Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 135.22
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Lisifuni jina la Bwana, Enyi watumishi wa Bwana, sifuni.Psaumes 134.1 Psaumes 107.8 Psaumes 113.1-113.3 Néhémie 9.5 Exode 34.5-34.7
2 Ninyi msimamao nyumbani mwa Bwana, Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu.Psaumes 116.19 Psaumes 92.13 Luc 2.37 Psaumes 96.8 1 Chroniques 16.37-16.42
3 Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema, Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.Psaumes 147.1 Psaumes 119.68 Psaumes 107.1 Matthieu 19.17 Psaumes 106.1
4 Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo, Na Israeli, wawe watu wake hasa.Deutéronome 10.15 1 Pierre 2.9 Tite 2.14 Deutéronome 7.6-7.7 Malachie 3.17
5 Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu, Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.Psaumes 95.3 Psaumes 48.1 Psaumes 97.9 Jérémie 10.10-10.11 Daniel 6.26-6.27
6 Bwana amefanya kila lililompendeza, Katika mbingu na katika nchi, Katika bahari na katika vilindi vyote.Psaumes 115.3 Matthieu 8.26-8.27 Matthieu 28.18 Psaumes 33.9 Daniel 4.35
7 Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika hazina zake.Jérémie 10.13 Jérémie 51.16 Zacharie 10.1 Psaumes 148.8 Job 28.25-28.26
8 Aliwapiga wazaliwa wa kwanza wa Misri, Wa wanadamu na wa wanyama.Psaumes 78.51 Exode 12.12 Psaumes 105.36 Exode 12.29-12.30 Exode 13.15
9 Alipeleka ishara na maajabu kati yako, Ee Misri, Juu ya Farao na watumishi wake wote.Psaumes 136.15 Deutéronome 6.22 Jérémie 32.20-32.21 Psaumes 78.43-78.50 Psaumes 105.27-105.29
10 Aliwapiga mataifa mengi, Akawaua wafalme wenye nguvu;Psaumes 136.17-136.22 Nombres 21.24 Psaumes 44.2-44.3
11 Sihoni, mfalme wa Waamori, Na Ogu, mfalme wa Bashani, Na falme zote za Kanaani.Josué 12.7-12.24 Deutéronome 2.30-3.11 Néhémie 9.22 Deutéronome 29.7 Josué 10.1-10.12
12 Akaitoa nchi yao iwe urithi, Urithi wa Israeli watu wake.Psaumes 78.55 Psaumes 136.21-136.22 Josué 11.23 Josué 12.7 Nombres 33.54
13 Ee Bwana, jina lako ni la milele, Bwana, kumbukumbu lako vizazi hata vizazi.Exode 3.15 Psaumes 102.12 Exode 34.5-34.7 Psaumes 102.21 Osée 12.5
14 Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumishi wake.Deutéronome 32.36 Psaumes 50.4 Amos 7.3 Osée 11.8-11.9 Amos 7.6
15 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu.Psaumes 115.4-115.8 Habakuk 2.18-2.19 Esaïe 46.6-46.7 Actes 17.29 Esaïe 37.19
16 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni,Esaïe 6.10 Matthieu 13.14-13.16
17 Zina masikio lakini hazisikii, Wala hamna pumzi vinywani mwake. 18 Wazifanyao watafanana nazo, Na kila mmoja anayezitumainia.Psaumes 97.7 Jérémie 10.8 2 Corinthiens 4.4 Esaïe 44.18-44.20 Psaumes 115.8
19 Enyi mlango wa Israeli, mhimidini Bwana; Enyi mlango wa Haruni, mhimidini Bwana;Psaumes 147.19-147.20 Psaumes 145.10 Psaumes 118.1-118.4 Apocalypse 19.5 Psaumes 115.9-115.11
20 Enyi mlango wa Lawi, mhimidini Bwana; Ninyi mnaomcha Bwana, mhimidini Bwana. 21 Na ahimidiwe Bwana toka Sayuni, Akaaye Yerusalemu. Haleluya.Psaumes 134.3 Psaumes 132.13-132.14 Esaïe 12.6 2 Chroniques 6.6 Psaumes 48.1

Cette Bible est dans le domaine public.