Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 3.19
Bible en Swahili de l’est


1 Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake.Jérémie 20.14-20.15 Psaumes 106.33 Psaumes 39.2-39.3 Job 2.9-2.10 Job 3.3
2 Ayubu akajibu, na kusema;Juges 18.14
3 Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi, Na ule usiku uliosema, Mtoto mume ametungishwa mimba.Jérémie 20.14-20.18 Job 10.18-10.19 Jérémie 15.10
4 Siku hiyo na iwe giza; Mungu asiiangalie toka juu, Wala mwanga usiiangazie.Actes 27.20 Exode 10.22-10.23 Amos 5.18 Matthieu 27.45 Joël 2.2
5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake; Wingu na likae juu yake; Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.Job 10.21-10.22 Psaumes 23.4 Jérémie 13.16 Job 28.3 Esaïe 9.2
6 Tena usiku huo, na ushikwe na giza kuu; Usihesabiwe katika siku za mwaka; Wala kutiwa katika hesabu ya miezi. 7 Tazama, usiku huo na uwe tasa; Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe.Apocalypse 18.22-18.23 Jérémie 7.34 Esaïe 24.8 Esaïe 13.20-13.22
8 Na waulaani hao waulaanio mchana, Hao walio tayari kumwamsha huyo lewiathani.Job 41.1 Job 41.10 2 Chroniques 35.25 Marc 5.38 Matthieu 11.17
9 Nyota za mapambazuko yake na ziwe giza; Na utafute mwanga lakini usiupate; Wala usiyaone makope ya asubuhi;Job 41.18 Job 30.26 Jérémie 13.16 Jérémie 8.15
10 Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu. Wala kunifichia taabu machoni.Job 23.2 Genèse 20.18 Ecclésiaste 6.3-6.5 Job 10.1 Ecclésiaste 11.10
11 Mbona si kufa mimi tokea mimbani? Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni?Job 10.18-10.19 Jérémie 15.10 Psaumes 22.9-22.10 Psaumes 58.8 Esaïe 46.3
12 Mbona hayo magoti kunipokea? Au hayo maziwa, hata nikanyonya?Esaïe 66.12 Genèse 30.3 Genèse 50.23 Ezéchiel 16.4-16.5
13 Maana hapo ningelala na kutulia; Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;Job 19.27 Job 14.10-14.12 Ecclésiaste 9.10 Job 7.21 Job 21.23
14 Pamoja na wafalme na washauri wa dunia, Hao waliojijengea maganjoni;Job 15.28 Esaïe 14.10-14.16 Esaïe 58.12 Ecclésiaste 8.8 Psaumes 89.48
15 Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza fedha nyumba zao;Zacharie 9.3 Sophonie 1.18 Job 12.21 Esaïe 2.7 Job 22.25
16 Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako; Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.Psaumes 58.8 1 Corinthiens 15.8 Ecclésiaste 6.3
17 Huko waovu huacha kusumbua; Huko nako hao waliochoka wapumzikaJob 17.16 Apocalypse 14.13 2 Pierre 2.8 Psaumes 55.5-55.8 Matthieu 10.28
18 Huko wafungwa waona raha pamoja; Hawaisikii sauti yake msimamizi.Job 39.7 Esaïe 14.3-14.4 Juges 4.3 Exode 5.15-5.19 Exode 5.6-5.8
19 Wakuu na wadogo wako huko; Mtumishi yu huru kwa bwana wake.Psaumes 49.14-49.20 Ecclésiaste 12.5 Luc 16.22-16.23 Ecclésiaste 8.8 Hébreux 9.27
20 Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga, Na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai;Jérémie 20.18 Job 7.15-7.16 Proverbes 31.6 1 Samuel 1.10 Job 3.16
21 Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati; Na kuyachimbulia zaidi ya kutafuta hazina iliyostirika;Apocalypse 9.6 Proverbes 2.4 Jonas 4.8 Jonas 4.3 Nombres 11.15
22 Ambao wafurahi mno, Na kushangilia watakapoliona kaburi? 23 Kwa nini mtu aliyezibiwa njia kupewa mwanga, Ambaye Mungu amemzingira kwa ukingo?Job 19.8 Lamentations 3.7 Esaïe 40.27 Psaumes 88.8 Job 19.12
24 Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.Psaumes 102.9 Psaumes 80.5 Psaumes 38.8 Psaumes 42.3-42.4 Esaïe 59.11
25 Maana jambo hilo nichalo hunipata, Nalo linitialo hofu hunijilia.Job 1.5 Job 30.15 Job 31.23
26 Mimi sioni raha, wala situlii, wala kupumzika; Lakini huja taabu.Job 7.14 Psaumes 143.11 Job 27.9

Cette Bible est dans le domaine public.