Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Exode 1.11
Bible en Swahili de l’est


1 Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo.Genèse 46.8-46.26 Genèse 35.23-35.26 1 Chroniques 2.1-2.2 Genèse 49.3-49.27 Genèse 35.18
2 Reubeni, na Simeoni na Lawi, na Yuda;Genèse 35.22
3 na Isakari, na Zabuloni, na Benyamini;Exode 28.20 Genèse 35.23
4 na Dani, na Naftali, na Gadi, na Asheri. 5 Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo.Deutéronome 10.22 Genèse 46.26-46.27 Exode 1.20 Juges 8.30
6 Yusufu akafa, na ndugu zake wote, na watu wote wa kizazi kile.Genèse 50.26 Actes 7.14-7.16 Genèse 50.24
7 Na wana wa Israeli walikuwa na uzazi sana, na kuongezeka mno, na kuzidi kuwa wengi, nao wakaendelea na kuongezeka nguvu; na ile nchi ilikuwa imejawa na wao.Genèse 46.3 Genèse 35.11 Genèse 12.2 Deutéronome 26.5 Genèse 47.27
8 Basi akainuka mfalme mpya kutawala Misri, asiyemjua Yusufu.Actes 7.18 Ecclésiaste 2.18-2.19 Ecclésiaste 9.15
9 Akawaambia watu wake, Angalieni, watu wa wana wa Israeli ni wengi tena wana nguvu kuliko sisi.Psaumes 105.24-105.25 Jacques 3.14-3.16 Jacques 4.5 Ecclésiaste 4.4 Nombres 22.4-22.5
10 Haya! Na tuwatendee kwa akili, wasije wakaongezeka; tena, ikitokea vita, wao nao wasije wakashikamana na adui zetu na kupigana nasi, na kutoka katika nchi hii.Actes 7.19 Psaumes 105.25 Psaumes 83.3-83.4 Nombres 22.6 Proverbes 1.11
11 Basi wakaweka wasimamizi juu yao wawatese kwa mizigo yao. Nao wakamjengea Farao miji ya kuwekea akiba, Pithomu na Ramesesi.Genèse 15.13 Genèse 47.11 Exode 3.7 Exode 2.11 Deutéronome 26.6
12 Lakini kwa kadiri ya walivyowatesa ndivyo walivyoongezeka na kuzidi kuenea. Nao walichukiwa kwa sababu ya wana wa Israeli.Actes 4.2-4.4 Exode 1.9 Psaumes 105.24 Hébreux 12.6-12.11 Job 5.2
13 Wamisri wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali;Deutéronome 4.20
14 wakafanya maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.Exode 6.9 Exode 2.23 Actes 7.19 Nombres 20.15 Psaumes 81.6
15 Kisha mfalme wa Misri akasema na wazalisha wa Waebrania, mmoja jina lake aliitwa Shifra, na wa pili jina lake aliitwa Pua; 16 akasema, Wakati mwazalishapo wanawake wa Kiebrania na kuwaona wa katika kuzaa, ikiwa ni mtoto mwanamume, basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto mwanamke, na aishi.Exode 1.22 Apocalypse 12.4 Matthieu 21.38
17 Lakini wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, wasifanye kama walivyoamriwa na huyo mfalme wa Misri, lakini wakawahifadhi hai wale wanaume.Actes 5.29 Daniel 3.16-3.18 Proverbes 16.6 Daniel 6.13 Exode 1.21
18 Basi mfalme wa Misri akawaita wale wazalisha na kuwauliza, Kwa nini kufanya jambo hili, na kuwahifadhi watoto waume wawe hai?Ecclésiaste 8.4 2 Samuel 13.28
19 Wazalisha wakamwambia Farao, Ni kwa sababu hao wanawake wa Kiebrania si kama wanawake wa Kimisri; kwa kuwa ni hodari hao, nao huzaa kabla mzalisha hajapata kuwafikilia.2 Samuel 17.19-17.20 Josué 2.4-2.24 1 Samuel 21.2
20 Basi Mungu akawatendea mema wale wazalisha; na hao watu wakaongezeka sana, wakaendelea na kuzidi kuwa na nguvu nyingi.Exode 1.12 Esaïe 3.10 Ecclésiaste 8.12 Proverbes 11.18 Hébreux 6.10
21 Ilikuwa kwa sababu wale wazalisha walikuwa wakimcha Mungu, akawasimamishia nyumba.1 Samuel 2.35 1 Rois 11.38 1 Rois 2.24 2 Samuel 7.27-7.29 Psaumes 127.1
22 Kisha huyo Farao akawaagiza watu wake, akisema, Kila mtoto mwanamume atakayezaliwa mtamtupa mtoni, na kila mtoto mwanamke mtamhifadhi hai.Actes 7.19 Proverbes 27.4 Psaumes 105.25 Apocalypse 16.4-16.6 Exode 7.19-7.21

Cette Bible est dans le domaine public.