1  Mizani ya hadaa ni chukizo kwa Bwana; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. 
Proverbes 16.11  Proverbes 20.23  Proverbes 20.10  Deutéronome 25.13-25.16  Lévitique 19.35-19.36  
 2  Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. 
Luc 18.14  Proverbes 16.18-16.19  Luc 14.8-14.11  Proverbes 15.33  Proverbes 29.23  
 3  Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. 
Proverbes 13.6  Esaïe 1.28  Ecclésiaste 7.17  Jean 7.17  Proverbes 19.3  
 4  Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. 
Genèse 7.1  Sophonie 1.18  Proverbes 10.2  Ezéchiel 7.19  1 Timothée 4.8  
 5  Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. 
Proverbes 5.22  2 Samuel 17.23  Proverbes 11.3  Esther 7.3-7.10  Proverbes 1.31-1.32  
 6  Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. 
Ecclésiaste 10.8  Proverbes 5.22  1 Rois 2.44  Psaumes 7.15-7.16  1 Samuel 12.3-12.4  
 7  Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake lapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. 
Proverbes 10.28  Job 8.13-8.14  Job 11.20  Psaumes 146.4  Proverbes 14.32  
 8  Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. 
Proverbes 21.18  Daniel 6.23-6.24  Esther 7.9-7.10  Esaïe 43.3-43.4  
 9  Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. 
Psaumes 55.12  Proverbes 2.10-2.16  1 Rois 22.20-22.23  1 Rois 13.18-13.22  2 Corinthiens 11.13-11.15  
 10  Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu waangamiapo, watu hupiga kelele. 
Proverbes 28.12  Esther 8.15-8.16  Psaumes 58.10-58.11  Proverbes 28.28  Juges 5.31  
 11  Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu. 
Proverbes 29.8  Proverbes 14.34  Genèse 45.8  Jacques 3.6  Esther 9.1-9.16  
 12  Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. 
Proverbes 14.21  Luc 16.14  Proverbes 10.19  Juges 9.38  Juges 9.27-9.29  
 13  Mwenye kitango akisingizia hufunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo. 
Proverbes 20.19  Lévitique 19.16  Josué 2.14  1 Timothée 5.13  Jérémie 38.27  
 14  Pasipo mashauri taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu. 
Proverbes 15.22  Proverbes 24.6  Proverbes 20.18  Esaïe 19.11-19.14  Actes 15.6-15.21  
 15  Amdhaminiye mgeni hakosi ataumia; Achukiaye mambo ya dhamana yu salama. 
Proverbes 17.18  Proverbes 22.26-22.27  Proverbes 20.16  Proverbes 6.1-6.5  
 16  Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; Na watu wakali hushika mali siku zote. 
1 Samuel 25.32-25.33  Proverbes 31.30-31.31  Romains 16.2-16.4  Luc 21.2-21.4  Actes 16.14-16.15  
 17  Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake. 
Matthieu 5.7  Matthieu 25.34-25.40  2 Corinthiens 9.6-9.14  Esaïe 57.1  Proverbes 15.27  
 18  Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika. 
Osée 10.12-10.13  Jacques 3.18  Ecclésiaste 10.8  Galates 6.8-6.9  Job 27.13-27.23  
 19  Haki huelekea uzima; Afuataye maovu hufuata mauti yake mwenyewe. 
Proverbes 10.16  Proverbes 19.23  Proverbes 12.28  Proverbes 1.16-1.19  1 Jean 3.10  
 20  Wenye kuhalifu moyoni ni chukizo kwa Bwana; Walio wakamilifu katika njia zao humpendeza. 
1 Chroniques 29.17  Psaumes 119.1  Psaumes 51.6  Proverbes 8.13  Proverbes 12.22  
 21  Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka. 
Proverbes 16.5  Actes 2.39  Jérémie 32.39  Psaumes 112.1-112.2  Psaumes 37.26  
 22  Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili. 
Proverbes 31.30  Proverbes 7.10  1 Pierre 3.3-3.4  Genèse 24.47  Proverbes 9.13  
 23  Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. 
Romains 2.8-2.9  Proverbes 10.28  Psaumes 119.5  Psaumes 119.10  Psaumes 10.17  
 24  Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. 
Proverbes 19.17  Luc 6.38  2 Corinthiens 9.5-9.11  Psaumes 112.9  Proverbes 11.18  
 25  Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. 
2 Corinthiens 9.6-9.9  Matthieu 5.7  Esaïe 32.8  Proverbes 28.27  Esaïe 58.7-58.11  
 26  Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. 
Job 29.13  Proverbes 24.24  Amos 8.4-8.6  Genèse 42.6  
 27  Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. 
Psaumes 7.15-7.16  Esther 7.10  Psaumes 57.6  Psaumes 9.15-9.16  Proverbes 17.11  
 28  Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. 
Jérémie 17.8  Psaumes 1.3  1 Timothée 6.17  Psaumes 49.6  Job 31.24-31.25  
 29  Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. 
Ecclésiaste 5.16  Proverbes 14.19  Proverbes 15.27  Josué 7.24-7.25  1 Samuel 25.38  
 30  Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. 
Daniel 12.3  Jacques 5.20  Proverbes 3.18  1 Corinthiens 9.19-9.23  1 Thessaloniciens 2.19  
 31  Tazama, mwenye haki atalipwa duniani; Basi mwovu na mkosaji si mara nyingi zaidi? 
Jérémie 25.29  2 Samuel 12.9-12.12  1 Pierre 4.17-4.18  2 Samuel 7.14-7.15  1 Rois 13.24