Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Marc 10.15
Bible en Swahili de l’est


1 Akaondoka huko akafika mipakani mwa Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani; makutano mengi wakakutanika tena wakamwendea; akawafundisha tena kama alivyozoea.Jean 10.40 Jean 11.7 Marc 6.34 Matthieu 19.1-19.12 Jean 18.20
2 Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.Luc 11.53-11.54 Matthieu 23.13 Jean 8.6 Matthieu 9.34 Jean 11.47
3 Naye akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?Esaïe 8.20 Luc 10.25 Jean 5.39 Galates 4.21
4 Wakasema, Musa alitoa ruhusa kuandika hati ya talaka na kumwacha.Deutéronome 24.1-24.4 Matthieu 5.31-5.32 Matthieu 19.7 Matthieu 1.19 Jérémie 3.1
5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.Matthieu 19.8 Néhémie 9.16-9.17 Actes 7.51 Hébreux 3.7-3.10 Deutéronome 31.27
6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.Genèse 1.27 Genèse 5.2 2 Pierre 3.4 Genèse 2.20-2.23 Genèse 1.1
7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;Genèse 2.24 Ephésiens 5.31 Matthieu 19.5-19.6
8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.1 Corinthiens 6.16 Ephésiens 5.28 Genèse 2.24
9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.Romains 7.1-7.3
10 Hata nyumbani tena wanafunzi wakamwuliza habari ya neno hilo.Marc 9.28 Marc 4.10 Marc 9.33
11 Akawaambia, Kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake;Luc 16.18 1 Corinthiens 7.10-7.11 Romains 7.3 Matthieu 19.9 1 Corinthiens 7.4
12 na mke, akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine, azini.1 Corinthiens 7.11 1 Corinthiens 7.13
13 Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.Matthieu 19.13-19.15 Luc 18.15-18.17 Marc 10.48 Exode 10.9-10.11 Marc 9.38
14 Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao.1 Pierre 2.2 Matthieu 18.4 Matthieu 19.14 Matthieu 18.10 2 Timothée 3.15
15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.Matthieu 18.3 Luc 18.17 Jean 3.3-3.6
16 Akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabarikia.Marc 9.36 Luc 2.28-2.34 Deutéronome 28.3 Luc 24.50-24.51 Esaïe 40.11
17 Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele?Luc 18.18-18.30 Marc 1.40 Matthieu 19.16-19.30 Luc 10.25 1 Jean 2.25
18 Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? Hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.Luc 18.19 1 Samuel 2.2 Matthieu 19.17 Romains 3.12 Psaumes 86.5
19 Wazijua amri, Usiue, Usizini, Usiibe, Usishuhudie uongo, Usidanganye, Waheshimu baba yako na mama yako.Romains 13.9 Exode 20.12-20.17 Luc 18.20 Galates 4.21 Marc 12.28-12.34
20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.Matthieu 19.20 Philippiens 3.6 Ezéchiel 33.31-33.32 Luc 10.29 2 Timothée 3.5
21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.Actes 2.45 Luc 12.33 Luc 16.9 Matthieu 6.19-6.21 1 Timothée 6.17-6.19
22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.1 Timothée 6.9-6.10 1 Jean 2.15-2.16 Luc 12.15 Job 21.7-21.15 2 Timothée 4.10
23 Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!Luc 18.24 Marc 3.5 1 Corinthiens 1.26 Jean 3.5 Marc 10.15
24 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu!1 Timothée 6.17 Jean 21.5 Psaumes 52.7 Jean 13.33 Proverbes 11.28
25 Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.Matthieu 19.24-19.25 Luc 18.25 Jérémie 13.23 Matthieu 23.24 Matthieu 7.3-7.5
26 Nao wakashangaa mno, wakimwambia, Ni nani, basi, awezaye kuokoka?Luc 13.23 Marc 7.37 Actes 16.31 2 Corinthiens 11.23 Romains 10.9-10.13
27 Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu.Matthieu 19.26 Luc 1.37 Jérémie 32.17 Luc 18.27 Job 42.2
28 Petro akaanza kumwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe.Luc 18.28-18.30 Luc 14.33 Marc 1.16-1.20 Matthieu 4.20 Matthieu 4.22
29 Yesu akasema, Amin, nawaambieni, Hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,Marc 8.35 Apocalypse 2.3 Genèse 12.1-12.3 1 Corinthiens 9.23 Hébreux 11.24-11.26
30 ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.Jean 16.22-16.23 Luc 18.30 Philippiens 3.8 2 Corinthiens 6.10 Apocalypse 3.18
31 Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho; na wa mwisho watakuwa wa kwanza.Matthieu 19.30 Matthieu 20.16 Luc 13.30 Romains 9.30-9.33 Actes 13.46-13.48
32 Nao walikuwako njiani, huku wakipanda kwenda Yerusalemu; na Yesu alikuwa akiwatangulia, wakashangaa, nao katika kufuata wakaogopa. Akawatwaa tena wale Thenashara, akaanza kuwaambia habari za mambo yatakayompata,Matthieu 20.17-20.19 Luc 9.51 Matthieu 13.11 Luc 18.31-18.34 Zacharie 3.8
33 akisema, Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemu; na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa wakuu wa makuhani na waandishi, nao watamhukumu afe, watamtia mikononi mwa Mataifa,Matthieu 27.2 Actes 3.13-3.14 Matthieu 16.21 Matthieu 26.66 Marc 8.31
34 nao watamdhihaki, na kumtemea mate, na kumpiga mijeledi, na kumwua; na baada ya siku tatu atafufuka.Marc 14.65 Matthieu 16.21 Matthieu 26.67 Marc 15.29-15.31 1 Corinthiens 15.4
35 Na Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wakamwendea, wakamwambia, Mwalimu, twataka utufanyie lo lote tutakalokuomba.Matthieu 20.20-20.28 2 Samuel 14.4-14.11 1 Rois 2.16 Marc 1.19-1.20 Marc 14.33
36 Akawaambia, Mwataka niwafanyie nini?Marc 10.51 1 Rois 3.5-3.15 Jean 15.7
37 Wakamwambia, Utujalie sisi tuketi, mmoja mkono wako wa kuume, na mmoja mkono wako wa kushoto, katika utukufu wako.Matthieu 19.28 Matthieu 25.31 1 Rois 22.19 Luc 24.26 1 Pierre 1.11
38 Yesu akawaambia, Hamjui mnaloliomba. Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi?Luc 12.50 Esaïe 51.22 Luc 22.42 Marc 14.36 Jean 18.11
39 Wakamwambia, Twaweza. Yesu akawaambia, Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa;Apocalypse 1.9 Actes 12.2 Marc 14.36 Marc 14.31 Matthieu 10.25
40 lakini habari ya kuketi mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto si langu kuwapa, ila wao watapewa waliowekewa tayari.Matthieu 25.34 Matthieu 20.23 Jean 17.2 Hébreux 11.16 Jean 17.24
41 Hata wale kumi waliposikia wakaanza kuwakasirikia Yakobo na Yohana.Philippiens 2.3 Proverbes 13.10 Romains 12.10 Luc 22.24 Jacques 4.5
42 Yesu akawaita, akawaambia, Mwajua ya kuwa wale wanaohesabiwa kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha.1 Pierre 5.3 Luc 22.25 Matthieu 20.25
43 Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu anayetaka kuwa mkubwa kwenu, atakuwa mtumishi wenu,Matthieu 23.8-23.12 1 Corinthiens 9.19-9.23 Marc 9.35 Luc 18.14 Matthieu 20.26-20.27
44 na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote. 45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.Matthieu 20.28 Philippiens 2.5-2.8 Jean 13.14 Tite 2.14 Esaïe 53.10-53.12
46 Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia.Matthieu 20.29-20.34 Jean 9.8 Luc 18.35-19.1 Actes 3.2-3.3 Luc 16.22
47 Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.Matthieu 9.27 Luc 18.36-18.37 Marc 1.24 Matthieu 1.1 Esaïe 11.1
48 Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu.Matthieu 19.13 Psaumes 62.12 Luc 18.39 Marc 7.26-7.29 Luc 18.1-18.8
49 Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.Jean 11.28 Psaumes 86.15 Luc 18.40 Psaumes 145.8 Hébreux 2.17
50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu.Philippiens 3.7-3.9 Hébreux 12.1
51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona.Marc 10.36 Jean 20.16 Matthieu 23.7 Philippiens 4.6 Matthieu 7.7
52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.Matthieu 9.22 Marc 5.34 Marc 8.25 Luc 7.50 Matthieu 9.28-9.30

Cette Bible est dans le domaine public.