Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 56.8
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita.Psaumes 27.2 Psaumes 69.13-69.16 Psaumes 57.1-57.3 Psaumes 16.1 1 Corinthiens 15.54
2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.Michée 6.6 Psaumes 92.8 Apocalypse 16.14 Psaumes 91.1 Psaumes 35.1
3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;Psaumes 55.4-55.5 Psaumes 34.4 1 Samuel 30.6 1 Samuel 21.12 2 Corinthiens 7.5-7.6
4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?Psaumes 118.6 Hébreux 13.6 Psaumes 119.160 Psaumes 27.1 Psaumes 56.10-56.11
5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.2 Pierre 3.16 Jean 2.19 1 Samuel 18.21 Jérémie 18.18 Psaumes 41.7
6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.Psaumes 71.10 Psaumes 59.3 Psaumes 140.2 Psaumes 57.6 Psaumes 89.51
7 Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.Psaumes 55.23 Psaumes 36.12 Ecclésiaste 8.8 Jérémie 10.25 Esaïe 28.15
8 Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)Psaumes 39.12 2 Rois 20.5 Malachie 3.16 Psaumes 139.16 Apocalypse 7.17
9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;Romains 8.31 Psaumes 118.6 Psaumes 102.2 Psaumes 46.11 Jérémie 33.3
10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake.Psaumes 56.4 Genèse 32.11 Hébreux 6.18 2 Pierre 1.4 Matthieu 24.35
11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?Esaïe 51.12-51.13 Psaumes 112.7-112.8 Esaïe 51.7-51.8 Psaumes 27.1
12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.Psaumes 50.14 Psaumes 9.1-9.3 Psaumes 21.13 Psaumes 76.11 Psaumes 66.13-66.14
13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.Psaumes 116.8-116.9 Job 33.30 Genèse 17.1 1 Thessaloniciens 1.10 Psaumes 94.18

Cette Bible est dans le domaine public.