Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Psaumes 116.16
Bible en Swahili de l’est


1 Haleluya. Nampenda Bwana kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu.1 Jean 4.19 1 Jean 5.2-5.3 Psaumes 66.19-66.20 Jean 21.17 Psaumes 69.33
2 Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote.Luc 18.1 Job 27.10 Psaumes 31.2 Psaumes 40.1 Psaumes 145.18-145.19
3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Naliona taabu na huzuni;Psaumes 38.6 Esaïe 53.3-53.4 Luc 22.44 Hébreux 5.7 Psaumes 18.4-18.6
4 Nikaliitia jina la Bwana. Ee Bwana, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu.Psaumes 118.5 Psaumes 22.20 Psaumes 34.6 2 Chroniques 33.12-33.13 Psaumes 6.4
5 Bwana ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema.Néhémie 9.8 Esdras 9.15 Psaumes 119.137 Psaumes 86.15 Psaumes 145.17
6 Bwana huwalinda wasio na hila; Nalidhilika, akaniokoa.Psaumes 79.8 Psaumes 19.7 Psaumes 142.6 Psaumes 106.43 Matthieu 11.25
7 Ee nafsi yangu, urudi rahani mwako, Kwa kuwa Bwana amekutendea ukarimu.Jérémie 6.16 Psaumes 13.6 Jérémie 30.10 Psaumes 95.11 Matthieu 11.28-11.29
8 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka.Psaumes 56.13 Apocalypse 21.4 Psaumes 86.13 Esaïe 25.8 Esaïe 38.5
9 Nitaenenda mbele za Bwana Katika nchi za walio hai.Psaumes 27.13 Esaïe 53.8 1 Rois 8.25 Genèse 17.1 Luc 1.75
10 Naliamini, kwa maana nitasema, Mimi naliteswa sana.2 Corinthiens 4.13 Proverbes 21.28 Nombres 14.6-14.9 Hébreux 11.1 2 Pierre 1.21
11 Mimi nalisema kwa haraka yangu, Wanadamu wote ni waongo.Psaumes 31.22 Romains 3.4 2 Rois 4.16 Jérémie 9.4-9.5 1 Samuel 27.1
12 Nimrudishie Bwana nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea?Psaumes 103.2 1 Corinthiens 6.20 Romains 12.1 2 Corinthiens 5.14-5.15 2 Chroniques 32.25
13 Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la Bwana;Psaumes 105.1 Psaumes 16.5 Luc 22.20 Psaumes 116.17 Psaumes 116.2
14 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.Psaumes 22.25 Jonas 2.9 Psaumes 116.18 Psaumes 50.14 Psaumes 56.12
15 Ina thamani machoni pa Bwana Mauti ya wacha Mungu wake.Psaumes 72.14 Psaumes 37.32-37.33 Luc 16.22 Apocalypse 1.18 Apocalypse 14.3
16 Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu.Psaumes 86.16 Psaumes 143.12 Psaumes 119.125 2 Chroniques 33.11-33.13 Jean 12.26
17 Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la Bwana;Psaumes 50.14 Lévitique 7.12 Psaumes 116.13 Actes 2.42 Hébreux 13.15
18 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana, Naam, mbele ya watu wake wote.Psaumes 116.14 Psaumes 76.11 Psaumes 22.25 Ecclésiaste 5.5
19 Katika nyua za nyumba ya Bwana, Ndani yako, Ee Yerusalemu.Psaumes 135.2 Psaumes 96.8 Psaumes 100.4 2 Chroniques 6.6 Psaumes 122.3-122.4

Cette Bible est dans le domaine public.