Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 26.10
Bible en Swahili de l’est


1 Ee Bwana, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini Bwana bila wasiwasi.Psaumes 7.8 Psaumes 28.7 Proverbes 20.7 2 Rois 20.3 1 Corinthiens 4.3-4.6
2 Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu.Psaumes 7.9 Psaumes 17.3 Job 31.4-31.6 Jérémie 20.12 Psaumes 139.23-139.24
3 Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako.2 Rois 20.3 Psaumes 25.5 Psaumes 101.2 Psaumes 52.1 2 Corinthiens 8.9
4 Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki.Psaumes 1.1 Psaumes 119.115 Jérémie 15.17 Proverbes 13.20 Proverbes 9.6
5 Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu.Psaumes 31.6 Psaumes 139.21-139.22 Psaumes 101.3-101.8 1 Corinthiens 5.9-5.11 Psaumes 1.1
6 Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BwanaPsaumes 73.13 Psaumes 43.4 Exode 30.19-30.20 Tite 3.5 Malachie 2.11-2.13
7 Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.Psaumes 9.1 Psaumes 100.4-100.5 Psaumes 116.12-116.14 Psaumes 66.13-66.15 Psaumes 134.2
8 Bwana, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako.Luc 2.49 Jean 2.14-2.17 Esaïe 38.22 Psaumes 84.10 Psaumes 84.1-84.2
9 Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.Psaumes 139.19 Psaumes 55.23 2 Samuel 21.1 2 Samuel 16.7 Matthieu 25.44
10 Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.1 Samuel 8.3 Exode 23.8 Deutéronome 16.19 Amos 5.12 Proverbes 1.16
11 Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili.Psaumes 69.18 Psaumes 26.1 Psaumes 49.7 1 Pierre 1.18-1.19 Néhémie 13.31
12 Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana.Psaumes 27.11 Psaumes 40.2 Psaumes 111.1 Proverbes 10.9 Psaumes 22.22-22.25

Cette Bible est dans le domaine public.