Prière de l’homme intègre
 1  Ee Bwana, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini Bwana bila wasiwasi. 
Psaumes 7.8  Psaumes 28.7  Proverbes 20.7  2 Rois 20.3  Psaumes 37.31  
 2  Ee Bwana, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. 
Psaumes 7.9  Psaumes 17.3  Job 31.4-31.6  Jérémie 20.12  Psaumes 139.23-139.24  
 3  Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako. 
2 Rois 20.3  Ephésiens 4.32-5.2  Psaumes 85.10-85.13  1 Jean 4.19-4.21  Matthieu 5.44-5.48  
 4  Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki. 
Psaumes 1.1  Psaumes 119.115  Jérémie 15.17  Proverbes 9.6  Proverbes 12.11  
 5  Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. 
Psaumes 31.6  Psaumes 139.21-139.22  Psaumes 101.3-101.8  1 Corinthiens 5.9-5.11  Psaumes 1.1  
 6  Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee Bwana 
Psaumes 73.13  Exode 30.19-30.20  Psaumes 43.4  Hébreux 10.19-10.22  Psaumes 24.4  
 7  Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu. 
Psaumes 9.1  Psaumes 95.2  Psaumes 116.18-116.19  Psaumes 119.27  Psaumes 118.19  
 8  Bwana, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. 
Luc 2.49  Jean 2.14-2.17  Exode 40.34-40.35  2 Chroniques 5.14-6.2  Exode 25.21-25.22  
 9  Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu. 
Psaumes 139.19  Matthieu 25.32  Malachie 3.18  Psaumes 28.1-28.3  Matthieu 24.51  
 10  Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa. 
Exode 23.8  Deutéronome 16.19  1 Samuel 8.3  Psaumes 52.2  Michée 7.3  
 11  Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili. 
Psaumes 69.18  Psaumes 26.1  Job 1.1  Psaumes 49.15  2 Chroniques 31.20-31.21  
 12  Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi Bwana. 
Psaumes 27.11  Psaumes 40.2  Proverbes 10.9  Psaumes 111.1  Psaumes 122.4