Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 20.1
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Sofari, Mnaamathi, akajibu, na kusema,Job 2.11 Job 11.1 Job 42.9
2 Kwa hiyo mawazo yangu hunipa jawabu, Kwa ajili ya haraka niliyo nayo ndani yangu.Psaumes 31.22 Ecclésiaste 7.9 Proverbes 29.20 Romains 10.2 Psaumes 39.2-39.3
3 Nimesikia maonyo yanayonitahayarisha, Nayo roho ya ufahamu wangu hunijibu.Psaumes 49.3 Job 33.3 Job 27.11 Job 20.2 Psaumes 78.2-78.5
4 Je! Hujui neno hili tangu zamani za kale, Tangu wanadamu kuwekwa juu ya nchi,Job 32.7 Psaumes 115.16 Job 15.10 Job 8.8-8.9 Genèse 1.28
5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo, Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?Psaumes 37.35-37.36 Job 8.12-8.13 Jacques 4.16 Psaumes 73.18-73.20 Exode 15.9-15.10
6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni, Na kichwa chake kufikilia mawinguni;Esaïe 14.13-14.14 Abdias 1.3-1.4 Genèse 11.4 Amos 9.2 Daniel 4.22
7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?Psaumes 83.10 2 Rois 9.37 Job 14.10 1 Rois 14.10 Job 4.20
8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,Psaumes 73.20 Psaumes 90.5 Esaïe 29.7-29.8 Psaumes 18.10 Job 18.18
9 Jicho lililomwona halitamwona tena; Wala mahali pake hapatamtazama tena.Job 7.8 Job 7.10 Psaumes 37.10 Job 8.18 Psaumes 37.36
10 Watoto wake watataka fadhili kwa maskini, Na mikono yake itarudisha mali yake.Job 20.18 Job 27.16-27.17 Exode 9.2 Exode 22.1 Job 5.4
11 Mifupa yake imejaa ujana wake, Lakini utalala nchi naye mavumbini.Job 21.26 Job 13.26 Psaumes 25.7 Jean 8.24 Ezéchiel 32.27
12 Ingawa uovu una tamu kinywani mwake, Ingawa auficha chini ya ulimi wake;Psaumes 10.7 Job 15.16 Proverbes 20.17 Psaumes 109.17-109.18 Genèse 3.6
13 Ingawa auhurumia, asikubali kuuacha uende zake. Lakini akaushika vivyo kinywani mwake;Marc 9.43-9.49 Matthieu 5.29-5.30 Nombres 11.18-11.20 Romains 8.13
14 Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.Psaumes 51.8-51.9 Malachie 2.2 Job 20.16 Proverbes 23.20-23.21 Proverbes 23.29-23.35
15 Amemeza mali, naye atayatapika tena; Mungu atayatoa tumboni mwake.Proverbes 23.8 Matthieu 27.3-27.4
16 Ataamwa sumu ya majoka; Na ulimi wa fira utamwua.Romains 3.13 Actes 28.3-28.6 Matthieu 3.7 Deutéronome 32.24 Esaïe 30.6
17 Hataiangalia hiyo mito ya maji, Vile vijito vilivyojaa asali na siagi.Deutéronome 32.13-32.14 Job 29.6 2 Rois 7.2 2 Samuel 17.29 Nombres 14.23
18 Aliyoyataabikia kazi atayarudisha, asiyameze; Kwa mali aliyoyapata, hatafurahi.Job 20.15 Job 20.10 Jérémie 51.34 Osée 9.1 Matthieu 23.13
19 Kwa maana amewaonea na kuwaacha maskini; Amenyang’anya nyumba kwa jeuri, wala hataijenga.Job 35.9 Proverbes 14.31 Proverbes 22.22-22.23 Michée 2.2 Job 31.38-31.39
20 Kwa sababu hakujua utulivu ndani yake, Hataponya cho chote katika hicho alichokifurahia.Ecclésiaste 5.13-5.14 Esaïe 57.20-57.21
21 Hakikusalia kitu asichokula; Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.Job 18.19 Luc 16.24-16.25 Job 15.29 Jérémie 17.11
22 Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki; Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia.Job 3.17 Ecclésiaste 2.18-2.20 Esaïe 10.6 Apocalypse 18.7 Job 18.7
23 Hapo atakapo kulijaza tumbo lake, Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake, Na kuunyesha juu yake akiwa anakula.Psaumes 78.30-78.31 Nombres 11.33 Esaïe 21.4 Exode 9.23 Genèse 19.24
24 Ataikimbia silaha ya chuma, Na uta wa shaba utamchoma kwa pili.Amos 5.19 Esaïe 24.18 2 Samuel 22.35 Proverbes 7.23 Jérémie 48.43-48.44
25 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake; Naam, ncha ing’aayo yatoka katika nyongo yake; Vitisho viko juu yake.Job 16.13 Job 18.11 Deutéronome 32.41 Job 6.4 Psaumes 7.12
26 Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake; Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla; Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.Psaumes 21.9 Matthieu 8.12 Esaïe 8.22 Matthieu 3.12 Psaumes 120.4
27 Mbingu zitafunua wazi uovu wake, Nayo nchi itainuka kinyume chake.Job 16.18 Esaïe 26.21 Job 18.18 1 Corinthiens 4.5 Psaumes 44.20-44.21
28 Maongeo ya nyumba yake yataondoka, Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake.Deutéronome 28.31 Jacques 5.1-5.3 Job 20.18-20.22 Job 21.30 Proverbes 11.4
29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu, Na urithi aliowekewa na Mungu.Job 27.13 Job 31.2-31.3 Job 18.21 Lamentations 3.38 Deutéronome 29.20-29.28

Cette Bible est dans le domaine public.