Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 56.11
Bible en Swahili de l’est


1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita.Psaumes 16.1 Psaumes 27.2 Psaumes 69.13-69.16 Psaumes 57.1-57.3 Psaumes 60.1
2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa, Maana waletao vita juu yangu kwa kiburi ni wengi.Psaumes 57.3 Psaumes 118.10-118.12 Daniel 5.18 Esaïe 57.15 Michée 6.6
3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;Psaumes 55.4-55.5 Psaumes 34.4 1 Samuel 30.6 1 Samuel 21.12 2 Corinthiens 7.5-7.6
4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwenye mwili atanitenda nini?Psaumes 118.6 Hébreux 13.6 Psaumes 56.10-56.11 Psaumes 119.160 Psaumes 27.1
5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.2 Pierre 3.16 1 Samuel 20.33 1 Samuel 18.17 Luc 22.3-22.6 Luc 11.54
6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa wameniotea nafsi yangu.Psaumes 59.3 Psaumes 71.10 Psaumes 140.2 Matthieu 27.1 Matthieu 26.57
7 Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.Psaumes 55.23 Habakuk 1.13 Psaumes 55.9 Psaumes 36.12 Ecclésiaste 8.8
8 Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)Psaumes 39.12 2 Rois 20.5 Malachie 3.16 Matthieu 10.30 Psaumes 139.16
9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;Romains 8.31 Psaumes 118.6 Psaumes 102.2 Psaumes 9.3 Esaïe 8.9-8.10
10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake.Psaumes 56.4 Genèse 32.11 Hébreux 6.18 2 Pierre 1.4 Matthieu 24.35
11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?Esaïe 51.12-51.13 Psaumes 112.7-112.8 Esaïe 51.7-51.8 Psaumes 27.1
12 Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru.Psaumes 50.14 Psaumes 9.1-9.3 Psaumes 119.106 Ecclésiaste 5.4-5.6 Nombres 30.2-30.16
13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.Psaumes 116.8-116.9 Job 33.30 Psaumes 86.12-86.13 1 Samuel 2.9 Apocalypse 21.23-21.24

Cette Bible est dans le domaine public.