Fermer le panneau de recherche

Appuyez sur Entrée pour rechercher ou ESC pour annuler.

Job 8.12
Bible en Swahili de l’est


1 Ndipo Bildadi huyo Mshuhi akajibu, na kusema,Job 2.11
2 Wewe utanena maneno haya hata lini? Maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo mkuu hata lini?Job 6.26 Job 15.2 1 Rois 19.11 Job 16.3 Exode 10.7
3 Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?2 Chroniques 19.7 Deutéronome 32.4 Genèse 18.25 Daniel 9.14 Job 34.10-34.12
4 Kwamba watoto wako wamemfanyia dhambi, Naye amewatia mkononi mwa kosa lao;Job 1.5 Job 1.18-1.19 Genèse 19.13-19.25 Genèse 13.13 Job 5.4
5 Wewe ukimtafuta Mungu kwa bidii, Na kumsihi huyo Mwenyezi;Job 11.13 Jacques 4.7-4.10 Hébreux 3.7-3.8 Matthieu 7.7-7.8 2 Chroniques 33.12-33.13
6 Ukiwa wewe u safi na mwelekevu; Hakika yeye sasa angeamka kwa ajili yako, Na kuyafanya makazi ya haki yako kufanikiwa.Psaumes 7.6 1 Jean 3.19-3.22 Job 5.24 Job 1.8 Proverbes 15.8
7 Tena ujapokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, Lakini mwisho wako ungeongezeka sana.Job 42.12-42.13 Matthieu 13.31-13.32 Zacharie 4.10 Proverbes 4.18 Matthieu 13.12
8 Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;Job 15.18 Deutéronome 4.32 Deutéronome 32.7 Psaumes 44.1 Job 12.12
9 (Kwani sisi tu wa jana tu, wala hatujui neno, Kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu;)1 Chroniques 29.15 Psaumes 144.4 Job 14.2 Job 7.6 Psaumes 102.11
10 Je! Hawatakufunza wao, na kukueleza, Na kutamka maneno yatokayo mioyoni mwao?Matthieu 12.35 Hébreux 12.1 Job 12.7-12.8 Hébreux 11.4 Proverbes 18.15
11 Je! Hayo mafunjo yamea pasipo matope Na makangaga kumea pasipo maji?Exode 2.3 Esaïe 19.5-19.7
12 Yakiwa yakali mabichi bado, wala hayakukatwa, Hunyauka mbele ya majani mengine.Jérémie 17.6 1 Pierre 1.24 Matthieu 13.20 Jacques 1.10-1.11 Psaumes 129.6-129.7
13 Ndivyo ulivyo mwisho wa hao wamsahauo Mungu; Na matumaini yake huyo mbaya huangamia;Psaumes 9.17 Job 15.34 Job 13.16 Job 11.20 Proverbes 10.28
14 Uthabiti wake utavunjika, Na matumaini yake huwa ni nyuzi za buibui.Esaïe 59.5-59.6
15 Ataitegemea nyumba yake, isisimame; Atashikamana nayo, isidumu.Job 27.18 Matthieu 7.24-7.27 Luc 6.47-6.49 Psaumes 112.10 Psaumes 49.11
16 Yeye huwa mti mbichi mbele ya jua, Nayo machipukizi yake huenea katika bustani yake.Psaumes 80.11 Jérémie 11.16 Psaumes 37.35-37.36 Job 5.3 Job 21.7-21.15
17 Mizizi yake huzonga-zonga chuguu, Huangalia mahali penye mawe.Esaïe 5.24 Marc 11.20 Job 29.19 Esaïe 40.24 Jérémie 12.1-12.2
18 Lakini, aking’olewa mahali pake, Ndipo patamkana, na kusema, Mimi sikukuona.Job 7.10 Job 7.8 Psaumes 37.36 Psaumes 37.10 Job 20.9
19 Tazama, furaha ya njia yake ni hii, Na wengine watachipuka kutoka katika nchi.Job 20.5 1 Samuel 2.8 Psaumes 113.7 Psaumes 75.7 Matthieu 13.20-13.21
20 Tazama, Mungu hatamtupa mtu mkamilifu, Wala hatawathibitisha watendao uovu.Job 4.7 Psaumes 37.24 Esaïe 45.1 Job 9.22 Psaumes 94.14
21 Bado atakijaza kinywa chako kicheko, Na midomo yako ataijaza shangwe.Psaumes 126.2 Genèse 21.6 Esaïe 65.13-65.14 Esdras 3.11-3.13 Psaumes 98.4
22 Hao wakuchukiao watavikwa aibu; Nayo hema yake mwovu haitakuwako tena.Psaumes 109.29 Psaumes 35.26 Psaumes 132.18 Job 8.18 Job 18.14

Cette Bible est dans le domaine public.