Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 132.14
Bible en Swahili de l’est


1 Bwana, umkumbukie Daudi Taabu zake zote alizotaabika.Psaumes 120.1 Psaumes 121.1 Lamentations 5.1 Psaumes 131.1 Psaumes 128.1
2 Ndiye aliyemwapia Bwana, Akaweka nadhiri kwa Shujaa wa Yakobo.Genèse 49.24 Psaumes 66.13-66.14 2 Samuel 7.1 Psaumes 46.11 Psaumes 119.106
3 Sitaingia hemani mwa nyumba yangu, Wala sitapanda matandiko ya kitanda changu;Ecclésiaste 9.10 Matthieu 6.33 Aggée 1.4
4 Sitaacha macho yangu kuwa na usingizi, Wala kope zangu kusinzia;Proverbes 6.4 Ruth 3.18 Genèse 24.33
5 Hata nitakapompatia Bwana mahali, Na Shujaa wa Yakobo maskani.1 Chroniques 22.7 Ephésiens 2.22 Esaïe 66.1 1 Chroniques 15.12 1 Chroniques 15.3
6 Tazama, tulisikia habari zake katika Efrata, Katika konde la Yearimu tuliiona.1 Samuel 17.12 1 Samuel 7.1 Michée 5.2 Ruth 1.2 Genèse 35.19
7 Na tuingie katika maskani yake, Tusujudu penye kiti cha kuwekea miguu yake.Psaumes 99.5 Psaumes 5.7 Lamentations 2.1 Psaumes 118.19 Psaumes 99.9
8 Ee Bwana, uinuke, uende kwenye raha yako, Wewe na sanduku la nguvu zako.2 Chroniques 6.41-6.42 Psaumes 68.1 Nombres 10.35-10.36 Psaumes 78.61
9 Makuhani wako na wavikwe haki, Watauwa wako na washangilie.Job 29.14 Esaïe 61.10 Psaumes 132.16 Psaumes 149.5 Psaumes 93.1
10 Kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako, Usiurudishe nyuma uso wa masihi2 Chroniques 6.42 Osée 3.5 2 Rois 19.34 1 Rois 11.34 Psaumes 89.38-89.39
11 Bwana amemwapia Daudi neno la kweli, Hatarudi nyuma akalihalifu, Baadhi ya wazao wa mwili wako Nitawaweka katika kiti chako cha enzi.2 Samuel 7.12 Psaumes 110.4 Psaumes 89.3-89.4 2 Chroniques 6.16 Actes 2.30
12 Wanao wakiyashika maagano yangu, Na shuhuda nitakazowafundisha; Watoto wao nao wataketi Katika kiti chako cha enzi milele.Esaïe 9.7 Psaumes 89.30-89.35 Esaïe 59.21 Actes 2.30 Psaumes 115.14
13 Kwa kuwa Bwana ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake.Psaumes 68.16 Esaïe 14.32 Psaumes 76.1-76.2 Psaumes 78.68-78.69 Hébreux 12.22
14 Hapo ndipo mahali pangu pa raha milele, Hapo nitakaa kwa maana nimepatamani.Psaumes 132.8 Esaïe 66.1 Psaumes 68.16 1 Rois 8.27 Sophonie 3.17
15 Hakika nitavibariki vyakula vyake Wahitaji wake nitawashibisha chakula.Psaumes 147.14 Psaumes 107.9 Psaumes 37.19 Luc 1.53 Esaïe 33.16
16 Na makuhani wake nitawavika wokovu, Na watauwa wake watashangilia.2 Chroniques 6.41 Psaumes 132.9 Jean 16.24 Zacharie 9.15-9.17 Zacharie 9.9
17 Hapo nitamchipushia Daudi pembe, Na taa nimemtengenezea masihi wangu.Ezéchiel 29.21 Luc 1.69 2 Chroniques 21.7 1 Rois 11.36 1 Rois 15.4
18 Adui zake nitawavika aibu, Bali juu yake taji yake itasitawi.Job 8.22 Psaumes 109.29 Psaumes 35.26 Psaumes 21.8-21.9 Apocalypse 17.14

Cette Bible est dans le domaine public.