Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 16.4
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema, 2 Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo; Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.Job 13.4-13.5 Job 11.2-11.3 Job 19.2-19.3 Jacques 1.19 Psaumes 69.26
3 Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho? Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?Job 6.26 Job 15.2 Job 8.2 Tite 1.11 Tite 2.8
4 Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi; Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu, Ningeweza kutunga maneno juu yenu, Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.Psaumes 22.7 Psaumes 109.25 Lamentations 2.15 2 Rois 19.21 Jérémie 18.16
5 Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu, Na utuzo wa midomo yangu ungetuliza.Job 6.14 Proverbes 27.9 Psaumes 27.14 Proverbes 27.17 Job 4.3-4.4
6 Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi; Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?Job 10.1 Psaumes 88.15-88.18 Psaumes 77.1-77.9
7 Lakini sasa amenichokesha; Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.Job 7.3 Job 1.15-1.19 Michée 6.13 Psaumes 6.6-6.7 Proverbes 3.11-3.12
8 Umenishika sana, ni ushahidi juu yangu; Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.Job 10.17 Job 19.20 Ruth 1.21 Psaumes 109.24 Esaïe 10.16
9 Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesaga-saga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali.Lamentations 2.16 Psaumes 35.16 Job 13.24 Actes 7.54 Job 18.4
10 Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hujikutanisha pamoja juu yangu.Psaumes 22.13 Psaumes 35.15 Actes 23.2 Michée 5.1 Lamentations 3.30
11 Mungu amenitia kwa hao wapotovu, Na kunitupa mikononi mwao waovu.Psaumes 31.8 Psaumes 27.12 Job 1.13-1.19 Job 2.7 2 Corinthiens 12.7
12 Nilikuwa katika raha, naye akanivunja-vunja; Naam, amenishika shingo, na kuniponda; Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.Job 7.20 Lamentations 3.4 Lamentations 3.11-3.12 Job 29.3 Ezéchiel 29.7
13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote, Hunipasua viuno vyangu, asinihurumie; Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.Job 6.4 Job 20.25 Lamentations 2.11 2 Pierre 2.5 Romains 8.32
14 Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu; Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.Juges 15.8 Joël 2.7 Job 9.17 Psaumes 42.7 Lamentations 3.3-3.5
15 Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na pembe yangu nimeidhili uvumbini.Genèse 37.34 Psaumes 7.5 Esaïe 22.12 Psaumes 75.5 1 Rois 21.27
16 Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi, Na giza tupu li katika kope zangu;Psaumes 31.9 Marc 14.34 Job 17.7 Esaïe 52.14 Psaumes 116.3
17 Ijapokuwa hapana jeuri mikononi mwangu, Na kuomba kwangu ni safi.Job 8.5-8.6 Job 15.20 Job 11.14 Job 22.5-22.9 Job 31.1-31.40
18 Ee nchi, usiifunike damu yangu, Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.Ezéchiel 24.7 Esaïe 26.21 Genèse 4.11 Psaumes 66.18-66.19 Esaïe 58.9-58.10
19 Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni. Na huyo atakayenidhamini yuko juu.Romains 1.9 Genèse 31.50 1 Samuel 12.5 1 Thessaloniciens 2.5 2 Corinthiens 11.31
20 Rafiki zangu hunidharau; Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;Luc 6.11-6.12 Job 16.4 Job 12.4-12.5 Hébreux 5.7 Psaumes 142.2
21 Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu, Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.Job 31.35 Job 9.34-9.35 Job 13.3 Esaïe 45.9 Job 13.22
22 Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.Job 14.10 Job 14.14 Ecclésiaste 12.5 Job 7.9-7.10 Job 14.5

Cette Bible est dans le domaine public.