Scandale des procès entre chrétiens
 1  Je! Mtu wa kwenu akiwa ana daawa juu ya mwenzake athubutu kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? 
Actes 18.14-18.15  Actes 19.38  1 Corinthiens 16.1  Matthieu 18.15-18.17  1 Corinthiens 14.33  
 2  Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 
Matthieu 19.28  Luc 22.30  Apocalypse 20.4  Apocalypse 2.26-2.27  Daniel 7.22  
 3  Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? 
Luc 8.14  Matthieu 25.41  Jude 1.6  Luc 21.34  1 Corinthiens 6.4  
 4  Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa? 
1 Corinthiens 5.12  Actes 6.2-6.4  
 5  Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake? 
1 Corinthiens 4.14  1 Corinthiens 15.34  Jacques 3.13-3.18  Proverbes 14.8  1 Corinthiens 3.18  
 6  Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini. 
2 Corinthiens 6.14  1 Jean 2.9-2.11  1 Jean 3.11-3.15  Actes 7.26  Genèse 45.24  
 7  Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu? 
Proverbes 20.22  1 Pierre 3.9  Jacques 4.1-4.3  Romains 12.17-12.19  1 Pierre 2.19-2.23  
 8  Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu. 
1 Thessaloniciens 4.6  Marc 10.19  Colossiens 3.25  Malachie 3.5  Michée 2.2  
 9  Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 
Galates 5.19-5.21  1 Timothée 1.9-1.10  Lévitique 20.13  Ephésiens 5.4-5.5  Lévitique 18.22  
 10  wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. 
1 Corinthiens 5.11  Galates 5.21  Ezéchiel 22.27  Matthieu 23.33  Ezéchiel 22.29  
 11  Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu. 
1 Corinthiens 1.2  Actes 22.16  Ephésiens 5.26  Hébreux 10.22  1 Corinthiens 12.2  
Liberté chrétienne et appartenance à Christ
 12  Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote. 
1 Corinthiens 10.23-10.33  1 Corinthiens 9.27  Romains 14.14-14.23  1 Corinthiens 8.7-8.13  Hébreux 12.15-12.16  
 13  Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. 
1 Corinthiens 6.15  1 Corinthiens 6.19  Matthieu 15.17  Ephésiens 5.23  1 Corinthiens 3.16  
 14  Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. 
Actes 2.24  Ephésiens 1.19-1.20  Jean 6.39-6.40  Actes 17.31  Jean 11.25-11.26  
 15  Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha! 
Romains 12.5  Ephésiens 5.30  1 Corinthiens 12.27  Luc 20.16  Ephésiens 4.15-4.16  
 16  Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 
Genèse 2.24  Ephésiens 5.31  Marc 10.8  Matthieu 19.5-19.6  Hébreux 11.31  
 17  Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 
Jean 17.21-17.23  1 Corinthiens 12.13  Jean 3.6  Ephésiens 4.3-4.4  Galates 2.20  
 18  Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 
Hébreux 13.4  Colossiens 3.5  1 Thessaloniciens 4.3  Romains 6.12-6.13  1 Pierre 2.11  
 19  Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 
1 Corinthiens 3.16  2 Corinthiens 6.16  1 Pierre 2.5  Ephésiens 2.21-2.22  Jean 2.21  
 20  maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu. 
1 Corinthiens 7.23  Romains 12.1  1 Pierre 1.18  1 Pierre 2.9  Actes 20.28