Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 6.23
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu na kusema,Job 4.1
2 Laiti uchungu wangu ungepimwa, Na msiba wangu kutiwa katika mizani pamoja!Job 23.2 Job 31.6 Job 4.5
3 Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.Proverbes 27.3 Psaumes 40.5 Psaumes 77.4 Job 37.19-37.20 Job 23.2
4 Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi i ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.Psaumes 38.2 Job 30.15 Psaumes 88.15-88.16 Job 16.12-16.14 Proverbes 18.14
5 Je! Huyo punda-mwitu hulia akiwa na majani? Au, ng’ombe hulia malishoni?Psaumes 104.14 Joël 1.18-1.20 Jérémie 14.6 Psaumes 42.1
6 Je! Kitu kisicho na ladha yumkini kulika pasipo chumvi? Au je, uto wa yai una tamu iwayo yote?Colossiens 4.6 Lévitique 2.13 Job 6.30 Luc 14.34 Psaumes 119.103
7 Roho yangu inakataa hata kuvigusa; Kwangu mimi ni kama chakula kichukizacho.1 Rois 22.27 Ezéchiel 4.16 1 Rois 17.12 Ezéchiel 4.14 Psaumes 102.9
8 Laiti ningepewa haja yangu, Naye Mungu angenipa neno hilo ninalolitamani sana!Job 6.11-6.13 Job 17.14-17.16 Psaumes 119.81
9 Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniseta; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!1 Rois 19.4 Job 7.15-7.16 Jonas 4.3 Jonas 4.8 Nombres 11.14-11.15
10 Hapo ndipo ningefarijika hata sasa; Naam, ningejikuza katika maumivu yasiyoniacha; Kwa kuwa sikuyakana maneno yake Mtakatifu.Lévitique 19.2 Esaïe 57.15 Job 23.12 Osée 11.9 Romains 8.32
11 Nguvu zangu ni zipi, hata ningoje? Na mwisho wangu ni nini, hata nisubiri?Psaumes 102.23 Psaumes 39.5 Psaumes 103.14-103.16 Job 17.1 Job 13.25
12 Je! Nguvu zangu ni nguvu za mawe? Au mwili wangu, je! Ni shaba?Job 40.18 Job 41.24
13 Je! Si kwamba sina msaada ndani yangu. Tena kwamba kufanikiwa kumeondolewa mbali nami?Job 19.28 Galates 6.4 2 Corinthiens 1.12 Job 12.2-12.3 Job 26.2
14 Kwake huyo atakaye kuzima roho inapasa atendewe mema na rafiki; Hata kwake huyo aachaye kumcha Mwenyezi.Proverbes 17.17 Job 4.3-4.5 Psaumes 36.1-36.3 Romains 12.15 Job 16.5
15 Ndugu zangu wametenda udanganyifu kama kijito cha maji. Mfano wa fumbi la vijito vipitavyo.Jérémie 15.18 Psaumes 38.11 Psaumes 41.9 Jean 16.32 Jean 13.18
16 Vilivyokuwa vyeusi kwa sababu ya barafu, Ambamo theluji hujificha. 17 Wakati vipatapo moto hutoweka; Kukiwako hari, hukoma mahali pao.1 Rois 17.1 Job 24.19
18 Misafara isafiriyo kwa njia yao hugeuka; Hukwea kwenda barani, na kupotea. 19 Misafara ya Tema huvitazama, Majeshi ya Sheba huvingojea.Esaïe 21.14 Genèse 25.15 Jérémie 25.23 1 Rois 10.1 Genèse 25.3
20 Wametahayari kwa sababu walitumaini; Wakaja huku, nao walifadhaika.Jérémie 17.13 Romains 5.5 Jérémie 14.3-14.4 Romains 9.33
21 Kwani sasa ninyi mmekuwa vivyo; Mwaona jambo la kutisha, mkaogopa.Psaumes 38.11 Esaïe 2.22 Job 2.11-2.13 Matthieu 26.31 2 Timothée 4.16
22 Je! Nilisema, Nipeni? Au, Nitoleeni toleo katika mali yenu?Actes 20.33 Job 42.11 1 Samuel 12.3
23 Au, Niokoeni na mkono wa adui? Au, Nikomboeni na mikono ya hao waoneao?Job 5.20 Jérémie 15.21 Psaumes 49.15 Néhémie 5.8 Psaumes 49.7-49.8
24 Nifunzeni, nami nitanyamaa kimya; Mkanijulishe ni jambo gani nililokosa.Jacques 3.2 Psaumes 39.1-39.2 Proverbes 9.9 Psaumes 19.12 Job 10.2
25 Jinsi yafaavyo maneno ya uelekevu! Lakini kuhoji kwenu, je! Kumeonya nini?Proverbes 25.11 Job 24.25 Proverbes 18.21 Job 16.3-16.5 Ecclésiaste 12.10-12.11
26 Je! Mwafikiri kuyakemea maneno? Maana maneno ya huyo aliyekata tamaa ni kama upepo.Job 8.2 Job 34.3-34.9 Job 3.3-3.26 Job 2.10 Job 10.1
27 Naam, mwapenda kuwapigia kura hao mayatima, Na kufanya biashara ya rafiki yenu.Psaumes 7.15 Joël 3.3 2 Pierre 2.3 Job 22.9 Jacques 1.27
28 Sasa basi iweni radhi kuniangalia; Kwani hakika sitanena uongo usoni penu.Job 27.4 Job 36.4 Job 13.4 Job 33.3 Job 11.3
29 Rudini, nawasihi, lisiwe neno la udhalimu; Naam, rudini tena, neno langu ni la haki.Job 17.10 Job 34.5 Job 23.10 Malachie 3.18 Job 27.4-27.6
30 Je! Mna udhalimu ulimini mwangu? Je! Makaakaa yangu hayatambui mambo ya madhara?Job 12.11 Job 42.3-42.6 Job 6.6 Job 33.8-33.12 Job 34.3

Cette Bible est dans le domaine public.