Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 44
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini sikia sasa, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na Israeli, niliyekuchagua; Jérémie 30.10 Esaïe 41.8 Jérémie 46.27-46.28 Esaïe 48.16-48.18 Genèse 17.7
2 Bwana, aliyekufanya, na kukuumba toka tumboni, yeye atakayekusaidia, asema hivi; Usiogope, Ee Yakobo, mtumishi wangu; na wewe, Yeshuruni, niliyekuchagua. Jérémie 1.5 Esaïe 43.1 Esaïe 44.24 Esaïe 49.1 Esaïe 43.7
3 Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa; Joël 2.28 Actes 2.17 Esaïe 59.21 Jean 7.37-7.39 Apocalypse 21.6
4 nao watatokea katika manyasi, kama mierebi karibu na mifereji ya maji. Psaumes 1.3 Esaïe 58.11 Actes 4.4 Actes 2.41-2.47 Psaumes 137.1-137.2
5 Mmoja atasema, Mimi ni wa Bwana; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa Bwana, na kujiita kwa jina la Israeli. Psaumes 116.16 Michée 4.2 Deutéronome 26.17-26.19 Zacharie 13.9 2 Corinthiens 8.5
6 Bwana, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, Bwana wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu. Esaïe 41.4 Apocalypse 1.8 Esaïe 48.12 Apocalypse 22.13 Esaïe 43.10-43.11
7 Naye ni nani kama mimi atakayeita, na kuyahubiri haya, na kunitengenezea, tangu nilipowaweka watu wa kale? Na mambo yanayokuja na yatakayotokea, wayatangaze. Esaïe 41.26 Esaïe 41.22 Esaïe 48.3-48.8 Esaïe 41.4 Genèse 17.7-17.8
8 Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuhubiri haya zamani na kuyaonyesha? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine. Esaïe 43.10 Deutéronome 4.35 1 Samuel 2.2 Deutéronome 4.39 Deutéronome 32.39
9 Wachongao sanamu, wote ni ubatili; wala mambo yao yawapendezayo hayatafaa kitu; wala mashahidi wao wenyewe hawaoni, wala hawajui; ili watahayarike. Esaïe 41.24 Esaïe 41.29 Psaumes 97.7 Jérémie 14.22 Juges 10.14
10 Ni nani aliyejichongea mungu mmoja, au aliyesubu sanamu isiyofaa kitu? Jérémie 10.5 Habakuk 2.18 Actes 19.26 1 Corinthiens 8.4 1 Rois 12.28
11 Tazama, wenziwe wote watatahayari; na mafundi, hao ni wanadamu; na wakusanyike pamoja, wakasimame; wataogopa na kutahayari pamoja. Esaïe 42.17 Esaïe 45.16 Psaumes 97.7 Esaïe 1.29 1 Rois 18.19-18.29
12 Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia. Esaïe 40.19 Esaïe 41.6-41.7 Esaïe 46.6-46.7 Habakuk 2.13 Exode 32.8
13 Seremala hunyosha uzi; huiandika kwa kalamu ya mate; huitengeneza kwa randa, huiandika kwa bikari, huifanza kwa mfano wa mwanadamu, sawasawa na uzuri wa mwanadamu, ili ikae nyumbani. Juges 17.4-17.5 Psaumes 115.5-115.7 Ezéchiel 8.12 Deutéronome 4.28 Actes 17.29
14 Yeye hujikatia mierezi, hutwaa mtiriza, na mwaloni, hujichagulia mti mmoja katika miti ya msituni; hupanda mvinje, mvua ikausitawisha. Esaïe 40.20 Jérémie 10.3-10.8 Habakuk 2.19 Osée 4.12
15 Kisha utamfaa mwanadamu kwa kuni; hutwaa kipande, akaota moto; naam, huuwasha moto, akaoka mkate; naam, huufanya mungu, akauabudu; huifanya sanamu ya kuchonga, akaisujudia. 2 Chroniques 25.14 Apocalypse 9.20 Esaïe 44.10 Esaïe 45.20 Juges 2.19
16 Sehemu moja huiteketeza; kwa sehemu nyingine hula nyama; huoka chakula kiokwacho, akashiba; naam, huota moto, akasema, Aha, nimeota moto, nimeona moto; 17 na kwa sehemu iliyobakia hufanya mungu, yaani, sanamu yake ya kuchonga; husujudu mbele yake akaiabudu, akaiomba, akasema, Uniokoe; maana wewe u mungu wangu. Esaïe 45.20 Daniel 3.17 Esaïe 36.19-36.20 1 Rois 18.26 Daniel 6.16
18 Hawajui wala hawafikiri; maana amewafumba macho, wasione, na mioyo yao, wasiweze kufahamu. Psaumes 81.12 Esaïe 6.9-6.10 2 Corinthiens 4.3-4.4 Esaïe 29.10 Jérémie 5.21
19 Wala hapana atiaye moyoni, wala hapana maarifa, wala fahamu kusema, Nimeteketeza sehemu motoni, naam, pia nimeoka mkate juu ya makaa yake; nimeoka nyama nikaila; nami, je! Kilichobaki nikifanye kuwa chukizo? Je! Nisujudie shina la mti? Deutéronome 27.15 1 Rois 11.5 1 Rois 11.7 2 Rois 23.13 Esaïe 45.20
20 Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu? Job 15.31 Psaumes 102.9 Osée 4.12 Romains 1.25 Osée 12.1
21 Kumbuka haya, Ee Yakobo; nawe Israeli, maana wewe u mtumishi wangu; nimekuumba; u mtumishi wangu; Ee Israeli, hutasahauliwa na mimi. Esaïe 44.1-44.2 Esaïe 43.15 Esaïe 42.23 Zacharie 10.9 Deutéronome 4.9
22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa. Esaïe 43.25 1 Corinthiens 6.20 Psaumes 51.9 Esaïe 43.1 Esaïe 48.20
23 Imbeni, enyi mbingu, maana Bwana ametenda hayo; Pigeni kelele, enyi mabonde ya nchi; Pazeni nyimbo, enyi milima; Nawe, msitu, na kila mti ndani yake. Maana Bwana amemkomboa Yakobo, Naye atajitukuza katika Israeli. Esaïe 49.13 Psaumes 69.34 Jérémie 51.48 Psaumes 98.7-98.8 Esaïe 49.3
24 Bwana, mkombozi wako, yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja nami? Esaïe 42.5 Esaïe 43.14 Esaïe 45.12 Esaïe 44.2 Esaïe 51.13
25 Nizitanguaye ishara za waongo, na kuwatia waganga wazimu; niwarudishaye nyuma wenye hekima, na kuyageuza maarifa yao kuwa ujinga; Psaumes 33.10 Job 5.12-5.14 2 Samuel 15.31 Jérémie 50.36 Jérémie 51.57
26 nilithibitishaye neno la mtumishi wangu, na kuyafikiliza mashauri ya wajumbe wangu; niuambiaye Yerusalemu, Utakaliwa na watu, nayo miji ya Yuda, Itajengwa, nami nitapainua mahali pake palipobomoka; Zacharie 1.6 2 Pierre 1.19-1.21 Esaïe 54.3 Zacharie 2.4 1 Rois 13.3-13.5
27 niviambiaye vilindi, Kauka, nami nitaikausha mito yako; Jérémie 51.36 Esaïe 42.15 Jérémie 50.38 Esaïe 11.15-11.16 Jérémie 51.32
28 nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa. Esaïe 45.1 Esaïe 45.13 2 Chroniques 36.22-1.3 Daniel 10.1 Esaïe 63.11

Cette Bible est dans le domaine public.