Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Pierre 3.10
Bible en Swahili de l’est


1 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno;Colossiens 3.18 1 Corinthiens 7.16 Genèse 3.16 1 Corinthiens 11.3 Ephésiens 5.33
2 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu.1 Pierre 2.12 Philippiens 1.27 1 Timothée 4.12 Ephésiens 6.5 1 Pierre 3.15-3.16
3 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;1 Timothée 2.9-2.10 Esaïe 3.18-3.24 Tite 2.3-2.15 Ezéchiel 16.7-16.13 Genèse 24.53
4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.Romains 2.29 Romains 7.22 1 Samuel 16.7 Tite 3.2 Colossiens 3.12
5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.1 Timothée 5.5 Tite 2.3-2.4 1 Timothée 2.10 1 Samuel 2.1 1 Timothée 2.15
6 Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote.Genèse 18.12 Daniel 3.16-3.18 Actes 4.8-4.13 1 Pierre 3.14-3.15 Genèse 18.15
7 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.Colossiens 3.19 Ephésiens 5.33 Malachie 2.14-2.16 Ephésiens 5.25-5.28 1 Thessaloniciens 4.4
8 Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;Ephésiens 4.31-5.2 Romains 12.10 1 Pierre 1.22 Ephésiens 4.2 Colossiens 3.12
9 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.Romains 12.17 Romains 12.14 Proverbes 20.22 1 Thessaloniciens 5.15 Matthieu 5.39
10 Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila.Psaumes 34.12-34.16 Jacques 1.26 1 Pierre 2.22 Jean 12.25 Jean 1.47
11 Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.Matthieu 5.9 Psaumes 34.14 Hébreux 12.14 Romains 12.18 1 Timothée 6.18
12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya.Jean 9.31 Proverbes 15.29 Psaumes 34.15-34.16 Proverbes 15.3 Proverbes 15.8
13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema?Proverbes 16.7 Romains 8.28 Psaumes 38.20 Proverbes 15.9 3 Jean 1.11
14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.1 Pierre 2.19-2.20 Esaïe 8.12-8.13 Luc 6.22-6.23 Matthieu 10.28 Marc 10.29
15 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.Colossiens 4.6 2 Timothée 2.25-2.26 Luc 21.14-21.15 1 Pierre 3.2 Hébreux 6.1
16 Nanyi mwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo.1 Pierre 2.12 Hébreux 13.18 1 Pierre 2.15 Matthieu 5.11 1 Pierre 2.19
17 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya.1 Pierre 2.15 1 Pierre 2.20 1 Pierre 3.14 1 Pierre 4.19 Actes 21.14
18 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa,1 Pierre 4.1 Hébreux 9.28 Hébreux 9.26 Tite 2.14 1 Pierre 4.6
19 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri;1 Pierre 4.6 Esaïe 61.1 Esaïe 42.7 Esaïe 49.9 Apocalypse 20.7
20 watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.Genèse 6.3 Hébreux 11.7 Genèse 6.5 2 Pierre 2.5 Genèse 8.18
21 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo.Marc 16.16 Galates 3.27 1 Pierre 1.3 Actes 2.38 1 Corinthiens 12.13
22 Naye yupo mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.Marc 16.19 Hébreux 8.1 Ephésiens 1.20-1.21 Romains 8.38 1 Corinthiens 15.24

Cette Bible est dans le domaine public.