Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Esaïe 25.10
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.Exode 15.2 Psaumes 40.5 Nombres 23.19 Psaumes 98.1 Psaumes 118.28
2 Kwa sababu umefanya mji kuwa ni chungu; Mji wenye boma kuwa ni magofu; Jumba la wageni kuwa si mji; Hautajengwa tena milele.Esaïe 17.1 Esaïe 13.22 Esaïe 25.12 Apocalypse 18.19 Esaïe 17.3
3 Kwa hiyo watu walio hodari watakutukuza, Mji wa mataifa watishao utakuogopa.Zacharie 14.9 Esaïe 49.23-49.26 Esaïe 13.11 Ezéchiel 38.23 Ezéchiel 39.21-39.22
4 Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Kivuli wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao, Kama dhoruba ipigayo ukuta.Matthieu 7.25-7.27 Esaïe 32.2 Sophonie 3.12 Jacques 2.5 Psaumes 107.41
5 Kama vile hari katika mahali pakavu Utaushusha mshindo wa wageni; Kama ilivyo hari kwa kivuli cha wingu, Wimbo wa hao watishao utashushwa.Apocalypse 16.1-16.19 Esaïe 49.10 Psaumes 74.3-74.23 Esaïe 64.1-64.2 Esaïe 10.8-10.15
6 Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana.Psaumes 63.5 Esaïe 2.2-2.3 Zacharie 9.16-9.17 Matthieu 8.11 Jérémie 31.12-31.13
7 Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote.Ephésiens 4.18 Actes 17.30 Hébreux 10.19-10.21 Ephésiens 3.5-3.6 Hébreux 9.24
8 Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo.Apocalypse 21.4 1 Corinthiens 15.54 Osée 13.14 Apocalypse 7.17 Esaïe 35.10
9 Katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.Psaumes 20.5 Genèse 49.18 Psaumes 27.14 Apocalypse 1.7 2 Pierre 3.12
10 Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa.Jérémie 48.2 Sophonie 2.9 Esaïe 25.6 Esaïe 10.31 Zacharie 9.9-9.11
11 Naye atanyosha mikono yake katikati yake, kama vile aogeleaye anyoshavyo mikono yake ili aogelee, naye atashusha kiburi chake, pamoja na hila za mikono yake.Esaïe 14.26 Esaïe 5.25 Esaïe 16.6 Esaïe 16.14 Esaïe 2.11
12 Na boma la ngome ya kuta zako ameliinamisha, na kulilaza chini, na kulitupa chini hata mavumbini.Esaïe 26.5 Esaïe 15.1 Esaïe 14.23 2 Corinthiens 10.4-10.5 Apocalypse 18.21

Cette Bible est dans le domaine public.