Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Nombres 15.39
Bible en Swahili de l’est


Règles relatives aux sacrifices

1 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
2 Nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtakapoingia nchi yenu ya kukaa, niwapayo,
Lévitique 23.10 Nombres 15.18 Deutéronome 12.1 Deutéronome 7.1-7.2 Deutéronome 12.9
3 nanyi mwataka kumsongezea Bwana sadaka kwa moto, kwamba ni sadaka ya kuteketezwa, au dhabihu ya kuchinjwa, ili kuondoa nadhiri, au kuwa sadaka ya hiari, au katika sikukuu zenu zilizoamriwa, ili kumfanyia Bwana harufu ipendezayo, katika ng’ombe, au katika kondoo;
Exode 29.18 Genèse 8.21 Nombres 28.27 Philippiens 4.18 Lévitique 27.2
4 ndipo yeye atakayetoa matoleo yake na amtolee Bwana sadaka ya unga ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta;
Exode 29.40 Lévitique 23.13 Lévitique 2.1 Lévitique 6.14 Lévitique 14.10
5 na divai kwa sadaka ya kinywaji, robo ya hini, utaiandaa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa ajili ya kila mwana-kondoo.
Nombres 28.7 Nombres 28.14 Psaumes 116.13 2 Timothée 4.6 Matthieu 26.28-26.29
6 Au kwa ajili ya kondoo mume, utaiandaa sadaka ya unga ya sehemu za kumi mbili za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta;
Nombres 28.12-28.14 Nombres 15.4
7 na kwa sadaka ya kinywaji utasongeza sehemu ya tatu ya hini ya divai, kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana.
8 Tena hapo utakapomwandaa ng’ombe mume kwa sadaka ya kuteketezwa, au kwa dhabihu ya kuchinjwa, kwa kuondoa nadhiri, au kwa sadaka za amani kwa Bwana;
Lévitique 3.1 Lévitique 7.11-7.18 Lévitique 1.3
9 ndipo utakapotoa, pamoja na huyo ng’ombe, sadaka ya unga ya sehemu za kumi tatu za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na nusu ya hini ya mafuta.
Nombres 28.14 Nombres 28.12 Lévitique 14.10 Lévitique 6.14 Lévitique 7.37
10 Tena utasongeza nusu ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji, kwa sadaka iliyosongezwa kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.
Nombres 6.15 Nombres 15.5
11 Ndivyo itakavyofanywa kwa kila ng’ombe, au kwa kila kondoo mume, au kwa kila mwana-kondoo mume, au kila mwana-mbuzi.
12 Kama hesabu ilivyo ya hao mtakaowaandaa, ndivyo mtakavyofanya kwa kila mmoja, sawasawa na hesabu yao.
13 Wote ambao wamezaliwa kwenu watafanya hayo yote kwa kuandama mfano huo, katika kusongeza sadaka kwa moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.
14 Tena kwamba mgeni amekaa kwenu, au mtu ye yote aliye kati yenu katika vizazi vyenu, naye yuataka kusongeza sadaka kwa moto, na harufu ya kupendeza kwa Bwana; kama ninyi mfanyavyo, na yeye atafanya vivyo.
15 Katika huo mkutano, kutakuwa na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye pamoja nanyi; ni amri ya milele katika vizazi vyenu; kama ninyi mlivyo, na mgeni atakuwa vivyo mbele za Bwana.
Nombres 15.29 Nombres 9.14 Exode 12.49 Ephésiens 2.11-2.22 Colossiens 3.11
16 Itakuwa sheria moja na amri moja kwenu ninyi na kwa mgeni akaaye nanyi.
17 Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
18 Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapoingia nchi niwapelekayo,
Nombres 15.2 Deutéronome 26.1-26.15
19 ndipo itakapokuwa ya kwamba hapo mtakapokula katika chakula cha nchi hiyo, mtamsongezea Bwana sadaka ya kuinuliwa.
Josué 5.11-5.12
20 Katika unga wenu wa kwanza wa chenga-chenga mtasongeza mkate uwe sadaka ya kuinuliwa; vile vile kama mfanyavyo sadaka ya kuinuliwa ya sakafu ya kupuria nafaka, ndivyo mtakavyoiinua.
Lévitique 2.14 Néhémie 10.37 Exode 23.19 Exode 34.26 Ezéchiel 44.30
21 Malimbuko ya unga wenu mtampa Bwana sadaka ya kuinuliwa, katika vizazi vyenu.
Nombres 18.26 Exode 29.28
22 Tena mtakapokosa, msiyashike maagizo hayo yote Bwana aliyomwambia Musa,
Lévitique 4.2 Psaumes 19.12 Lévitique 4.27 Lévitique 5.15-5.17 Lévitique 5.13
23 hayo yote Bwana aliyowaagiza kwa mkono wa Musa, tangu siku hiyo Bwana aliyoleta maagizo, na baadaye katika vizazi vyenu
24 ndipo itakapokuwa, kama ni kosa lililofanywa pasipo kujua, wala mkutano haukuwa na fahamu, ndipo mkutano wote utasongeza ng’ombe mume mmoja mdogo kuwa sadaka ya kuteketezwa, kuwa harufu ya kupendeza kwa Bwana, pamoja na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya kinywaji, kama amri ilivyo, na mbuzi mume mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
Lévitique 4.23 Nombres 28.15 Lévitique 4.13-4.21 Lévitique 5.15 Nombres 15.8-15.10
25 Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mkutano wote wa wana wa Israeli, nao watasamehewa; maana, lilikuwa ni kosa, nao wamekwisha leta matoleo yao, sadaka iliyosongezwa kwa Bwana kwa moto, na sadaka yao ya dhambi pia wameileta mbele za Bwana kwa ajili ya kosa lao;
Lévitique 4.20 Romains 3.25 Lévitique 4.26 Hébreux 2.17 Luc 23.34
26 nao mkutano wote wa wana wa Israeli watasamehewa, na mgeni akaaye kati yao; maana, katika habari za hao wote jambo hilo lilitendeka pasipo kujua.
Nombres 15.24
27 Tena kama mtu mmoja akifanya dhambi pasipo kujua, ndipo atasongeza mbuzi mmoja mke wa mwaka wa kwanza kuwa sadaka ya dhambi.
Lévitique 4.27-4.28 1 Timothée 1.13 Actes 3.17 Actes 17.30
28 Naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mtu akosaye, atakapofanya dhambi pasipo kujua, mbele za Bwana, ili kufanya upatanisho kwa ajili yake; naye atasemehewa.
Lévitique 4.35
29 Mtakuwa na sheria moja kwa huyo afanyaye neno lo lote pasipo kujua, kwa huyo aliyezaliwa kwenu kati ya wana wa Israeli, na kwa mgeni akaaye kati yao.
Nombres 15.15 Lévitique 16.29 Romains 3.29-3.30 Lévitique 17.15 Nombres 9.14
30 Lakini mtu afanyaye neno lo lote kwa kusudi, kama ni mzalia, kama ni mgeni, huyo amtukana Bwana; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.
Psaumes 19.13 Deutéronome 1.43 Hébreux 10.26 Lévitique 20.3 Esaïe 37.23-37.24
31 Kwa sababu amelidharau neno la Bwana, na kuyavunja maagizo yake; mtu huyo atakatiliwa mbali, uovu wake utakuwa juu yake.
Proverbes 13.13 2 Samuel 12.9 Ezéchiel 18.20 Lévitique 5.1 Psaumes 119.126

Un viol du sabbat

32 Kisha wakati huo wana wa Israeli walipokuwako jangwani, wakamwona mtu mmoja akikusanya kuni siku ya Sabato.
Exode 35.2-35.3 Exode 20.8-20.10 Exode 31.14-31.15 Exode 16.27-16.28 Exode 16.23
33 Hao waliomwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote.
Jean 8.3-8.20
34 Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa.
Lévitique 24.12 Nombres 9.8
35 Bwana akamwambia Musa, Mtu huyo lazima atauawa; mkutano wote watampiga kwa mawe huko nje ya marago.
Exode 31.14-31.15 Actes 7.58 Lévitique 24.23 1 Rois 21.13 Lévitique 20.2
36 Basi mkutano wote wakampeleka nje ya marago, nao wakampiga kwa mawe, akafa; kama Bwana alivyomwagiza Musa.
Josué 7.25

La frange au bord des vêtements

37 Kisha Bwana akasema na Musa, na kumwambia,
38 Nena na wana wa Israeli, na kuwaagiza ya kwamba wajifanyie vishada katika ncha za nguo zao, katika vizazi vyao, tena ya kwamba watie katika kila kishada cha kila ncha nyuzi za rangi ya samawi;
Matthieu 23.5 Deutéronome 22.12 Matthieu 9.20 Luc 8.44
39 nacho kitakuwa kwenu ni kishada, ili mpate kukiangalia, na kuyakumbuka maagizo yote ya Bwana, na kuyafanya; tena kwamba msiende kutanga-tanga kuandama mioyo yenu wenyewe, na macho yenu wenyewe, ambayo mlikuwa mkiyaandama kwa uasherati hapo kwanza;
Psaumes 73.27 Ezéchiel 6.9 Job 31.7 Ecclésiaste 11.9 Psaumes 106.39
40 ili mpate kukumbuka na kuyafanya maagizo yangu yote, na kuwa watakatifu kwa Mungu wenu.
Romains 12.1 1 Thessaloniciens 4.7 Lévitique 11.44-11.45 Ephésiens 1.4 Lévitique 19.2
41 Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, niliyewaleta kutoka nchi ya Misri, ili kwamba niwe Mungu wenu; mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.
Lévitique 22.33 Ezéchiel 36.25-36.27 Jérémie 31.31-31.33 Psaumes 105.45 Hébreux 11.16

Cette Bible est dans le domaine public.