Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 132
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika. Psaumes 120.1 Psaumes 121.1 Psaumes 25.6-25.7 Psaumes 127.1 Genèse 8.1
2 Ndiye aliyemwapia Bwana, Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo. Genèse 49.24 Psaumes 56.12 Psaumes 116.14-116.18 Esaïe 60.16 Psaumes 66.13-66.14
3 Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu; Ecclésiaste 9.10 Matthieu 6.33 Aggée 1.4
4 Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia; Proverbes 6.4 Ruth 3.18 Genèse 24.33
5 Hata nitakapompatia Bwana mahali, Na Shujaa wa Yakobo maskani. Ephésiens 2.22 1 Chroniques 22.7 2 Chroniques 2.6 2 Samuel 6.17 Esaïe 66.1
6 Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika konde la Yearimu tuliiona. 1 Samuel 17.12 1 Samuel 7.1 Genèse 35.19 1 Chroniques 13.5-13.6 Michée 5.2
7 Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake. Psaumes 99.5 Psaumes 5.7 Psaumes 66.13-66.14 Lamentations 2.1 Psaumes 118.19
8 Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako. 2 Chroniques 6.41-6.42 Psaumes 78.61 Psaumes 68.1 Nombres 10.35-10.36
9 Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie. Job 29.14 Esaïe 61.10 Psaumes 132.16 Zacharie 9.9 Psaumes 68.3
10 Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi Psaumes 84.9 1 Rois 15.4-15.5 1 Rois 11.12-11.13 2 Chroniques 6.42 Osée 3.5
11 Bwana amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi. 2 Samuel 7.12 Actes 2.30 Psaumes 110.4 Psaumes 89.3-89.4 2 Chroniques 6.16
12 Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele. Psaumes 115.14 Psaumes 102.28 Luc 1.32-1.33 Esaïe 9.7 Psaumes 89.30-89.35
13 Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake. Psaumes 68.16 Hébreux 12.22 Psaumes 48.1-48.3 Psaumes 87.2 Esaïe 14.32
14 Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani. Esaïe 66.1 Psaumes 132.8 Joël 3.21 Esaïe 57.15 Psaumes 68.16
15 Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula. Psaumes 147.14 Psaumes 37.3 Matthieu 6.32-6.33 Deutéronome 14.29 Marc 8.6-8.9
16 Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia. 2 Chroniques 6.41 Psaumes 132.9 Psaumes 140.4 Galates 3.27 Jean 16.24
17 Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu. 2 Chroniques 21.7 1 Rois 11.36 Ezéchiel 29.21 Luc 1.69 1 Rois 15.4
18 Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi. Job 8.22 Psaumes 109.29 Psaumes 35.26 Psaumes 21.8-21.9 Matthieu 28.18

Cette Bible est dans le domaine public.