Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

2 Corinthiens 7
Bible en Swahili de l’est


1 Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. Proverbes 8.13 1 Thessaloniciens 4.7 1 Pierre 2.11 2 Pierre 1.4-1.8 Hébreux 12.28
2 Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu. Actes 20.33 2 Corinthiens 6.3-6.7 Nombres 16.15 2 Corinthiens 1.12 1 Thessaloniciens 2.3-2.6
3 Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja. 2 Corinthiens 6.11-6.12 2 Corinthiens 11.11 2 Corinthiens 12.15 2 Corinthiens 3.2 2 Corinthiens 7.12
4 Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi. 2 Corinthiens 3.12 2 Corinthiens 1.4 Colossiens 1.24 Philippiens 2.17 2 Corinthiens 2.14
5 Kwa maana hata tulipokuwa tumefika Makedonia miili yetu haikupata nafuu; bali tulidhikika kote kote; nje palikuwa na vita, ndani hofu. Deutéronome 32.25 2 Corinthiens 2.13 Jérémie 6.25 2 Corinthiens 2.3 Genèse 8.9
6 Lakini Mungu, mwenye kuwafariji wanyonge, alitufariji kwa kuja kwake Tito. 2 Corinthiens 1.3-1.4 2 Corinthiens 7.13 1 Thessaloniciens 3.6-3.7 Esaïe 61.1-61.2 Esaïe 51.12
7 Wala si kwa kuja kwake tu, bali kwa zile faraja nazo alizofarijiwa kwenu, akituarifu habari ya shauku yenu, na maombolezo yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu, hata nikazidi kufurahi. 2 Jean 1.4 Jérémie 31.18-31.20 Juges 2.4-2.5 Jacques 5.17 Psaumes 38.18
8 Kwa sababu, ijapokuwa naliwahuzunisha kwa waraka ule, sijuti; hata ikiwa nalijuta, naona ya kwamba waraka ule uliwahuzunisha, ingawa ni kwa kitambo tu. Jean 21.17 Hébreux 12.9-12.11 Exode 5.22-5.23 Jean 16.6 Jérémie 20.7-20.9
9 Sasa nafurahi, si kwa sababu ya ninyi kuhuzunishwa, bali kwa sababu mlihuzunishwa, hata mkatubu. Maana mlihuzunishwa kwa jinsi ya Mungu, ili msipate hasara kwa tendo letu katika neno lo lote. 2 Corinthiens 13.8-13.10 Actes 20.21 Luc 15.10 Esaïe 6.9-6.11 Ecclésiaste 7.3
10 Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti. Actes 11.18 2 Samuel 12.13 1 Rois 8.47-8.50 Actes 3.19 2 Timothée 2.25-2.26
11 Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko kwa jinsi ya Mungu kulitenda bidii kama nini ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na hofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi! Kwa kila njia mmejionyesha wenyewe kuwa safi katika jambo hilo. 2 Corinthiens 7.7 Hébreux 12.15-12.16 1 Pierre 2.2 Ephésiens 4.26 Marc 9.43-9.48
12 Basi, ijapokuwa naliwaandikia, sikuandika kwa ajili yake yeye aliyedhulumu, wala si kwa ajili yake yeye aliyedhulumiwa, bali bidii yenu kwa ajili yetu ipate kudhihirishwa kwenu mbele za Mungu. 2 Corinthiens 2.9 1 Corinthiens 5.1-5.2 1 Timothée 3.5 2 Corinthiens 11.11 2 Corinthiens 11.28
13 Kwa hiyo tulifarijiwa. Tena katika kufarijiwa kwetu tulifurahi sana kupita kiasi kwa sababu ya furaha ya Tito; maana roho yake imeburudishwa na ninyi nyote. 2 Corinthiens 7.6 Romains 15.32 Romains 12.15 2 Timothée 1.16 2 Corinthiens 7.15
14 Kwa maana, ikiwa nimejisifu mbele yake katika neno lo lote kwa ajili yenu, sikutahayarishwa; bali, kama tulivyowaambia mambo yote kwa kweli, vivyo hivyo na kujisifu kwetu kwa Tito kulikuwa kweli. 2 Corinthiens 8.24 2 Corinthiens 7.4 2 Corinthiens 9.2-9.4 2 Thessaloniciens 1.4 2 Corinthiens 10.8
15 Na mapenzi yake kwenu yamekuwa mengi kupita kiasi, akumbukapo kutii kwenu ninyi nyote, jinsi mlivyomkaribisha kwa hofu na kutetemeka. Philippiens 2.12 2 Corinthiens 2.9 Esaïe 66.2 2 Corinthiens 6.12 1 Jean 3.17
16 Nafurahi, kwa sababu katika kila neno nina moyo mkuu kwa ajili yenu. 2 Corinthiens 2.3 Philémon 1.8 Philémon 1.21 2 Thessaloniciens 3.4

Cette Bible est dans le domaine public.