1  Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami. 
2 Corinthiens 11.4  2 Corinthiens 11.19  2 Corinthiens 5.13  2 Corinthiens 11.16-11.17  2 Corinthiens 11.21  
 2  Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi. 
Osée 2.19-2.20  Esaïe 54.5  Ephésiens 5.26-5.27  Jean 3.29  Esaïe 62.4-62.5  
 3  Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. 
Apocalypse 12.9  1 Timothée 2.14  Colossiens 2.4  Galates 1.6  Colossiens 2.8  
 4  Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! 
Galates 1.6-1.8  1 Corinthiens 3.11  Actes 4.12  Galates 3.2  1 Corinthiens 12.4-12.11  
 5  Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu. 
2 Corinthiens 12.11-12.12  Galates 2.6-2.9  1 Corinthiens 15.10  
 6  Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu. 
Ephésiens 3.4  1 Corinthiens 1.17  2 Corinthiens 4.2  2 Corinthiens 12.12  2 Corinthiens 5.11  
 7  Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira? 
2 Corinthiens 12.13  1 Corinthiens 9.6  Actes 20.34  Actes 18.1-18.3  1 Corinthiens 9.14-9.18  
 8  Naliwanyang’anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi. 
2 Corinthiens 11.9  Philippiens 4.14-4.16  Philippiens 4.18  
 9  Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda. 
1 Thessaloniciens 2.6  2 Corinthiens 12.13-12.16  2 Thessaloniciens 3.8-3.9  Philippiens 4.10-4.16  1 Thessaloniciens 2.9  
 10  Kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya. 
Romains 9.1  Actes 18.12  Romains 1.9  2 Corinthiens 1.23  1 Thessaloniciens 2.10  
 11  Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua. 
2 Corinthiens 12.15  2 Corinthiens 6.11-6.12  2 Corinthiens 7.3  Jean 21.17  Psaumes 44.21  
 12  Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi. 
1 Corinthiens 9.12  1 Corinthiens 5.6  2 Corinthiens 11.18  Job 23.13  2 Corinthiens 1.17  
 13  Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 
Apocalypse 2.2  Galates 1.7  Philippiens 3.2  Galates 2.4  2 Corinthiens 11.15  
 14  Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 
Galates 1.8  2 Corinthiens 11.3  Apocalypse 12.9  2 Corinthiens 2.11  Matthieu 4.1-4.10  
 15  Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. 
Philippiens 3.19  Jude 1.4  2 Corinthiens 3.9  Jérémie 23.14-23.15  Jérémie 29.32  
 16  Nasema tena, mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; ili mimi nami nipate kujisifu ngaa kidogo. 
2 Corinthiens 11.1  2 Corinthiens 12.6  2 Corinthiens 11.21-11.23  2 Corinthiens 11.19  2 Corinthiens 12.11  
 17  Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu. 
1 Corinthiens 7.12  2 Corinthiens 9.4  1 Corinthiens 7.25  2 Corinthiens 11.18-11.27  Philippiens 3.3-3.6  
 18  Kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu. 
1 Pierre 1.24  2 Corinthiens 12.5-12.6  2 Corinthiens 11.12  2 Corinthiens 11.21-11.23  1 Corinthiens 4.10  
 19  Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha. 
1 Corinthiens 4.10  1 Corinthiens 8.1  1 Corinthiens 10.15  Apocalypse 3.17  
 20  Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni. 
Galates 2.4  Galates 4.3  Galates 4.9  Galates 5.1  2 Corinthiens 1.24  
 21  Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri. 
2 Corinthiens 10.10  2 Corinthiens 11.17  2 Corinthiens 10.1-10.2  2 Corinthiens 11.22-11.27  Philippiens 3.3-3.6  
 22  Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. 
Philippiens 3.5  Romains 11.1  Romains 9.4  Genèse 17.8-17.9  Exode 9.1  
 23  Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. 
2 Corinthiens 6.4-6.5  1 Corinthiens 15.10  Actes 9.16  2 Corinthiens 3.6  1 Corinthiens 3.5  
 24  Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. 
Deutéronome 25.2-25.3  Marc 13.9  Matthieu 10.17  
 25  Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; 
Actes 14.19  Actes 16.22-16.23  Actes 16.37  Actes 7.58-7.59  Actes 22.24  
 26  katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang’anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; 
Actes 14.5  Actes 20.19  Actes 17.5  Actes 13.50  Actes 25.3  
 27  katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. 
2 Corinthiens 6.5  Philippiens 4.12  2 Thessaloniciens 3.8  1 Thessaloniciens 2.9  1 Corinthiens 4.11-4.12  
 28  Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote. 
Romains 16.4  Actes 18.23  Romains 15.16  1 Corinthiens 7.17  Actes 15.36  
 29  Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe? 
1 Corinthiens 8.13  1 Corinthiens 9.22  2 Corinthiens 2.4-2.5  Néhémie 13.23-13.25  Néhémie 13.15-13.20  
 30  Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu. 
1 Corinthiens 2.3  2 Corinthiens 12.5-12.11  2 Corinthiens 11.16-11.18  Jérémie 9.23-9.24  2 Corinthiens 12.1  
 31  Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo. 
Romains 9.5  Romains 1.25  Jean 10.30  Ephésiens 1.3  1 Thessaloniciens 2.5  
 32  Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata; 
Actes 9.24-9.25  2 Corinthiens 11.26  
 33  nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake. 
Actes 9.25  1 Samuel 19.12  Josué 2.18