Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Marc 2.6
Bible en Swahili de l’est


1 Akaingia Kapernaumu tena, baada ya siku kadha wa kadha, ikasikiwa ya kwamba yumo nyumbani.Matthieu 9.1 Luc 18.35-18.38 Marc 1.45 Jean 4.47 Marc 7.24
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.Marc 1.45 Marc 2.13 Romains 10.8 Actes 11.19 Psaumes 40.9
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.Luc 5.18-5.26 Matthieu 9.1-9.8 Matthieu 4.24
4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.Luc 5.19 Deutéronome 22.8
5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.Matthieu 9.2 Jean 5.14 Jacques 5.15 Matthieu 9.22 Marc 2.9-2.10
6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,Luc 5.21-5.22 Matthieu 16.7-16.8 2 Corinthiens 10.5 Marc 8.17
7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?Esaïe 43.25 Luc 7.49 Psaumes 130.4 Daniel 9.9 Jean 10.36
8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?1 Chroniques 29.17 Luc 5.22 Esaïe 55.7 Matthieu 9.4 Jean 21.17
9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?Matthieu 9.5 Luc 5.22-5.25
10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),Daniel 7.13-7.14 1 Timothée 1.13-1.16 Matthieu 16.13 Actes 5.31 Matthieu 9.6-9.8
11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.Jean 5.8-5.10 Marc 1.41 Jean 6.63
12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.Matthieu 9.8 Matthieu 9.33 Luc 7.16 Jean 9.32 Actes 4.21
13 Akatoka tena, akaenda kando ya bahari, mkutano wote ukamwendea, akawafundisha.Marc 1.45 Marc 2.2 Luc 21.38 Matthieu 9.9 Marc 4.1
14 Hata alipokuwa akipita, akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.Marc 3.18 Luc 5.27-5.32 Actes 1.13 Luc 6.15 Matthieu 4.19-4.22
15 Hata alipokuwa ameketi chakulani nyumbani mwake, watoza ushuru wengi na wenye dhambi waliketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake; kwa maana walikuwa wengi wakimfuata.Luc 15.1 Luc 5.29-5.30 Luc 6.17 Matthieu 9.10-9.11 Matthieu 21.31-21.32
16 Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?Esaïe 65.5 Actes 23.9 Luc 18.11 Luc 19.7 Matthieu 18.17
17 Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.Luc 5.31-5.32 Matthieu 9.12-9.13 Luc 19.10 Luc 15.7 1 Timothée 1.15-1.16
18 Nao wanafunzi wake Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga; basi walikuja, wakamwambia, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi?Matthieu 6.18 Luc 18.12 Matthieu 6.16 Matthieu 9.14-9.17 Romains 10.3
19 Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga.Genèse 29.22 Matthieu 25.1-25.10 Juges 14.10-14.11 Psaumes 45.14 Cantique 6.8
20 Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile.Esaïe 54.5 Luc 17.22 Jean 16.7 Psaumes 45.11 Actes 1.9
21 Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; ikiwa ashona, kile kipya kilichotiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipotatuka huzidi.Matthieu 9.16 Esaïe 57.16 Psaumes 103.13-103.15 1 Corinthiens 10.13
22 Wala hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa atia, ile divai mpya itavipasua viriba vile, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika. Bali hutia divai mpya katika viriba vipya.Luc 5.37-5.38 Matthieu 9.17 Josué 9.4 Josué 9.13 Psaumes 119.83
23 Ikawa alipokuwa akipita mashambani siku ya sabato, wanafunzi wake walianza kuendelea njiani wakivunja masuke.Luc 6.1-6.5 Matthieu 12.1-12.8 Deutéronome 23.24-23.25
24 Mafarisayo wakamwambia, Tazama, mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato?Matthieu 15.2-15.3 Exode 20.10 Matthieu 12.2 Hébreux 12.3 Nombres 15.32-15.36
25 Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa ana haja, na kuona njaa, yeye na wenziwe?1 Samuel 21.3-21.6 Matthieu 21.16 Marc 12.20 Luc 10.26 Matthieu 19.4
26 Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiathari, akaila mikate ile ya Wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe?2 Samuel 8.17 Lévitique 24.5-24.9 1 Samuel 21.1 1 Chroniques 24.6 1 Samuel 23.9
27 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.Colossiens 2.16 Deutéronome 5.14 Exode 23.12 Luc 6.9 Ezéchiel 20.20
28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.Apocalypse 1.10 Ephésiens 1.22 Jean 9.16 Luc 13.15-13.16 Marc 3.4

Cette Bible est dans le domaine public.