Proverbes de Lemuel
Conseils d’une mère
 1  Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake. 
Proverbes 6.20  2 Timothée 1.5  2 Timothée 3.15  Proverbes 1.8  Proverbes 30.1  
 2  Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu? 
Esaïe 49.15  1 Samuel 1.11  1 Samuel 1.28  
 3  Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme. 
Néhémie 13.26  Deutéronome 17.17  Proverbes 5.9-5.11  1 Rois 11.1  Proverbes 7.26-7.27  
 4  Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo? 
Ecclésiaste 10.17  Proverbes 20.1  Esaïe 5.22  Esaïe 28.7-28.8  Habakuk 2.5  
 5  Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. 
Habakuk 2.5  
 6  Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini. 
1 Timothée 5.23  1 Samuel 30.6  Job 3.20  Psaumes 104.15  2 Rois 4.27  
 7  Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake. 
Ephésiens 5.18  
 8  Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao; 
Psaumes 82.3-82.4  Proverbes 24.11-24.12  Jérémie 26.16-26.19  Jérémie 26.24  Jean 7.51  
 9  Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao. 
Esaïe 1.17  Deutéronome 1.16  Lévitique 19.15  Job 29.15-29.16  Jérémie 22.15-22.16  
Une femme de valeur
 10  Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani. 
Proverbes 19.14  Proverbes 12.4  Proverbes 18.22  Ruth 3.11  Ephésiens 5.25-5.33  
 11  Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato. 
2 Rois 4.9-4.10  1 Pierre 3.1-3.7  2 Rois 4.22-4.23  
 12  Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake. 
1 Samuel 25.26-25.27  1 Samuel 25.18-25.22  
 13  Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo. 
1 Timothée 5.10  Genèse 29.9-29.10  Genèse 24.13-24.14  Ruth 2.23  Esaïe 32.9-32.11  
 14  Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali. 
1 Rois 9.26-9.28  Proverbes 31.24  Ezéchiel 27.3-27.36  2 Chroniques 9.10  
 15  Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. 
Luc 12.42  Romains 12.11  Marc 1.35  Proverbes 20.13  Ecclésiaste 9.10  
 16  Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu. 
Matthieu 13.44  Josué 15.18  Cantique 8.12  
 17  Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu. 
1 Rois 18.46  Job 38.3  2 Rois 4.29  1 Pierre 1.13  Genèse 49.24  
 18  Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku. 
Psaumes 127.2  2 Thessaloniciens 3.7-3.9  Genèse 31.40  1 Thessaloniciens 2.9  Matthieu 25.3-25.10  
 19  Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia. 
Exode 35.25-35.26  
 20  Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake. 
Ephésiens 4.28  Proverbes 22.9  Hébreux 13.16  Job 31.16-31.20  Marc 14.7  
 21  Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu. 
Proverbes 25.20  Genèse 45.22  2 Samuel 1.24  
 22  Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani. 
Genèse 41.42  Proverbes 7.16  Apocalypse 19.14  Psaumes 45.13-45.14  Esther 5.1  
 23  Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi. 
Ruth 4.1  Proverbes 12.4  Deutéronome 16.18  Ruth 4.11  Deutéronome 21.19  
 24  Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi. 
Ezéchiel 27.16  Proverbes 31.19  1 Rois 10.28  Proverbes 31.13  Luc 16.19  
 25  Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. 
Job 40.10  Psaumes 132.16  Esaïe 65.13-65.14  Esaïe 61.10  Job 29.14  
 26  Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake. 
Proverbes 10.31  Ephésiens 4.29  Cantique 2.14  Juges 13.23  Luc 1.42-1.56  
 27  Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. 
Proverbes 14.1  Tite 2.4  1 Timothée 5.10  1 Thessaloniciens 4.11  2 Thessaloniciens 3.6  
 28  Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, 
2 Timothée 3.15-3.17  Proverbes 31.1  1 Rois 2.19  Esaïe 62.4-62.5  Psaumes 116.16  
 29  Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. 
Cantique 6.8-6.9  Ephésiens 5.27  
 30  Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa. 
1 Pierre 3.4-3.5  Proverbes 11.22  Proverbes 6.25  Psaumes 147.11  Luc 1.6  
 31  Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni. 
Matthieu 7.16  Matthieu 7.20  Romains 6.21-6.22  Hébreux 6.10  Romains 16.12