Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 25.3
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, nakuinulia nafsi yangu,Psaumes 143.8 Psaumes 86.4 Psaumes 24.4 1 Samuel 1.15 Lamentations 3.41
2 Ee Mungu wangu, Nimekutumaini Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.Psaumes 41.11 Psaumes 31.1 Esaïe 49.23 Psaumes 71.1 Esaïe 26.3
3 Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.Lamentations 3.25 Esaïe 49.23 Psaumes 62.5 Esaïe 40.31 Michée 7.7
4 Ee Bwana, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako,Psaumes 27.11 Exode 33.13 Psaumes 86.11 Psaumes 5.8 Psaumes 143.8
5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.Psaumes 88.1 Psaumes 79.9 Apocalypse 7.17 Esaïe 30.18 Psaumes 25.10
6 Ee Bwana, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.Psaumes 103.17 Psaumes 69.16 Esaïe 63.15 Psaumes 98.3 Psaumes 107.1
7 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee Bwana kwa ajili ya wema wako.Psaumes 51.1 Job 13.26 Job 20.11 Jérémie 3.25 Esaïe 43.25
8 Bwana yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.Psaumes 92.15 Psaumes 32.8 Jacques 1.5 Matthieu 9.13 Matthieu 11.29-11.30
9 Wenye upole atawaongoza katika hukumu, Wenye upole atawafundisha njia yake.Jean 14.6 Psaumes 76.9 Psaumes 147.6 Psaumes 149.4 Ezéchiel 11.19-11.20
10 Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.Jean 1.17 Hébreux 12.14 Hébreux 8.8-8.12 Esaïe 43.2 Esaïe 25.1
11 Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.Psaumes 31.3 Psaumes 79.9 Esaïe 43.25 Psaumes 109.21 Romains 5.20-5.21
12 Ni nani amchaye Bwana? Atamfundisha katika njia anayoichagua.Psaumes 37.23 2 Thessaloniciens 2.10-2.12 Proverbes 2.5 Jean 3.20-3.21 Psaumes 32.8
13 Nafsi yake itakaa hali ya kufanikiwa; Wazao wake watairithi nchi.Psaumes 37.11 Proverbes 1.33 Proverbes 19.23 Proverbes 29.25 Psaumes 37.26
14 Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.Jean 7.17 Proverbes 3.32 Genèse 18.17-18.19 Colossiens 3.3 Jean 15.15
15 Macho yangu humwelekea Bwana daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.Psaumes 141.8 Psaumes 31.4 Psaumes 123.2 Jérémie 5.26 2 Timothée 2.25-2.26
16 Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa.Psaumes 143.4 Psaumes 86.16 Psaumes 69.14-69.20 Psaumes 88.15-88.18 Marc 15.33-15.35
17 Katika shida za moyo wangu unifanyie nafasi, Na kunitoa katika dhiki zangu.Psaumes 77.2-77.4 2 Corinthiens 4.8-4.9 Psaumes 38.1-38.8 Psaumes 42.7 Psaumes 34.19
18 Utazame teso langu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.2 Samuel 16.12 Psaumes 32.1-32.5 Psaumes 119.153 Psaumes 119.132 Psaumes 51.8-51.9
19 Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Wananichukia kwa machukio ya ukali.Psaumes 52.2 Psaumes 140.1 Psaumes 27.12 Psaumes 56.2 Psaumes 140.11
20 Unilinde nafsi yangu na kuniponya, Nisiaibike, maana nakukimbilia Wewe.Actes 7.59 Psaumes 121.7 Psaumes 22.20-22.21 Luc 23.46 Psaumes 71.1-71.2
21 Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe.Psaumes 41.12 Proverbes 20.7 Actes 24.16 Psaumes 26.11 Actes 25.10-25.11
22 Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote.Psaumes 130.8 Psaumes 51.18-51.19 Psaumes 122.6 Psaumes 14.7

Cette Bible est dans le domaine public.