Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 26.7
Bible en Swahili de l’est


1 Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.Esaïe 60.18 Jérémie 33.11 Psaumes 31.21 Esaïe 62.11 Esaïe 27.1-27.2
2 Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.Esaïe 60.11 Actes 2.47 Esaïe 62.10 Esaïe 54.14 Esaïe 62.2
3 Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.Philippiens 4.7 Jean 14.27 Jean 16.33 Psaumes 9.10 Romains 4.18-4.21
4 Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.Esaïe 12.2 Philippiens 4.13 Esaïe 50.10 Psaumes 62.8 Psaumes 55.22
5 Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, Mji ule ulioinuka, aushusha, Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.Job 40.11-40.13 Esaïe 14.13 Jérémie 51.37 Jérémie 50.31-50.32 Esaïe 25.11-25.12
6 Mguu utaukanyaga chini, Naam, miguu yao walio maskini, Na hatua zao walio wahitaji.Luc 10.19 Esaïe 25.10 Jacques 2.5 Apocalypse 2.26 Esaïe 3.15
7 Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.1 Samuel 2.2-2.4 Ephésiens 2.10 Psaumes 18.23-18.26 Esaïe 42.16 1 Jean 3.10
8 Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee Bwana; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.Exode 3.15 Cantique 5.8 Psaumes 37.3-37.7 Cantique 1.2-1.4 Psaumes 73.25
9 Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.Matthieu 6.33 Psaumes 63.1 Luc 6.12 Osée 5.15 Proverbes 8.17
10 Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa Bwana.Jean 5.37-5.38 Osée 11.7 Esaïe 32.6 Exode 9.34 Michée 2.10
11 Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.Esaïe 5.24 Michée 5.9 Esaïe 60.14 Luc 16.23 Actes 28.27
12 Bwana, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.Deutéronome 30.6 Ezéchiel 20.14 Ezéchiel 36.25 Ezéchiel 20.9 Esaïe 57.10
13 Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.Esaïe 2.8 1 Corinthiens 4.7 Josué 23.7 Romains 6.22 Esaïe 51.22
14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.Esaïe 8.19 Apocalypse 19.19-19.21 Apocalypse 18.2-18.3 Matthieu 2.20 Deutéronome 4.28
15 Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.Esaïe 9.3 Esaïe 54.2-54.3 Esaïe 33.17 Deutéronome 4.27-4.28 Jean 12.23-12.28
16 Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.Osée 5.15 Osée 7.14 Psaumes 91.15 1 Samuel 1.15 2 Chroniques 6.37-6.38
17 Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee Bwana.Jean 16.21 Esaïe 13.8 1 Thessaloniciens 5.3 Esaïe 21.3 Jérémie 4.31
18 Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.Psaumes 17.14 Exode 5.22-5.23 1 Samuel 14.45 Esaïe 37.3 Esaïe 33.11
19 Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.Daniel 12.2 Ezéchiel 37.1-37.14 Ephésiens 5.14 Osée 13.14 Esaïe 25.8
20 Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.Psaumes 91.4 Psaumes 30.5 Esaïe 54.7-54.8 Psaumes 91.1 2 Corinthiens 4.17
21 Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.Job 16.18 Ezéchiel 9.3-9.6 Apocalypse 18.24 Apocalypse 16.6 Psaumes 50.2-50.3

Cette Bible est dans le domaine public.