Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Proverbes 31.17
Bible en Swahili de l’est


1 Maneno ya mfalme Lemueli; mausia aliyofundishwa na mama yake.Proverbes 6.20 Proverbes 1.8 2 Timothée 1.5 2 Timothée 3.15 Proverbes 30.1
2 Ni nini, mwanangu? Tena ni nini, mwana wa tumbo langu? Tena, ni nini mwana wa nadhiri zangu?Esaïe 49.15 1 Samuel 1.11 1 Samuel 1.28
3 Usiwape wanawake nguvu zako; Wala moyo wako usiwape wale wawaharibuo wafalme.Néhémie 13.26 Deutéronome 17.17 Proverbes 5.9-5.11 Proverbes 7.26-7.27 Osée 4.11
4 Ee Lemueli, kunywa mvinyo hakuwafai wafalme, hakuwafai wafalme; Wala haifai wakuu waseme, Ki wapi kileo?Ecclésiaste 10.17 Proverbes 20.1 Esaïe 5.22 Osée 4.11-4.12 Esaïe 28.7-28.8
5 Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni.Habakuk 2.5
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.1 Timothée 5.23 2 Rois 4.27 1 Samuel 1.10 Job 29.13 1 Samuel 30.6
7 Anywe akausahau umaskini wake; Asiikumbuke tena taabu yake.Ephésiens 5.18
8 Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu; Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;Psaumes 82.3-82.4 1 Samuel 22.14-22.15 Jérémie 38.7-38.10 Proverbes 24.11-24.12 Jérémie 26.16-26.19
9 Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki; Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.Esaïe 1.17 Deutéronome 1.16 Lévitique 19.15 Job 29.15-29.16 Jérémie 22.15-22.16
10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.Proverbes 19.14 Proverbes 12.4 Proverbes 18.22 Ruth 3.11 Proverbes 8.11
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.2 Rois 4.9-4.10 1 Pierre 3.1-3.7 2 Rois 4.22-4.23
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.1 Samuel 25.26-25.27 1 Samuel 25.18-25.22
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.1 Timothée 5.10 Ruth 2.2-2.3 Tite 2.5 Actes 9.39-9.40 1 Thessaloniciens 4.11
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.1 Rois 9.26-9.28 Proverbes 31.24 Ezéchiel 27.3-27.36 2 Chroniques 9.10
15 Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.Romains 12.11 Luc 12.42 2 Chroniques 36.15 Psaumes 119.147-119.148 Josué 3.1
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.Matthieu 13.44 Josué 15.18 Cantique 8.12
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.2 Rois 4.29 1 Pierre 1.13 1 Rois 18.46 Job 38.3 Ephésiens 6.14
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.Matthieu 25.3-25.10 Psaumes 127.2 2 Thessaloniciens 3.7-3.9 Genèse 31.40 1 Thessaloniciens 2.9
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.Exode 35.25-35.26
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.Ephésiens 4.28 Proverbes 22.9 Hébreux 13.16 Job 31.16-31.20 Psaumes 41.1
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.Proverbes 25.20 Genèse 45.22 2 Samuel 1.24
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.Genèse 41.42 Proverbes 7.16 Apocalypse 19.14 Ezéchiel 16.10-16.13 1 Pierre 3.3
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.Ruth 4.1 Deutéronome 16.18 Proverbes 12.4 Job 29.7 Proverbes 24.7
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.Ezéchiel 27.16 Luc 16.19 Juges 14.12 Proverbes 31.19 1 Rois 10.28
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.1 Pierre 5.5-5.6 Psaumes 97.11-97.12 Psaumes 132.9 Job 40.10 Psaumes 132.16
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.Proverbes 10.31 Ephésiens 4.29 Esther 8.3-8.6 Malachie 2.6 Proverbes 31.8-31.9
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.Proverbes 14.1 1 Timothée 5.10 Tite 2.4 1 Thessaloniciens 4.11 2 Thessaloniciens 3.6
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,2 Timothée 3.15-3.17 Psaumes 116.16 Cantique 7.1-7.9 Proverbes 31.1 1 Rois 2.19
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.Cantique 6.8-6.9 Ephésiens 5.27
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.1 Pierre 3.4-3.5 Proverbes 6.25 Proverbes 11.22 2 Samuel 14.25 Psaumes 147.11
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.Romains 16.6 Apocalypse 14.13 1 Timothée 5.25 Marc 14.7-14.9 Philippiens 4.17

Cette Bible est dans le domaine public.