Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Lamentations 5.11
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.Psaumes 44.13-44.16 Lamentations 3.61 Job 7.7 Néhémie 1.8 Job 10.9
2 Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya makafiri.Sophonie 1.13 Esaïe 1.7 Psaumes 79.1-79.2 Esaïe 5.17 Esaïe 63.18
3 Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane.Jérémie 18.21 Exode 22.24 Osée 14.3 Jérémie 15.8
4 Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa.Esaïe 3.1 Ezéchiel 4.9-4.17 Deutéronome 28.48
5 Watufuatiao wa juu ya shingo zetu; Tumechoka tusipate raha yo yote.Néhémie 9.36-9.37 Jérémie 27.11-27.12 Jérémie 27.2 Actes 15.10 Jérémie 27.8
6 Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula.Osée 9.3 Osée 12.1 Jérémie 2.18 2 Rois 10.15 Osée 5.13
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.Jérémie 16.12 Ezéchiel 18.2 Jérémie 31.29 Zacharie 1.5 Jérémie 14.20
8 Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.Zacharie 11.6 Néhémie 5.15 Proverbes 30.22 Psaumes 7.2 Osée 2.10
9 Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani.Jérémie 40.9-40.12 Ezéchiel 12.18-12.19 2 Samuel 23.17 Jérémie 41.18 Jérémie 42.14
10 Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuu; Kwa sababu ya hari ya njaa ituteketezayo.Lamentations 4.8 Job 30.30 Lamentations 3.4 Psaumes 119.83
11 Huwatia jeuri wanawake katika Sayuni; Na mabikira katika miji ya Yuda.Zacharie 14.2 Esaïe 13.16 Deutéronome 28.30
12 Wakuu hutungikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima.Lamentations 4.16 Esaïe 47.6 Jérémie 39.6-39.7 Jérémie 52.10-52.11 Jérémie 52.25-52.27
13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni.Juges 16.21 Esaïe 58.6 Néhémie 5.1-5.5 Esaïe 47.2 Exode 2.11
14 Wazee wameacha kwenda langoni; Na vijana kwenda ngomani.Jérémie 7.34 Lamentations 1.19 Esaïe 24.7-24.11 Lamentations 1.4 Ezéchiel 26.13
15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo.Amos 8.10 Psaumes 30.11 Jacques 4.9-4.10 Jérémie 25.10 Amos 6.4-6.7
16 Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.Psaumes 89.39 Jérémie 13.18 Esaïe 3.9-3.11 Lamentations 1.1 Job 19.9
17 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema.Esaïe 1.5 Lamentations 2.11 Psaumes 6.7 Job 17.7 Ezéchiel 21.7
18 Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.Michée 3.12 1 Rois 9.7-9.8 Jérémie 9.11 Jérémie 52.13 Psaumes 74.2-74.3
19 Wewe, Bwana, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi.Psaumes 102.12 Psaumes 45.6 Psaumes 102.25-102.27 Psaumes 9.7 Psaumes 145.13
20 Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi?Psaumes 13.1 Psaumes 44.24 Psaumes 74.1 Psaumes 89.46 Psaumes 77.7-77.10
21 Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.Psaumes 80.3 Jérémie 31.18 Psaumes 80.19 Psaumes 80.7 Ezéchiel 36.37
22 Isipokuwa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.Psaumes 60.1-60.2 Osée 1.6 Psaumes 44.9 Jérémie 15.1-15.5 Esaïe 64.9

Cette Bible est dans le domaine public.