Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Genèse 18
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Genèse 14.13 Genèse 13.18 Genèse 48.3 Genèse 26.2 Actes 7.2
2 Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, Hébreux 13.2 Genèse 18.22 Genèse 19.1 Juges 13.3 Genèse 18.16
3 akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Genèse 32.5
4 Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Genèse 19.2 Genèse 43.24 Genèse 24.32 Luc 7.44 1 Timothée 5.10
5 Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Juges 13.15 Genèse 19.8 Psaumes 104.15 Genèse 33.10 Juges 19.5
6 Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. Romains 12.13 1 Pierre 4.9 Actes 16.15 Esaïe 32.8 Hébreux 13.2
7 Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng’ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. Malachie 1.14 Genèse 19.3 Amos 6.4 Luc 15.27 Luc 15.30
8 Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala. Genèse 19.3 Jean 12.2 Deutéronome 32.14 Luc 24.30 Juges 13.15
9 Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani. Genèse 24.67 Genèse 31.33 Genèse 4.9 Tite 2.5
10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake. Genèse 21.2 Genèse 17.21 Genèse 17.19 Romains 9.8-9.9 Galates 4.23
11 Basi Ibrahimu na Sara walikuwa wazee, na umri wao mkubwa, na Sara alikuwa amekoma katika desturi ya wanawake. Genèse 17.17 Hébreux 11.11-11.12 Hébreux 11.19 Genèse 17.24 Lévitique 15.19
12 Kwa hiyo Sara akacheka moyoni mwake, akisema, Niwapo mkongwe, nitapata furaha, na bwana wangu mzee? Genèse 17.17 1 Pierre 3.6 Ephésiens 5.33 Genèse 21.6-21.7 Luc 1.34-1.35
13 Bwana akamwambia Ibrahimu, Mbona Sara amecheka akisema, Mimi kweli nitazaa mwana, nami ni mzee? Jean 2.25
14 Kuna neno gani lililo gumu la kumshinda Bwana? Kwa muhula wake nitakurudia, wakati huu huu mwakani, na Sara atapata mwana wa kiume. Jérémie 32.17 Matthieu 19.26 Luc 1.37 Jérémie 32.27 Marc 10.27
15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo, umecheka. Jean 2.25 Jean 18.25-18.27 Romains 3.19 Ephésiens 4.23 Proverbes 12.19
16 Kisha watu hao wakaondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao awasindikize. Actes 21.5 3 Jean 1.6 Romains 15.24 Actes 15.3 Actes 20.38
17 Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, Amos 3.7 Psaumes 25.14 Jean 15.15 Genèse 19.24 2 Chroniques 20.7
18 akiwa Ibrahimu atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa? Galates 3.8 Genèse 26.4 Genèse 22.17-22.18 Genèse 12.2-12.3 Actes 3.25-3.26
19 Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Deutéronome 4.9-4.10 Ephésiens 6.4 Josué 24.15 Deutéronome 11.19-11.21 Deutéronome 6.6-6.7
20 Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, Genèse 19.13 Esaïe 3.9 Genèse 4.10 Jacques 5.4 Esaïe 5.7
21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. Genèse 11.5 Exode 33.5 Exode 3.8 Genèse 11.7 Josué 22.22
22 Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Genèse 19.1 Psaumes 106.23 Jérémie 18.20 Actes 7.55 1 Timothée 2.1
23 Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Nombres 16.22 2 Samuel 24.17 Genèse 20.4 Psaumes 11.4-11.7 Job 8.3
24 Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Esaïe 1.9 Jérémie 5.1 Actes 27.24 Matthieu 7.13-7.14 Genèse 18.32
25 Hasha usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Job 8.20 Deutéronome 32.4 Esaïe 3.10-3.11 Job 8.3 Psaumes 94.2
26 Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Jérémie 5.1 Esaïe 65.8 Ezéchiel 22.30 Esaïe 10.22 Esaïe 19.24
27 Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Esaïe 6.5 Genèse 3.19 Luc 18.1 Genèse 2.7 Luc 5.8
28 Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Nombres 14.17-14.19 Job 23.3-23.4 Genèse 18.29 Genèse 18.26 1 Rois 20.32-20.33
29 Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Hébreux 4.16 Ephésiens 6.18
30 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. Esaïe 6.5 Psaumes 9.12 Esther 4.11-4.16 Genèse 44.18 Job 40.4
31 Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Hébreux 4.16 Matthieu 7.11 Luc 18.1 Genèse 18.27 Hébreux 10.20-10.22
32 Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. Juges 6.39 Jacques 5.15-5.17 Exode 34.6-34.7 Job 33.23 Proverbes 15.8
33 Basi Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibrahimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi mahali pake. Genèse 32.26 Genèse 31.55 Genèse 18.16 Genèse 18.22

Cette Bible est dans le domaine public.