Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 21
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, mfalme atazifurahia nguvu zako, Na wokovu wako ataufanyia shangwe nyingi sana. Psaumes 28.7 Psaumes 2.6 Psaumes 71.17-72.2 Psaumes 59.16-59.17 Psaumes 20.5-20.6
2 Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake. Psaumes 20.4-20.5 Psaumes 37.4 Psaumes 92.11 Hébreux 7.25 Psaumes 2.8-2.9
3 Maana umemsogezea baraka za heri, Umemvika taji ya dhahabu safi kichwani pake. 2 Samuel 12.30 1 Chroniques 20.2 1 Samuel 16.13 Psaumes 18.18 Apocalypse 19.12
4 Alikuomba uhai, ukampa, Muda mrefu wa siku nyingi, milele na milele. Psaumes 91.16 Psaumes 61.5-61.6 Psaumes 133.3 Psaumes 13.3 Psaumes 119.77
5 Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako, Heshima na adhama waweka juu yake. 1 Pierre 3.22 Jean 17.22 Jean 17.5 Psaumes 8.5 Psaumes 110.1
6 Maana umemfanya kuwa baraka za milele, Wamfurahisha kwa furaha ya uso wako. Psaumes 16.11 Psaumes 45.7 Galates 3.9 Genèse 12.2 Psaumes 72.17-72.19
7 Kwa kuwa mfalme humtumaini Bwana, Na kwa fadhili zake Aliye juu hataondoshwa. Psaumes 16.8 Psaumes 18.2 Psaumes 61.4 Hébreux 2.13 Daniel 7.14
8 Mkono wako utawapata adui zako wote, Mkono wako wa kuume utawapata wanaokuchukia. Esaïe 10.10 1 Samuel 25.29 Amos 9.2-9.3 1 Corinthiens 15.25 Psaumes 110.1-110.2
9 Utawafanya kuwa kama tanuru ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. Bwana atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawala. Malachie 4.1 Lamentations 2.2 Psaumes 2.5 Esaïe 26.11 Psaumes 18.8
10 Matunda yao utayaharibu na kuyaondoa katika nchi, Na wazao wao katika wanadamu. Psaumes 37.28 1 Rois 13.34 Esaïe 14.20 Psaumes 109.13 Job 18.16-18.19
11 Madhali walinuia kukutenda mabaya, Waliwaza hila wasipate kuitimiza. Psaumes 10.2 Psaumes 2.1 Matthieu 27.63-27.64 Jérémie 11.18-11.19 Matthieu 2.8
12 Kwa maana utawafanya kukupa kisogo, Kwa upote wa uta wako ukiwaelekezea mishale. Psaumes 7.12-7.13 Psaumes 18.40 Lamentations 3.12 Psaumes 56.9 Psaumes 9.3
13 Ee Bwana, utukuzwe kwa nguvu zako, Nasi tutaimba na kuuhimidi uweza wako. Apocalypse 19.1-19.6 Matthieu 6.10 Apocalypse 16.5-16.7 Psaumes 46.10 Matthieu 6.13

Cette Bible est dans le domaine public.