Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

1 Thessaloniciens 5.15
Bible en Swahili de l’est


1 Lakini, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira, hamna haja niwaandikie.Actes 1.7 1 Thessaloniciens 4.9 Matthieu 24.36 Jude 1.3 Marc 13.30-13.32
2 Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.2 Pierre 3.10 Apocalypse 16.15 Apocalypse 3.3 Matthieu 24.42-24.44 Luc 12.39-12.40
3 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.Luc 21.34-21.35 Hébreux 2.3 Luc 17.26-17.30 2 Thessaloniciens 1.9 Hébreux 12.23
4 Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.1 Jean 2.8 Jérémie 42.16 Deutéronome 28.45 Colossiens 1.13 1 Pierre 2.9-2.10
5 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.Ephésiens 5.8 Luc 16.8 Actes 26.18 Jean 12.36
6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi.1 Pierre 1.13 Luc 22.46 Romains 13.11-13.14 Matthieu 24.42 Apocalypse 16.15
7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku.2 Pierre 2.13 Actes 2.15 Proverbes 23.29-23.35 1 Corinthiens 15.34 Romains 13.13
8 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu.1 Pierre 1.13 Ephésiens 6.11 1 Thessaloniciens 5.5 Ephésiens 6.13-6.18 Hébreux 6.19
9 Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;1 Thessaloniciens 1.10 2 Thessaloniciens 2.13-2.14 2 Timothée 2.10 Matthieu 26.24 2 Pierre 1.1
10 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, kwamba twakesha au kwamba twalala.2 Corinthiens 5.15 Romains 14.8-14.9 1 Thessaloniciens 4.17 2 Corinthiens 5.21 Ephésiens 5.2
11 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, vile vile kama mnavyofanya.Ephésiens 4.29 Hébreux 10.25 Hébreux 3.13 Romains 14.19 Romains 15.2
12 Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni;Hébreux 13.17 1 Corinthiens 16.16 Hébreux 13.7 1 Corinthiens 15.10 1 Corinthiens 16.18
13 mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.Marc 9.50 Jean 13.34-13.35 Jean 15.17 Hébreux 12.14 Jacques 3.18
14 Ndugu, twawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote.2 Timothée 4.2 2 Thessaloniciens 3.6-3.7 Romains 14.1 Hébreux 12.12 Actes 20.35
15 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.1 Pierre 3.9 Galates 6.10 1 Pierre 2.22-2.23 Tite 3.2 1 Corinthiens 6.7
16 Furahini siku zote;Philippiens 4.4 Romains 12.12 Matthieu 5.12 2 Corinthiens 6.10 Luc 10.20
17 ombeni bila kukoma;Romains 12.12 Colossiens 4.2 Luc 18.1 Ephésiens 6.18 Luc 21.36
18 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.Ephésiens 5.20 Philippiens 4.6 Colossiens 3.17 Hébreux 13.15 1 Pierre 2.15
19 Msimzimishe Roho;Ephésiens 4.30 Actes 7.51 Esaïe 63.10 2 Timothée 1.6 Psaumes 51.11
20 msitweze unabii;1 Corinthiens 14.3-14.6 1 Corinthiens 14.1 1 Corinthiens 11.4 1 Corinthiens 14.29-14.32 1 Corinthiens 14.37-14.39
21 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;1 Jean 4.1 Romains 12.2 1 Corinthiens 2.14-2.15 Romains 12.9 Actes 17.11
22 jitengeni na ubaya wa kila namna.Philippiens 4.8 1 Corinthiens 10.31-10.33 Romains 12.17 1 Corinthiens 8.13 2 Corinthiens 6.3
23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.Hébreux 4.12 1 Thessaloniciens 3.13 Jude 1.24 Romains 15.33 1 Pierre 5.10
24 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.2 Thessaloniciens 3.3 1 Corinthiens 1.9 Nombres 23.19 Esaïe 25.1 1 Pierre 5.10
25 Ndugu, tuombeeni.Colossiens 4.3 Romains 15.30 Philippiens 1.19 Philémon 1.22 Ephésiens 6.18-6.20
26 Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.Romains 16.16 1 Corinthiens 16.20
27 Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu.Colossiens 4.16 Actes 19.13 Marc 5.7 1 Timothée 5.21 Hébreux 3.1
28 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.Romains 16.20 2 Thessaloniciens 3.18 Romains 16.23 Romains 1.7

Cette Bible est dans le domaine public.