Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Josué 9
Bible en Swahili de l’est


Ruse des Gabaonites

1 Kisha ikawa hapo wafalme wote waliokaa ng’ambo ya pili ya Yordani, hapo penye nchi ya vilima, na katika Shefela, na katika upande wa pwani yote ya bahari kubwa kuikabili Lebanoni, yaani, huyo Mhiti, na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi, waliposikia habari ya mambo hayo;
Nombres 34.6 Exode 3.17 Josué 3.10 Exode 23.23 Josué 1.15
2 ndipo walipojikutanisha pamoja wenyewe kwa wenyewe, ili kupigana na Yoshua, na hao Israeli, kwa nia moja.
Esaïe 8.9-8.10 Psaumes 83.2-83.8 Apocalypse 16.14 Apocalypse 20.8-20.9 Proverbes 11.21
3 Lakini wenyeji wa Gibeoni waliposikia habari ya hayo yote Yoshua aliyokuwa amewatenda watu wa Yeriko, na wa Ai,
Josué 10.2 Josué 9.17 2 Samuel 21.1-21.2 Josué 8.1-8.35 Josué 6.1-6.27
4 wao wakatenda kwa hila, nao wakaenda na kujifanya kama ndio wajumbe, wakaenda na magunia makuukuu juu ya punda zao, na viriba vya mvinyo vilivyokuwa vikuukuu vilivyoraruka-raruka, na kutiwa viraka;
Luc 16.8 Luc 5.37-5.38 Marc 2.22 Genèse 34.13 Matthieu 9.17
5 na viatu vilivyotoboka na kushonwa-shonwa katika miguu yao, na mavao makuukuu waliyokuwa wanavaa; tena mkate wote wa chakula chao ulikuwa umekauka na kuingia koga.
Luc 15.22 Deutéronome 33.25 Josué 9.13 Deutéronome 29.5
6 Nao wakamwendea Yoshua hata maragoni huko Gilgali, nao wakamwambia yeye na watu wa Israeli, Sisi tumetoka nchi ya mbali sana; basi kwa hiyo fanyeni agano pamoja nasi.
Josué 5.10 2 Rois 20.14 Deutéronome 20.11-20.15 Josué 9.9 1 Rois 8.41
7 Basi watu wa Israeli wakawaambia hao Wahivi, Labda mwakaa kati yetu; nasi tutawezaje kufanya agano nanyi?
Josué 11.19 Juges 2.2 Exode 3.8 Genèse 34.2 Genèse 10.17
8 Nao wakamwambia Yoshua, Sisi tu watumishi wako. Yoshua akawauliza, Ninyi ni nani? Nanyi mwatoka wapi?
Deutéronome 20.11 2 Rois 10.5 Josué 9.11 Josué 9.27 Josué 9.23
9 Nao wakamwambia, Sisi watumishi wako twatoka nchi iliyo mbali sana, kwa sababu ya jina la Bwana, Mungu wako; kwa kuwa sisi tumesikia sifa zake, na habari ya hayo yote aliyofanya huko Misri,
Deutéronome 20.15 Josué 9.24 Josué 2.9-2.10 Esaïe 55.5 1 Rois 8.41
10 na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng’ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.
Nombres 21.24-21.35 Deutéronome 1.4 Josué 12.4 Deutéronome 2.30-3.7 1 Chroniques 6.71
11 Kisha wazee wetu, na wenyeji wote wa nchi yetu, walinena nasi na kutuambia, Chukueni vyakula mkononi mwenu kwa ajili ya safari, mwende mkawalaki watu hao, na kuwaambia, Sisi tu watumishi wenu; basi sasa fanyeni agano nasi.
Esther 8.17 Josué 9.8 Josué 1.11 Matthieu 10.9-10.10 Luc 9.3
12 Huu mkate wetu tuliutwaa ukali moto katika nyumba zetu, siku hiyo tuliyotoka kuja kwenu, uwe chakula chetu; lakini sasa, tazama, umekauka, na kuingia koga;
Josué 9.4-9.5
13 na viriba vyetu hivi, tulivyovitia divai, vilikuwa ni vipya; sasa, tazama, vimeraruka-raruka; na haya mavazi yetu na viatu vyetu vimekuwa vikuukuu kwa vile tulivyokuja safari ya mbali sana.
14 Basi hao watu wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa Bwana.
Nombres 27.21 Juges 1.1 Juges 20.18 Jacques 1.5 1 Samuel 30.7-30.8
15 Naye Yoshua akafanya amani pamoja nao, na kufanya agano nao, ili kwamba waachwe hai; na wakuu wa mkutano wakawaapia.
2 Samuel 21.2 Josué 11.19 Exode 23.32 Deutéronome 20.10-20.11 Josué 2.12-2.19
16 Kisha ikawa, mwisho wa siku ya tatu baada ya kufanya hilo agano nao, walisikia habari ya kuwa watu hao ni jirani zao, na ya kwamba waliketi kati yao.
Proverbes 12.19
17 Kisha wana wa Israeli walisafiri, wakaifikilia miji ya watu hao siku ya tatu. Basi miji ya watu hao ilikuwa ni hii, Gibeoni, na Kefira, na Beerothi, na Kiriath-yearimu.
1 Samuel 7.1 Esdras 2.25 Josué 18.25-18.28 Néhémie 7.29 Josué 15.9
18 Wana wa Israeli hawakuwapiga, kwa sababu wakuu wa mkutano walikuwa wamekwisha kuwaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli. Nao mkutano wote wakawanung’unikia hao wakuu.
Psaumes 15.4 Ecclésiaste 9.2 Ecclésiaste 5.2 Ecclésiaste 5.6 2 Samuel 21.7
19 Lakini wakuu wote waliwaambia mkutano wote, Sisi tumewaapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli; basi sasa hatuwezi kuwagusa watu hawa.
Ecclésiaste 9.2 Ecclésiaste 8.2 Josué 9.20 Jérémie 4.2
20 Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho kiapo tulichowaapia.
2 Samuel 21.1-21.6 Ezéchiel 17.12-17.21 Malachie 3.5 Proverbes 20.25 Zacharie 5.3-5.4
21 Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia.
Deutéronome 29.11 Josué 9.27 Josué 9.23 2 Chroniques 2.17-2.18 Josué 9.15
22 Basi Yoshua akawaita, akanena nao, na kuwaambia, Mbona ninyi mmetudanganya, huku mkisema, Sisi tu mbali sana na ninyi; nanyi kumbe! Mwakaa kati yetu?
Josué 9.6 Josué 9.16 Genèse 27.35-27.36 Genèse 3.13-3.14 Genèse 29.25
23 Basi sasa mmelaaniwa kisha hatakosekana kuwapo mtu wa kwenu aliye mtumwa, wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya nyumba ya Mungu wangu.
Josué 9.27 Josué 9.21 Genèse 9.25-9.26 Lévitique 27.28-27.29
24 Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, Ni kwa sababu ya sisi watumishi wako kuambiwa hakika, jinsi huyo Bwana, Mungu wako alivyomwamuru mtumishi wake Musa kuwapa ninyi nchi hii yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi hii watoke mbele zenu; kwa sababu hii tuliogopa mno kwa ajili ya uhai wetu kwa sababu yenu, nasi tumefanya neno hili.
Exode 23.31-23.33 Deutéronome 7.1-7.2 Deutéronome 20.15-20.17 Nombres 33.51-33.52 Nombres 33.55-33.56
25 Basi sasa, tazama, sisi tu mkononi mwako; basi kama uonavyo kuwa ni vyema na haki kwako wewe kututenda, tutende vivyo.
Genèse 16.6 Juges 10.15 Jérémie 26.14 Esaïe 47.6 Jérémie 38.5
26 Naye akawafanyia hivyo, na kuwaokoa na mkono wa wana wa Israeli, ili wasiwaue.
27 Siku iyo hiyo Yoshua akawafanya kuwa ni wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano, na kwa ajili ya madhabahu ya Bwana, hata siku hii ya leo, katika mahali hapo atakapopachagua.
Deutéronome 12.5

Cette Bible est dans le domaine public.