Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 21.25
Bible en Swahili de l’est


1 Ikawa tulipokwisha kujitenga nao na kuabiri, tukafika Kosi kwa tanga moja, na siku ya pili yake tukafika Rodo na kutoka huko tukafika Patara,1 Thessaloniciens 2.17 Actes 27.4 1 Samuel 20.41-20.42 Luc 5.4 Actes 16.10-16.11
2 tukapata merikebu itakayovuka mpaka Foinike tukapanda tukatweka.Actes 15.3 Actes 11.19 Jonas 1.3 Actes 27.6
3 Na tulipoona Kipro tukaiacha upande wa kushoto; tukasafiri mpaka Shamu tukashuka Tiro. Kwa maana huko ndiko merikebu yetu itakakoshusha shehena yake.Matthieu 4.24 Actes 21.16 Actes 12.20 Actes 4.36 Actes 15.39
4 Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paulo kwa uweza wa Roho asipande kwenda Yerusalemu.Actes 20.22-20.23 Actes 11.26 Actes 21.10-21.12 Actes 20.6-20.7 Apocalypse 1.10
5 Hata tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote, pamoja na wake zao na watoto wao, wakatusindikiza mpake nje ya mji, tukapiga magoti pwani tukaomba;Actes 20.36 Actes 20.38 Actes 15.3 Actes 9.40 Josué 24.15
6 na baada ya kuagana tukapanda merikebuni, nao wakarudi kwao.Jean 19.27 Jean 7.53 2 Corinthiens 2.13 Jean 16.32 Jean 1.11
7 Hata tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro tukafika Tolemai, tukawaamkua ndugu tukakaa kwao siku moja.1 Samuel 10.4 Actes 21.19 Actes 12.20 1 Samuel 13.10 Actes 25.13
8 Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.Actes 6.5 2 Timothée 4.5 Ephésiens 4.11 Actes 8.26-8.40 Actes 8.5-8.13
9 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri.Actes 2.17 Apocalypse 2.20 Joël 2.28 Luc 2.36 Exode 15.20
10 Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi.Actes 11.28 Actes 21.4 Actes 20.16 Actes 21.7
11 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.Actes 21.33 Jérémie 13.1-13.11 Actes 20.23 1 Samuel 15.27-15.28 Actes 28.20
12 Basi tuliposikia haya, sisi na watu wa mahali pale, tukamsihi asipande kwenda Yerusalemu.Matthieu 16.21-16.23 Actes 20.22 Actes 21.4
13 Ndipo Paulo alipojibu, Mnafanya nini, kulia na kunivunja moyo? Kwa maana mimi, licha ya kufungwa, ni tayari hata kuuawa katika Yerusalemu kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.Actes 20.24 Philippiens 2.17 Actes 9.16 Romains 8.35-8.37 Philippiens 1.20-1.21
14 Alipokataa shauri letu, tukanyamaza tukisema, Mapenzi ya Bwana na yatendeke.Luc 22.42 Matthieu 26.42 Matthieu 26.39 Matthieu 6.10 Genèse 43.14
15 Baada ya siku zile tukachukua vyombo vyetu tukapanda kwenda Yerusalemu.Actes 18.22 Actes 25.1 Actes 25.9 Actes 25.6
16 Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakamchukua na Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani ambaye ndiye tutakayekaa kwake.Proverbes 16.31 Actes 21.8 Psaumes 92.14 1 Jean 2.13-2.14 Actes 21.3-21.4
17 Tulipofika Yerusalemu wale ndugu wakatukaribisha kwa furaha.Actes 15.4 Actes 21.7 Hébreux 13.1-13.2 Romains 15.7 3 Jean 1.7-1.8
18 Hata siku ya pili yake Paulo akaingia kwa Yakobo pamoja nasi, na wazee wote walikuwako.Actes 15.13 Actes 11.30 Actes 20.17 Galates 2.9 Galates 1.19
19 Na baada ya kuwaamkua, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyoyatenda katika Mataifa kwa huduma yake.Actes 14.27 Actes 1.17 Romains 15.18-15.19 Actes 15.4 1 Corinthiens 15.10
20 Nao waliposikia wakamtukuza Mungu, wakamwambia, Ndugu yetu, unaona jinsi Wayahudi walioamini walivyo elfu nyingi, nao wote wana wivu sana kwa ajili ya torati.Romains 10.2 Galates 1.14 Actes 22.3 Actes 15.1 Actes 11.18
21 Nao wameambiwa habari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika Mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi.Actes 21.28 1 Corinthiens 9.19-9.21 Galates 6.12-6.15 1 Corinthiens 7.18-7.19 Actes 28.17
22 Basi, ni nini? Bila shaka watasikia kwamba umekuja.Actes 15.12 Actes 19.32 Actes 15.22
23 Basi fanya neno hili tunalokuambia. Wako kwetu watu wanne waliofungwa na nadhiri.Actes 18.18 Nombres 6.2-6.7
24 Wachukue watu hao, ujitakase pamoja nao, na kuwagharimia ili wanyoe vichwa vyao, watu wote wapate kujua ya kuwa habari zile walizoambiwa juu yako si kitu, bali wewe mwenyewe unaenenda vizuri na kuishika torati.Actes 24.18 Actes 21.26 Actes 18.18 2 Chroniques 30.18-30.19 Juges 13.5
25 Lakini kwa habari za watu wa Mataifa walioamini, tuliandika na kutoa hukumu yetu ya wao kujilinda nafsi zao na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na kitu kilichosongolewa, na uasherati.Actes 15.29 Actes 15.19-15.20
26 Ndipo Paulo akawatwaa wanaume wale, na siku ya pili yake akajitakasa nafsi yake pamoja nao, akaingia ndani ya hekalu, akitangaza habari ya kutimiza siku za utakaso, hata sadaka itolewe kwa ajili ya kila mmoja wao.Actes 24.18 Nombres 6.13-6.20 Actes 21.24 1 Corinthiens 9.20
27 Basi zile siku saba zilipokuwa karibu kutimia, Wayahudi waliotoka Asia wakamwona ndani ya hekalu, wakawataharakisha watu wote, wakamkamata,Actes 24.18 Actes 26.21 Actes 13.50 Actes 14.2 Actes 5.18
28 wakapiga kelele, na kusema, Enyi wanaume wa Israeli, tusaidieni. Huyu ndiye mtu yule afundishaye watu wote kila mahali kinyume cha taifa letu na torati na mahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia unajisi mahali hapa patakatifu.Actes 24.5-24.6 Actes 21.21 Actes 24.18 Actes 26.20-26.21 Lamentations 1.10
29 Kwa maana walikuwa wamemwona Trofimo, Mwefeso, pamoja naye mjini, ambaye walidhania ya kuwa Paulo amemwingiza katika hekalu.Actes 20.4 2 Timothée 4.20 Actes 18.19
30 Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni; mara milango ikafungwa.Actes 26.21 Actes 7.57-7.58 Matthieu 21.10 Luc 4.29 Matthieu 2.3
31 Na walipokuwa wakitafuta njia ya kumwua, habari zikamfikilia jemadari wa kikosi ya kwamba Yerusalemu imechafuka, mji mzima.Actes 25.23 Actes 23.17 Actes 24.22 2 Corinthiens 11.23-11.33 Jean 16.2
32 Mara akatwaa askari na maakida, akawashukia mbio. Nao walipomwona jemadari na askari wakaacha kumpiga Paulo.Actes 23.27 Actes 22.19 Actes 23.23-23.24 Actes 24.6 Actes 18.17
33 Kisha jemadari akakaribia, akamshika, akaamuru afungwe kwa minyororo miwili; akauliza, Nani huyu? Tena, amefanya nini?Actes 12.6 Actes 21.11 Actes 20.23 Ephésiens 6.20 Actes 28.20
34 Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.Actes 19.32 Actes 23.10 Actes 22.24 Actes 23.16 Actes 21.37
35 Basi Paulo alipofika darajani ilikuwa kuchukuliwa na askari kwa sababu ya nguvu ya makutano.Habakuk 1.2-1.3 Genèse 6.11-6.12 Actes 21.40 Psaumes 58.2 Psaumes 55.9
36 Maana kundi kubwa la watu wakamfuata, wakipiga kelele, na kusema, Mwondoe huyu.Jean 19.15 Luc 23.18 Actes 22.22 1 Corinthiens 4.13 Actes 7.54
37 Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kiyunani?Actes 19.30 Luc 21.15 Actes 21.34 Actes 21.19 Matthieu 10.18-10.20
38 Wewe si yule Mmisri ambaye kabla ya siku hizi aliwafitinisha wale watu elfu nne, walioitwa Wauaji, akawaongoza jangwani?Matthieu 24.26 Actes 5.36-5.37 1 Corinthiens 4.13 Matthieu 5.11
39 Paulo akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, mtu wa Tarso, mji wa Kilikia, mwenyeji wa mji usiokuwa mnyonge. Nakuomba, nipe ruhusa niseme na wenyeji hawa.Actes 22.3 Actes 9.11 Actes 6.9 Actes 15.23 Actes 23.34
40 Basi, alipompa ruhusa, Paulo akasimama madarajani, akawapungia mkono wale wenyeji; na ilipokuwa kimya kabisa, akanena nao kwa lugha ya Kiebrania, akisema,Actes 12.17 Jean 5.2 Actes 26.14 Actes 22.2 Actes 21.35

Cette Bible est dans le domaine public.