Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Corinthiens 13.1
Bible en Swahili de l’est


1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.1 Pierre 4.8 1 Timothée 1.5 Galates 5.6 Galates 5.22 2 Pierre 2.18
2 Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.1 Corinthiens 13.3 Matthieu 17.20 Matthieu 21.21 1 Corinthiens 16.22 1 Jean 4.8
3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.Jacques 2.14-2.17 Hébreux 13.9 Jean 13.37 Philippiens 1.15-1.18 Jean 6.63
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;1 Pierre 4.8 Proverbes 10.12 Colossiens 3.12 1 Thessaloniciens 5.14 1 Jean 4.11
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;1 Corinthiens 10.24 Philippiens 2.21 1 Jean 3.16-3.17 Jacques 1.19 Esaïe 3.5
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;2 Jean 1.4 Proverbes 14.9 2 Thessaloniciens 2.12 Romains 1.32 Jérémie 13.17
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.1 Pierre 4.8 2 Timothée 2.24 1 Corinthiens 13.4 2 Timothée 2.3-2.10 1 Corinthiens 9.12
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.Hébreux 8.13 Actes 19.6 1 Corinthiens 13.13 Actes 2.4 1 Corinthiens 12.28-12.30
9 Kwa maana tunafahamu kwa sehemu; na tunafanya unabii kwa sehemu;1 Corinthiens 8.2 1 Corinthiens 13.12 Ephésiens 3.8 1 Jean 3.2 Romains 11.34
10 lakini ijapo ile iliyo kamili, iliyo kwa sehemu itabatilika.Apocalypse 22.4-22.5 Apocalypse 21.22-21.23 2 Corinthiens 5.7-5.8 Esaïe 60.19-60.20 1 Corinthiens 13.12
11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.1 Corinthiens 14.20 1 Corinthiens 3.1-3.2 Galates 4.1 Ecclésiaste 11.10
12 Maana wakati wa sasa tunaona kwa kioo kwa jinsi ya fumbo; wakati ule tutaona uso kwa uso; wakati wa sasa nafahamu kwa sehemu; wakati ule nitajua sana kama mimi nami ninavyojuliwa sana.1 Jean 3.2 2 Corinthiens 3.18 Jacques 1.23 Philippiens 3.12 1 Corinthiens 13.9-13.10
13 Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.1 Corinthiens 16.14 1 Corinthiens 13.1-13.8 1 Jean 4.7-4.18 Colossiens 3.14 Galates 5.6

Cette Bible est dans le domaine public.