1  Moyo wangu umefurika kwa neno jema, Mimi nasema niliyomfanyizia mfalme; Ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi mstadi. 
2 Samuel 23.2  Job 33.3  Cantique 1.12  Esdras 7.6  Psaumes 49.3  
 2  Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu; Neema imemiminiwa midomoni mwako, Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele. 
Luc 4.22  Psaumes 21.6  Hébreux 1.3-1.4  Zacharie 9.17  Hébreux 7.26  
 3  Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako. 
Apocalypse 1.16  Hébreux 4.12  Psaumes 21.5  Psaumes 96.6  Apocalypse 19.15  
 4  Katika fahari yako usitawi uendelee Kwa ajili ya kweli na upole na haki Na mkono wako wa kuume Utakufundisha mambo ya kutisha. 
Psaumes 110.2-110.3  Psaumes 65.5  Apocalypse 6.2  Psaumes 21.8-21.9  Matthieu 12.19-12.20  
 5  Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako; Imo mioyoni mwa adui za mfalme. 
Nombres 24.8  Psaumes 22.27  Psaumes 21.12  Psaumes 38.2  Psaumes 66.3-66.4  
 6  Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. 
Psaumes 93.2  Psaumes 145.13  Apocalypse 19.11  Esaïe 9.6-9.7  Hébreux 1.8-1.9  
 7  Umeipenda haki; Umeichukia dhuluma. Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta, Mafuta ya furaha kuliko wenzako. 
Psaumes 33.5  Hébreux 1.9  Psaumes 21.6  Colossiens 1.18-1.19  Luc 4.18-4.21  
 8  Mavazi yako yote hunukia manemane Na udi na mdalasini. Katika majumba ya pembe Vinubi vimekufurahisha. 
Cantique 1.3  2 Corinthiens 2.14-2.16  Jean 19.39  Cantique 4.6  Matthieu 2.11  
 9  Binti za wafalme wamo Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki. Mkono wako wa kuume amesimama malkia Amevaa dhahabu ya Ofiri. 
1 Rois 2.19  Esaïe 60.10-60.11  Cantique 6.8-6.9  Apocalypse 21.9  1 Rois 10.11  
 10  Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. 
Cantique 2.10-2.13  2 Corinthiens 6.17-7.1  2 Corinthiens 5.16  Deutéronome 21.13  Genèse 12.1  
 11  Naye mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie. 
Esaïe 54.5  Psaumes 95.6  Cantique 1.12-1.16  Esaïe 62.4-62.5  Jean 20.28  
 12  Na binti Tiro analeta kipawa chake, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako. 
Psaumes 22.29  Psaumes 72.10  Esaïe 49.23  Matthieu 2.11  Esaïe 60.10-60.11  
 13  Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu, Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu. 
Apocalypse 19.7-19.8  Esaïe 61.10  Romains 3.22  2 Corinthiens 5.17  Luc 11.40  
 14  Atapelekwa kwa mfalme Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake wanaomfuata, Watapelekwa kwako. 
Juges 5.30  2 Corinthiens 11.2  Cantique 6.8  Apocalypse 14.1-14.4  Cantique 5.8-5.9  
 15  Watapelekwa kwa furaha na shangwe, Na kuingia katika nyumba ya mfalme. 
Apocalypse 7.15-7.17  Esaïe 60.19-60.20  Jude 1.24  Esaïe 35.10  Apocalypse 3.12  
 16  Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako, Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote. 
Apocalypse 5.10  Apocalypse 1.6  1 Pierre 2.9  Apocalypse 20.6  Philippiens 3.7-3.8  
 17  Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu Katika vizazi vyote. Kwa hiyo mataifa watakushukuru Milele na milele. 
Malachie 1.11  Esaïe 61.9  1 Corinthiens 11.26  Esaïe 62.3  Psaumes 72.17-72.19