Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 15.9
Bible en Swahili de l’est


1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.Proverbes 25.15 Proverbes 29.22 Proverbes 15.18 1 Samuel 25.21-25.33 1 Rois 12.13-12.16
2 Ulimi wa mwenye hekima hutamka maarifa vizuri; Bali vinywa vya wapumbavu humwaga upumbavu.Proverbes 12.23 Proverbes 13.16 Proverbes 15.28 Esaïe 50.4 Proverbes 25.11-25.12
3 Macho ya Bwana yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.Hébreux 4.13 Jérémie 16.17 2 Chroniques 16.9 Job 31.4 Job 34.21-34.22
4 Ulimi safi ni mti wa uzima; Bali ukorofi wa ulimi huvunja moyo.Proverbes 3.18 Proverbes 16.24 Proverbes 12.18 Genèse 3.22-3.24 Malachie 4.2
5 Mpumbavu hudharau kurudiwa na babaye; Bali yeye aangaliaye maonyo hupata busara.Proverbes 13.18 Proverbes 13.1 Proverbes 15.31-15.32 Proverbes 10.1 1 Chroniques 28.9
6 Katika nyumba ya mwenye haki mna akiba nyingi; Bali mapato ya mtu mbaya huwa taabu tu.Proverbes 8.21 Psaumes 112.3 Proverbes 21.20 Proverbes 10.22 Ecclésiaste 5.10-5.14
7 Midomo ya mwenye haki hueneza maarifa; Bali moyo wa mpumbavu haufanyi hivyo.Matthieu 12.34 Cantique 4.11 Jacques 3.6 Romains 15.18-15.21 Matthieu 28.18-28.20
8 Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.Proverbes 15.29 Proverbes 21.27 1 Chroniques 29.17 Jérémie 6.20 Proverbes 28.9
9 Njia ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali humpenda mtu afuatiaye wema.1 Timothée 6.11 Proverbes 21.21 Habakuk 1.13 Esaïe 51.7 Matthieu 7.13
10 Adhabu kali ina yeye aiachaye njia; Naye achukiaye kukemewa atakufa.Proverbes 12.1 Proverbes 5.12 Proverbes 13.1 1 Rois 22.8 Jean 7.7
11 Kuzimu na Uharibifu vi wazi mbele za Bwana; Si zaidi basi, mioyo ya wanadamu?Psaumes 44.21 2 Chroniques 6.30 Psaumes 139.8 Job 26.6 Jean 2.24-2.25
12 Mwenye mzaha hapendi kukaripiwa; Wala yeye hawaendei wenye hekima.Amos 5.10 Jean 7.7 Jean 3.18-3.21 Job 21.14 Proverbes 9.7-9.8
13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.Proverbes 17.22 Proverbes 18.14 Proverbes 12.25 Proverbes 15.15 Jean 14.1
14 Moyo wa mwenye ufahamu hutafuta maarifa; Bali kinywa cha wapumbavu hula upumbavu.2 Pierre 3.18 Psaumes 119.100 Esaïe 30.10 Psaumes 119.97 Proverbes 18.15
15 Siku zote za mtu ateswaye ni mbaya; Bali ukunjufu wa moyo ni karamu ya daima.Proverbes 15.13 Proverbes 17.22 2 Corinthiens 6.10 Romains 5.11 Romains 5.2-5.3
16 Kuwa na mali chache pamoja na kumcha Bwana; Ni bora kuliko mali nyingi pamoja na taabu.Proverbes 16.8 1 Timothée 6.6 Psaumes 37.16 Ecclésiaste 5.10-5.12 Ecclésiaste 2.10-2.11
17 Chakula cha mboga penye mapendano; Ni bora kuliko ng’ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.Proverbes 17.1 Proverbes 21.19 Psaumes 133.1-133.3 Philippiens 2.1 Luc 15.23
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.Proverbes 26.21 Proverbes 29.22 Matthieu 5.9 Proverbes 15.1 Proverbes 14.29
19 Njia ya mtu mvivu ni kama boma la miiba; Bali mapito yao wenye unyofu hufanyika njia kuu.Proverbes 22.5 Proverbes 26.13 Proverbes 22.13 Esaïe 57.14 Psaumes 5.8
20 Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mpumbavu humdharau mamaye.Proverbes 29.3 Proverbes 10.1 Proverbes 30.17 1 Rois 5.7 Proverbes 23.22
21 Upumbavu ni furaha kwake aliyepungukiwa na akili; Bali mwenye ufahamu huunyosha mwenendo wake.Proverbes 10.23 Ephésiens 5.15 Proverbes 14.16 Proverbes 26.18-26.19 Psaumes 111.10
22 Pasipo mashauri makusudi hubatilika; Bali kwa wingi wa washauri huthibithika.Proverbes 11.14 Proverbes 20.18 Ecclésiaste 8.6
23 Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!Esaïe 50.4 Proverbes 12.14 Ephésiens 4.29 Proverbes 16.13 Proverbes 25.11-25.12
24 Kwa mtu mwenye akili njia ya uhai huenda juu; Ili atoke katika kuzimu chini.Colossiens 3.1-3.2 Philippiens 3.20 Proverbes 2.18 Proverbes 9.8 Psaumes 16.11
25 Bwana ataing’oa nyumba ya mwenye kiburi; Bali atauthibitisha mpaka wa mjane.Psaumes 146.9 Proverbes 23.10 Proverbes 12.7 Psaumes 68.5-68.6 Proverbes 14.11
26 Mashauri mabaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maneno yapendezayo ni safi.Proverbes 15.23 Psaumes 45.1 Proverbes 6.16-6.19 Matthieu 15.19 Psaumes 37.30-37.31
27 Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.Exode 23.8 Proverbes 11.29 Proverbes 1.19 Jérémie 17.11 2 Rois 5.27
28 Moyo wa mwenye haki hufikiri jinsi atakavyojibu; Bali kinywa cha wasio haki humwaga mabaya.1 Pierre 3.15 Proverbes 15.2 Tite 1.10-1.11 Matthieu 12.34 Proverbes 29.11
29 Bwana yu mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.Jean 9.31 Psaumes 145.18-145.19 Proverbes 15.8 1 Pierre 3.12 Jacques 5.16-5.18
30 Mng’ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa.Proverbes 25.25 Esaïe 58.11 Proverbes 3.8 Esdras 9.8 Psaumes 89.15
31 Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai Litakaa kati yao wenye hekima.Proverbes 15.5 Proverbes 25.12 Proverbes 9.8-9.9 Proverbes 1.23 Esaïe 55.3
32 Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.Proverbes 1.24-1.33 Proverbes 1.7 Matthieu 7.24-7.27 Jacques 1.22 Apocalypse 3.19
33 Kumcha Bwana ni maonyo ya hekima; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.Proverbes 18.12 Proverbes 1.7 1 Pierre 5.5 Jacques 4.10 Luc 14.11

Cette Bible est dans le domaine public.