Naye huyo mtumishi akamchukua Rebeka akaenda zake.
Psaumes 45.10 Esther 8.14 Esther 8.10 Genèse 2.24 Genèse 31.34
62 Basi Isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana alikaa katika nchi ya kusini.
Genèse 25.11 Genèse 16.14 Genèse 12.9 Genèse 20.1
63 Isaka akatoka ili kutafakari kondeni wakati wa jioni; akainua macho yake, akaona, kuna ngamia wanakuja.
Psaumes 119.15 Psaumes 1.2 Josué 1.8 Psaumes 119.27 Psaumes 104.34
64 Rebeka akainua macho, naye alipomwona Isaka, alishuka juu ya ngamia.
Josué 15.18 Juges 1.14
65 Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye kondeni kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika.
1 Timothée 2.9 1 Corinthiens 11.5-11.6 Genèse 20.16 1 Corinthiens 11.10
66 Yule mtumishi akamwambia Isaka mambo yote aliyoyatenda.
Marc 6.30
67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.
Genèse 37.35 Genèse 38.12 Esaïe 54.1-54.5 2 Corinthiens 11.1-11.2 Genèse 18.9-18.10

Cette Bible est dans le domaine public.