Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Actes 6.6
Bible en Swahili de l’est


1 Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung’uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.Actes 4.35 Actes 2.41 Actes 9.41 Actes 2.47 Actes 9.39
2 Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani.Deutéronome 1.9-1.14 Exode 18.17-18.26 Nombres 11.11-11.13 2 Timothée 2.4 Actes 25.27
3 Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;Deutéronome 1.13 Jacques 3.17-3.18 Actes 10.22 1 Corinthiens 16.3 Actes 16.2
4 na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno.Actes 1.14 Philippiens 1.9-1.11 1 Corinthiens 9.16 Ephésiens 1.15-1.17 Actes 20.19-20.31
5 Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia;Actes 11.24 Actes 21.8 Actes 6.3 Actes 6.8 Actes 13.1
6 ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.2 Timothée 1.6 Actes 8.17 1 Timothée 4.14 Actes 1.24 Actes 13.3
7 Neno la Mungu likaenea; na hesabu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemu; jamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani.Actes 19.20 Actes 12.24 Colossiens 1.6 Romains 1.5 Romains 16.26
8 Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.1 Timothée 3.13 Actes 6.5 Actes 8.6 Actes 6.10 Actes 4.29-4.30
9 Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;Actes 22.3 Actes 23.34 Actes 15.23 Actes 15.41 Actes 21.27
10 lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye.Luc 21.15 Job 32.8 Jérémie 15.20 1 Corinthiens 2.4 Luc 1.17
11 Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.Matthieu 26.59-26.60 Actes 25.3 Jean 5.45-5.47 Actes 21.28 Jean 1.17
12 Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.Proverbes 15.18 Actes 5.18 Actes 21.27 Actes 5.27 Actes 18.12
13 Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;Actes 21.28 Actes 6.11 Actes 25.8 Psaumes 35.11 Psaumes 27.12
14 maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa.Daniel 9.26 Actes 15.1 Actes 21.21 Hébreux 10.1-10.18 Esaïe 66.19-66.21
15 Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika.Ecclésiaste 8.1 Exode 34.29-34.35 Matthieu 5.22 Matthieu 13.43 2 Corinthiens 3.18

Cette Bible est dans le domaine public.