1  Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 
2 Timothée 2.24  1 Timothée 2.4  Tite 3.2  Jacques 5.16  1 Thessaloniciens 3.12  
 2  kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 
Esdras 6.10  Jérémie 29.7  1 Thessaloniciens 4.11  Romains 13.1-13.7  Proverbes 24.21  
 3  Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; 
1 Timothée 1.1  Luc 1.47  1 Timothée 5.4  1 Pierre 2.20  Ephésiens 5.9-5.10  
 4  ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. 
Ezéchiel 18.32  Ezéchiel 18.23  2 Pierre 3.9  Tite 2.11  2 Timothée 2.25  
 5  Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu; 
Galates 3.20  1 Corinthiens 8.6  Esaïe 44.6  Hébreux 7.25  Deutéronome 6.4  
 6  ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. 
Matthieu 20.28  1 Timothée 6.15  1 Corinthiens 1.6  Tite 1.3  Galates 4.4  
 7  Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli. 
2 Timothée 1.11  Actes 9.15  Ephésiens 3.7-3.8  Romains 9.1  Psaumes 111.7  
 8  Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano. 
Psaumes 134.2  Psaumes 63.4  Esaïe 1.15  Jérémie 7.9-7.10  Jean 4.21  
 9  Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani; 
Proverbes 31.22  Esaïe 3.16  Jérémie 2.32  1 Pierre 3.3-3.5  Jérémie 4.30  
 10  bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu. 
Actes 9.36  Proverbes 31.31  Apocalypse 2.19  1 Pierre 3.3-3.5  Ephésiens 2.10  
 11  Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna. 
1 Corinthiens 14.34-14.35  Genèse 3.16  1 Pierre 3.5-3.6  Esther 1.20  Colossiens 3.18  
 12  Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu. 
1 Corinthiens 14.34  
 13  Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. 
Genèse 2.18  1 Corinthiens 11.8-11.9  Genèse 2.22  Genèse 2.7  Genèse 1.27  
 14  Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa. 
Genèse 3.6  2 Corinthiens 11.3  Genèse 3.12-3.13  
 15  Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi. 
Tite 2.12  1 Pierre 4.7  1 Timothée 2.9  1 Timothée 1.5  Genèse 3.15-3.16