Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Galates 5.10
Bible en Swahili de l’est


1 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.2 Corinthiens 3.17 Galates 5.13 Jean 8.32-8.36 Galates 2.4 Romains 8.2
2 Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.Galates 5.6 Romains 9.31-9.32 Galates 5.3-5.4 Actes 15.1 Galates 2.3-2.5
3 Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.Galates 3.10 Ephésiens 4.17 Jacques 2.10-2.11 Romains 2.25 Deutéronome 27.26
4 Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema.2 Pierre 2.20-2.22 Galates 2.21 Romains 11.6 Romains 9.31-9.32 Galates 5.2
5 Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani.Psaumes 25.5 1 Thessaloniciens 1.10 Romains 8.23-8.25 Genèse 49.18 Philippiens 3.9
6 Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.Jacques 2.14-2.26 1 Jean 3.14-3.20 Matthieu 25.31-25.40 1 Thessaloniciens 1.3 1 Corinthiens 7.19
7 Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli?1 Corinthiens 9.24 Galates 3.1 1 Pierre 1.22 Romains 6.17 Hébreux 12.1
8 Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi.Galates 1.6 Romains 8.28
9 Chachu kidogo huchachua donge zima.1 Corinthiens 15.33 Marc 8.15 Luc 12.1 Luc 13.21 1 Corinthiens 5.6-5.7
10 Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote.Galates 5.12 2 Corinthiens 2.3 Galates 1.7 Galates 4.17 1 Timothée 1.20
11 Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika!1 Corinthiens 1.23 Galates 4.29 Galates 6.12 Actes 23.13-23.14 1 Corinthiens 1.18
12 Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!Galates 5.10 Josué 7.12 Exode 12.15 Josué 7.25 Galates 2.4
13 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.1 Corinthiens 9.19 1 Pierre 2.16 1 Corinthiens 8.9 Galates 5.14 Romains 15.1-15.2
14 Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.Matthieu 7.12 Lévitique 19.18 Matthieu 22.39-22.40 Romains 13.8-13.10 Galates 6.2
15 Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.1 Corinthiens 3.3 Galates 5.26 Jacques 3.14-4.3 Philippiens 3.2 2 Corinthiens 11.20
16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.Galates 5.24-5.25 Galates 5.19-5.21 Ephésiens 2.3 2 Corinthiens 7.1 Colossiens 3.5-3.10
17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.Romains 8.5-8.8 Romains 8.13 Jean 3.6 Romains 7.7-7.8 Psaumes 51.10-51.12
18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.Romains 8.14 Romains 6.14-6.15 Proverbes 8.20 Ezéchiel 36.27 Galates 5.16
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,1 Corinthiens 6.9-6.10 1 Pierre 4.2-4.4 Matthieu 15.18-15.19 Colossiens 3.5-3.8 Apocalypse 21.8
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,Actes 16.16-16.19 1 Samuel 15.23 Deutéronome 18.10 1 Corinthiens 11.19 Actes 8.9-8.11
21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.Romains 13.13 1 Corinthiens 6.9-6.10 Romains 8.13 Colossiens 3.6 1 Corinthiens 5.11
22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,Colossiens 3.12-3.17 1 Corinthiens 13.4-13.7 Jean 15.5 Ephésiens 5.9 Jean 15.2
23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.1 Timothée 1.9 Actes 24.25 Tite 1.8 Tite 2.2 1 Corinthiens 9.25
24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.Romains 6.6 Romains 8.13 Romains 13.14 Galates 6.14 1 Pierre 2.11
25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.Galates 5.16 Jean 6.63 Romains 8.4-8.5 1 Pierre 4.6 1 Corinthiens 15.45
26 Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.Jacques 3.14-3.16 Philippiens 2.1-2.3 Galates 5.15 1 Pierre 5.5 1 Corinthiens 3.7

Cette Bible est dans le domaine public.