Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 44.16
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini sikia sasa, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na Israeli, niliyekuchagua;Jérémie 30.10 Esaïe 41.8 Jérémie 46.27-46.28 Hébreux 3.7-3.8 Esaïe 42.23
2 Bwana, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua.Jérémie 1.5 Esaïe 43.1 Esaïe 44.24 Esaïe 49.1 Esaïe 43.7
3 Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;Joël 2.28 Actes 2.17 Esaïe 59.21 Jean 7.37-7.39 Apocalypse 21.6
4 nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji.Esaïe 58.11 Psaumes 1.3 Psaumes 137.1-137.2 Job 40.22 Ezéchiel 17.5
5 Mmoja atasema, Mimi ni wa Bwana; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa Bwana, na kujiita kwa jina la Israeli.Zacharie 13.9 2 Corinthiens 8.5 Zacharie 8.20-8.23 Exode 13.9 Néhémie 9.38-10.29
6 Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.Esaïe 41.4 Apocalypse 1.8 Apocalypse 22.13 Esaïe 43.10-43.11 Esaïe 48.12
7 Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze.Esaïe 41.26 Esaïe 41.22 Actes 17.26 Esaïe 46.9-46.10 Deutéronome 32.8
8 Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.Esaïe 43.10 Deutéronome 4.35 1 Samuel 2.2 Deutéronome 4.39 Esaïe 48.5
9 Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike.Esaïe 41.24 Esaïe 41.29 Psaumes 97.7 2 Corinthiens 4.4 Esaïe 43.8
10 Ni nani aliyejichongea mungu mmoja, au aliyesubu sanamu isiyofaa kitu?Jérémie 10.5 Habakuk 2.18 Actes 19.26 1 Corinthiens 8.4 1 Rois 12.28
11 Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja.Esaïe 42.17 Esaïe 45.16 Psaumes 97.7 Esaïe 1.29 Juges 6.29-6.32
12 Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia.Esaïe 40.19 Esaïe 41.6-41.7 Esaïe 46.6-46.7 Habakuk 2.13 Exode 32.8
13 Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani.Juges 17.4-17.5 Psaumes 115.5-115.7 Genèse 31.30 Romains 1.23 Exode 20.4-20.5
14 Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha.Esaïe 40.20 Jérémie 10.3-10.8 Habakuk 2.19 Osée 4.12
15 Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia.2 Chroniques 25.14 Apocalypse 9.20 Esaïe 44.10 Esaïe 45.20 Juges 2.19
16 Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto; 17 na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba, akasema, Uniokoe; maana wewe u mungu wangu.Esaïe 45.20 Esaïe 36.19-36.20 1 Rois 18.26 Daniel 6.16 Daniel 6.27
18 Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu.2 Corinthiens 4.3-4.4 Psaumes 81.12 Esaïe 6.9-6.10 Jérémie 5.21 Jean 12.39-12.40
19 Wala hapana atiaye moyoni, wala hapana maarifa, wala fahamu kusema, Nimeteketeza sehemu motoni, naam, pia nimeoka mkate juu ya makaa yake; nimeoka nyama nikaila; nami, je! Kilichobaki nikifanye kuwa chukizo? Je! Nisujudie shina la mti?Deutéronome 27.15 1 Rois 11.7 2 Rois 23.13 1 Rois 11.5 Esaïe 46.8
20 Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?Job 15.31 Psaumes 102.9 Osée 4.12 Romains 1.25 Osée 12.1
21 Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi.Esaïe 44.1-44.2 Esaïe 43.15 Deutéronome 31.19-31.21 Esaïe 49.15-49.16 Esaïe 46.8-46.9
22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.Esaïe 43.25 1 Corinthiens 6.20 Esaïe 43.1 Esaïe 48.20 Psaumes 51.1
23 Imbeni, enyi mbingu, maana Bwana ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana Bwana amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli.Esaïe 49.13 Psaumes 69.34 Jérémie 51.48 Psaumes 98.7-98.8 Esaïe 49.3
24 Bwana, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami?Esaïe 42.5 Esaïe 43.14 Esaïe 45.12 Esaïe 40.22 Esaïe 44.2
25 Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga;Job 5.12-5.14 2 Samuel 15.31 Psaumes 33.10 Jérémie 50.36 Esaïe 29.14
26 nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka;Zacharie 1.6 Zacharie 12.6 Esaïe 54.11-54.12 Psaumes 147.2 Matthieu 5.18
27 niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako;Esaïe 42.15 Jérémie 50.38 Jérémie 51.36 Esaïe 11.15-11.16 Jérémie 51.32
28 nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.Esaïe 45.13 2 Chroniques 36.22-1.3 Esaïe 45.1 Esaïe 48.14-48.15 Esaïe 46.11

Cette Bible est dans le domaine public.